---
title: Miongozo ya Ethereum
description: Mkusanyiko wa miongozo ya vitendo inayoelezea misingi ya kutumia Ethereum kwa wanaoanza.
lang: sw
---

Je, unataka kuanza safari yako ya Ethereum? Miongozo yetu ya vitendo inakuongoza hatua kwa hatua kuhusu jinsi ya kuanza, na kurahisisha kutumia teknolojia hii mpya.

## Kuanza {#getting-started}

1. [Jinsi ya "kuunda" akaunti ya Ethereum](/guides/how-to-create-an-ethereum-account/) - Mtu yeyote anaweza kuunda mkoba bila malipo. Mwongozo huu utakuonyesha wapi pa kuanzia.

2. [Jinsi ya kutumia mkoba](/guides/how-to-use-a-wallet/) - Jifunze jinsi ya kutuma na kupokea tokeni kwenye mkoba wako na jinsi ya kuunganisha mkoba kwenye miradi.

## Misingi ya usalama {#security-basics}

1. [Jinsi ya kubatilisha ufikiaji wa mkataba mahiri kwenye fedha zako za kripto](/guides/how-to-revoke-token-access/) - Ikiwa ghafla utaona muamala kwenye mkoba wako ambao hukuanzisha, mwongozo huu utakufundisha jinsi ya kuzuia hilo lisitokee tena.

2. [Jinsi ya kutambua tokeni za utapeli](/guides/how-to-id-scam-tokens/) - Tokeni za utapeli ni nini? Je, zinajifanyaje kuonekana halali, na unazitambuaje ili kujilinda na kuepuka kutapeliwa?

## Kutumia Ethereum {#using-ethereum}

1. [Jinsi ya kuvusha tokeni kwenye tabaka la 2 (l2)](/guides/how-to-use-a-bridge/) - Je, miamala ya Ethereum ni ya gharama kubwa sana? Fikiria kuhamia kwenye suluhisho za kuongeza uwezo za Ethereum zinazoitwa tabaka la 2 (l2).

2. [Jinsi ya kubadilisha tokeni](/guides/how-to-swap-tokens/) - Je, unataka kubadilisha tokeni zako kwa nyingine tofauti? Mwongozo huu rahisi utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.