---
title: Miundo ya data na usimbaji
description: Muhtasari wa miundo ya kimsingi ya data ya Ethereum.
lang: sw
sidebarDepth: 2
---

Ethereum huunda, kuhifadhi na kuhamisha viwango vikubwa vya data. Data hii lazima iumbizwe kwa njia sanifu na zinazotumia kumbukumbu vizuri ili kuruhusu mtu yeyote [kuendesha nodi](/run-a-node/) kwenye maunzi ya kawaida ya kiwango cha mtumiaji. Ili kufanikisha hili, miundo kadhaa maalum ya data inatumika kwenye staki ya Ethereum.

## Masharti {#prerequisites}

Unapaswa kuelewa misingi ya Ethereum na [programu ya mteja](/developers/docs/nodes-and-clients/). Uelewa wa tabaka la mtandao na [waraka mweupe wa Ethereum](/whitepaper/) unapendekezwa.

## Miundo ya data {#data-structures}

### Trie za Patricia merkle {#patricia-merkle-tries}

Trie za Patricia Merkle ni miundo inayosimba jozi za ufunguo-thamani kwenye trie thabiti na iliyothibitishwa kwa njia ya kificho. Hizi hutumika sana katika tabaka la utekelezaji la Ethereum.

[Zaidi kuhusu Trie za Patricia Merkle](/developers/docs/data-structures-and-encoding/patricia-merkle-trie)

### Recursive Length Prefix {#recursive-length-prefix}

Recursive Length Prefix (RLP) ni mbinu ya usanjari inayotumika sana katika tabaka la utekelezaji la Ethereum.

[Zaidi kuhusu RLP](/developers/docs/data-structures-and-encoding/rlp)

### Simple Serialize {#simple-serialize}

Simple Serialize (SSZ) ni umbizo kuu la usanjari kwenye tabaka la mwafaka la Ethereum kwa sababu ya utangamano wake na merklelization.

[Zaidi kuhusu SSZ](/developers/docs/data-structures-and-encoding/ssz)