---
title: Ethereum kwa Wasanidi wa Ruby
description: Jifunze jinsi ya kusanidi Ethereum ukitumia miradi na zana zinazotegemea Ruby.
lang: sw
incomplete: false
---

<FeaturedText>Jifunze jinsi ya kusanidi Ethereum ukitumia miradi na zana zinazotegemea Ruby.</FeaturedText>

Tumia Ethereum kuunda programu tumizi zilizogatuliwa (au "dapps") zinazotumia manufaa ya sarafu-fiche na teknolojia ya mnyororo wa vitalu. Dapps hizi zinaweza kuwa bila hitaji la uaminifu, ikimaanisha kwamba mara tu zinaposambazwa kwenye Ethereum, zitaendeshwa kila wakati kama zilivyopangwa. Zinaweza kudhibiti mali za kidijitali ili kuunda aina mpya za programu za kifedha. Zinaweza kuwa zilizogatuliwa, ikimaanisha kuwa hakuna chombo au mtu mmoja anayezidhibiti na ni karibu haiwezekani kuzidhibiti.

## Kuanza na mikataba mahiri na lugha ya Solidity {#getting-started-with-smart-contracts-and-solidity}

**Chukua hatua zako za kwanza za kuunganisha Ruby na Ethereum**

Je, unahitaji mwongozo wa kimsingi zaidi kwanza? Angalia [ethereum.org/learn](/learn/) au [ethereum.org/developers](/developers/).

- [Mnyororo wa Vitalu Umefafanuliwa](https://kauri.io/article/d55684513211466da7f8cc03987607d5/blockchain-explained)
- [Kuelewa Mikataba Mahiri](https://kauri.io/article/e4f66c6079e74a4a9b532148d3158188/ethereum-101-part-5-the-smart-contract)
- [Andika Mkataba Mahiri wako wa Kwanza](https://kauri.io/article/124b7db1d0cf4f47b414f8b13c9d66e2/remix-ide-your-first-smart-contract)
- [Jifunze Jinsi ya Kukusanya na Kusambaza Solidity](https://kauri.io/article/973c5f54c4434bb1b0160cff8c695369/understanding-smart-contract-compilation-and-deployment)

## Makala ya wanaoanza {#beginner-articles}

- [Hatimaye kuelewa akaunti za Ethereum](https://dev.to/q9/finally-understanding-ethereum-accounts-1kpe)
- [Hatimaye Kuthibitisha Watumiaji wa Rails na MetaMask](https://dev.to/q9/finally-authenticating-rails-users-with-metamask-3fj)
- [Jinsi ya kuunganisha kwenye mtandao wa Ethereum kwa kutumia Ruby](https://www.quicknode.com/guides/web3-sdks/how-to-connect-to-the-ethereum-network-using-ruby)
- [Jinsi ya kuzalisha anwani mpya ya Ethereum katika Ruby](https://www.quicknode.com/guides/web3-sdks/how-to-generate-a-new-ethereum-address-in-ruby)

## Makala ya kati {#intermediate-articles}

- [Programu ya Mnyororo wa Vitalu na Ruby](https://www.nopio.com/blog/blockchain-app-ruby/)
- [Tumia Ruby, iliyounganishwa na Ethereum, kutekeleza Mkataba Mahiri](https://titanwolf.org/Network/Articles/Article?AID=87285822-9b25-49d5-ba2a-7ad95fff7ef9)

## Miradi na zana za Ruby {#ruby-projects-and-tools}

### Inayotumika {#active}

- [eth.rb](https://github.com/q9f/eth.rb) - _Maktaba ya Ruby na mteja wa RPC kushughulikia akaunti, jumbe, na miamala ya Ethereum_
- [keccak.rb](https://github.com/q9f/keccak.rb) - _Heshi ya Keccak (SHA3) inayotumiwa na Ethereum_
- [siwe-ruby](https://github.com/signinwithethereum/siwe-ruby) - _Utekelezaji wa Ruby wa Kuingia na Ethereum (SIWE)_
- [siwe-rails](https://github.com/signinwithethereum/siwe-rails) - _Gem ya Rails inayoongeza njia za kuingia za ndani za SIWE_
- [siwe-rails-examples](https://github.com/signinwithethereum/siwe-rails-examples) - _Mfano wa SIWE unaotumia Ruby on Rails na kidhibiti maalum_
- [omniauth-siwe](https://github.com/signinwithethereum/omniauth-siwe) - _Mkakati wa OmniAuth wa Kuingia na Ethereum (SIWE)_
- [omniauth-nft](https://github.com/valthon/omniauth-nft) - _Mkakati wa OmniAuth wa kuthibitisha kupitia umiliki wa NFT_
- [ethereum-on-rails](https://github.com/q9f/ethereum-on-rails) - _Kiolezo cha Ethereum on Rails kinachoruhusu kuunganisha MetaMask kwenye Ruby on Rails_

### Iliyohifadhiwa / Haidumishwi tena {#archived--no-longer-maintained}

- [web3-eth](https://github.com/spikewilliams/vtada-ethereum) - _Kuita mbinu za RPC za nodi ya Ethereum kwa Ruby_
- [ethereum_tree](https://github.com/longhoangwkm/ethereum_tree) - _Maktaba ya Ruby ya kuzalisha anwani za ETH kutoka kwenye mkoba wa Hierarchical Deterministic kulingana na kiwango cha BIP32_
- [etherlite](https://github.com/budacom/etherlite) - _Ujumuishaji wa Ethereum kwa Ruby on Rails_
- [ethereum.rb](https://github.com/EthWorks/ethereum.rb) - _Mteja wa Ethereum wa Ruby anayetumia kiolesura cha JSON-RPC kwa kutuma miamala, kuunda na kuingiliana na mikataba pamoja na zana muhimu za kufanya kazi na nodi ya Ethereum_
- [omniauth-ethereum.rb](https://github.com/q9f/omniauth-ethereum.rb) - _Inatekeleza mkakati wa mtoa huduma wa Ethereum kwa OmniAuth_

Je, unatafuta rasilimali zaidi? Angalia [ukurasa wetu wa nyumbani wa Wasanidi](/developers/).

## Wachangiaji wa jumuiya ya Ruby {#ruby-community-contributors}

[Kikundi cha Telegram cha Ethereum Ruby](https://t.me/ruby_eth) ni mwenyeji wa jumuiya inayokua kwa kasi na ni rasilimali maalum kwa majadiliano kuhusu mradi wowote kati ya iliyo hapo juu na mada zinazohusiana.