---
title: Ethereum kwa wasanidi wa Dart
description: Jifunze jinsi ya kusanidi kwa ajili ya Ethereum ukitumia lugha ya Dart
lang: sw
incomplete: true
---

## Kuanza na mikataba mahiri na lugha ya Solidity {#getting-started-with-smart-contracts-and-solidity}

## Mafunzo {#tutorials}

- [Flutter na Mnyororo wa vitalu – Dapp ya Hello World](https://www.geeksforgeeks.org/flutter-and-blockchain-hello-world-dapp/) inakupeleka kupitia hatua zote ili kuanza:
  1.  Kuandika mkataba mahiri katika [Solidity](https://soliditylang.org/)
  2.  Kuandika kiolesura cha mtumiaji katika Dart
- [Kujenga dapp ya Simu na Flutter](https://medium.com/dash-community/building-a-mobile-dapp-with-flutter-be945c80315a) ni fupi zaidi, ambayo inaweza kuwa bora ikiwa tayari unajua mambo ya msingi
- Ikiwa unapendelea kujifunza kwa kutazama video, unaweza kutazama [Jenga Programu Yako ya Kwanza ya Flutter ya Mnyororo wa vitalu](https://www.youtube.com/watch?v=3Eeh3pJ6PeA), ambayo ina urefu wa takriban saa moja
- Ikiwa huna subira, unaweza kupendelea [Kujenga Programu tumizi iliyogatuliwa ya Mnyororo wa vitalu na Flutter na Dart kwenye Ethereum](https://www.youtube.com/watch?v=jaMFEOCq_1s), ambayo ni takriban dakika ishirini tu
- [Kuunganisha MetaMask katika programu ya Flutter na Web3Modal na WalletConnect](https://www.youtube.com/watch?v=v_M2buHCpc4) - video hii fupi inakupeleka kupitia hatua za kuunganisha MetaMask kwenye programu zako za Flutter na maktaba ya [Web3Modal](https://pub.dev/packages/web3modal_flutter) ya WalletConnect
- [Kozi ya Kambi ya Mafunzo ya Msanidi wa Mnyororo wa vitalu wa Simu na Solidity & Flutter](https://youtube.com/playlist?list=PL4V4Unlk5luhQ26ERO6hWEbcUwHDSSmVH) - orodha ya kucheza ya kozi ya msanidi wa mnyororo wa vitalu wa simu wa full stack

## Kufanya kazi na wateja wa Ethereum {#working-with-ethereum-clients}

Unaweza kutumia Ethereum kuunda programu tumizi zilizogatuliwa (au "dapps") zinazotumia faida za sarafu-fiche na teknolojia ya mnyororo wa vitalu.
Kuna angalau maktaba mbili zinazodumishwa kwa sasa za Dart ili kutumia [JSON-RPC API](/developers/docs/apis/json-rpc/) kwa ajili ya Ethereum.

1. [Web3dart kutoka pwa.ir](https://pub.dev/packages/web3dart)
1. [Ethereum 5.0.0 kutoka darticulate.com](https://pub.dev/packages/ethereum)

Pia kuna maktaba za ziada zinazokuruhusu kudhibiti anwani maalum za Ethereum, au zinazokuruhusu kupata bei za sarafu-fiche mbalimbali.
[Unaweza kuona orodha kamili hapa](https://pub.dev/dart/packages?q=ethereum).