---
title: Chemsha bongo
metaTitle: Kuongeza chemsha bongo
description: Sera tunayotumia tunapoongeza chemsha bongo kwenye ethereum.org
lang: sw
---

Chemsha bongo ni fursa kwa watumiaji kujipima ili kuona kama wameelewa maudhui kwenye ukurasa waliomaliza kusoma. Maswali yanapaswa kutegemea tu maudhui yaliyotolewa kwenye ukurasa na hayapaswi kuuliza kuhusu taarifa ambazo hazijatajwa kwenye ukurasa.

Maswali yamepangwa kama ifuatavyo. Swali lenyewe, jibu 1 sahihi pamoja na maelezo ya kwa nini ni sahihi, majibu 3 yasiyo sahihi pamoja na maelezo ya kwa nini si sahihi.

Baadhi ya mifano ya chemsha bongo za sasa inaweza kupatikana hapa:

- [tabaka la 2 (l2)](/layer-2)
- [NFT](/nft/)
- [Ethereum ni nini?](/what-is-ethereum/)
- [ETH ni nini?](/what-is-ether/)

## Kuongeza chemsha bongo ya kujifunza {#adding-a-learn-quiz}

Kama kuna ukurasa ambao haujatengenezewa chemsha bongo ya kujifunza, tafadhali [fungua suala](https://github.com/ethereum/ethereum-org-website/issues/new?assignees=&labels=&template=suggest_quiz.yaml) kwa ajili yake.

Tafadhali toa taarifa zifuatazo:

- Ukurasa unaotaka kuongeza chemsha bongo
- Maswali 5 yenye taarifa zifuatazo:
  - Sehemu ya ukurasa ambayo swali linategemea
  - Swali lenyewe
  - Jibu 1 sahihi pamoja na maelezo ya kwa nini ni sahihi
  - Majibu 3 yasiyo sahihi, kila moja likiwa na maelezo ya kwa nini si sahihi

## Kuongeza swali la chemsha bongo {#adding-a-quiz-question}

Kama kuna swali unalotaka kuongeza kwenye benki ya maswali kwa ajili ya chemsha bongo, tafadhali [fungua suala](https://github.com/ethereum/ethereum-org-website/issues/new?assignees=&labels=&template=suggest_quiz.yaml) na utoe taarifa zifuatazo:

- Ukurasa unaotaka kuongeza swali la chemsha bongo
- Kwa kila swali toa taarifa zifuatazo:
  - Sehemu ya ukurasa ambayo swali linategemea
  - Swali lenyewe
  - Jibu 1 sahihi pamoja na maelezo ya kwa nini ni sahihi
  - Majibu 3 yasiyo sahihi, kila moja likiwa na maelezo ya kwa nini si sahihi

## Kusasisha swali la chemsha bongo {#updating-a-quiz-question}

Kama kuna swali unalotaka kusasisha katika benki ya maswali kwa ajili ya chemsha bongo, tafadhali [fungua suala](https://github.com/ethereum/ethereum-org-website/issues/new?assignees=&labels=&template=suggest_quiz.yaml) na utoe taarifa zifuatazo:

- Ukurasa unaotaka kusasisha swali la chemsha bongo
- Kwa kila swali linalosasishwa, toa taarifa zifuatazo:
  - Sehemu ya ukurasa ambayo swali linategemea
  - Swali lenyewe unalotaka kusasisha
  - Swali lililosasishwa
  - Jibu 1 sahihi pamoja na maelezo ya kwa nini ni sahihi
  - Majibu 3 yasiyo sahihi, kila moja likiwa na maelezo ya kwa nini si sahihi

## Kuondoa swali la chemsha bongo {#removing-a-quiz-question}

Kama maudhui hayapo tena kwenye ukurasa kwa ajili ya swali na linahitaji kuondolewa, tafadhali [fungua suala](https://github.com/ethereum/ethereum-org-website/issues/new?assignees=&labels=&template=suggest_quiz.yaml) ili kuondoa swali na utoe taarifa zifuatazo:

- Ukurasa unaotaka kufuta swali la chemsha bongo
- Swali unalotaka kufuta
- Maelezo kama ni lazima ya kwa nini swali linapaswa kuondolewa