---
title: Jinsi ya kubadilisha tokeni
description: Mwongozo wa jinsi ya kubadilisha tokeni kwenye Ethereum.
lang: sw
---

Je, umechoka kutafuta soko la kubadilishia fedha ambalo linaorodhesha tokeni zako zote unazozipenda? Unaweza kubadilisha tokeni nyingi ukitumia [masoko yaliyogatuliwa](/glossary/#dex).

Badilishano la tokeni linahusisha ubadilishanaji wa rasilimali mbili tofauti zilizopo kwenye mtandao wa Ethereum, kwa mfano kubadilisha ETH kwa DAI (tokeni ya [ERC-20](/glossary/#erc-20)). Mchakato huu ni wa haraka sana na wa bei nafuu. Utahitaji kuwa na mkoba wa kripto ili kubadilisha tokeni.

**Mahitaji ya awali:**

- kuwa na [mkoba wa kripto](/glossary/#wallet); kama huna, unaweza kufuata mwongozo huu kuhusu [jinsi ya kuunda akaunti ya Ethereum](/guides/how-to-create-an-ethereum-account/)
- kuongeza fedha kwenye mkoba wako

## 1. Unganisha mkoba wako kwenye soko lililogatuliwa (DEX) unalolipendelea {#1-connect-your-wallet-to-the-decentralized-exchange-dex-of-your-choice}

Baadhi ya masoko maarufu ni:

- [Uniswap](https://app.uniswap.org/#/swap)
- [Sushiswap](https://www.sushi.com/swap)
- [1Inch](https://app.1inch.io/#/1/unified/swap/ETH/DAI)
- [Curve](https://www.curve.finance/dex/ethereum/swap/)

Inavutia? Jifunze zaidi kuhusu nini maana ya [fedha zilizogatuliwa (DeFi)](/defi/) na jinsi aina hizi mpya za masoko zinavyofanya kazi.

## 2. Chagua jozi ya tokeni unazotaka kubadilisha {#2-select-the-pair-of-tokens-you-wish-to-swap}

Kwa mfano, ETH na DAI. Hakikisha una fedha katika mojawapo ya tokeni hizo mbili.
![Common interface for swapping](./swap1.png)

## 3. Weka kiasi cha tokeni unachotaka kufanyia biashara na ubofye badilisha {#3-enter-the-amount-of-tokens-you-want-to-trade-and-click-swap}

Soko litahesabu kiotomatiki ni tokeni ngapi utapata.

![Common interface for swapping](./swap2.png)

## 4. Thibitisha muamala {#4-confirm-the-transaction}

Kagua maelezo ya muamala. Angalia kiwango cha ubadilishaji na ada nyingine zozote ili kuzuia mshangao mbaya.

![Common interface for reviewing the transaction](./swap3.png)

## 5. Subiri muamala uchakatwe {#5-wait-for-the-transaction-to-be-processed}

Unaweza kutazama maendeleo ya muamala kwenye kichunguzi chochote cha mnyororo wa vitalu. Mchakato huu haupaswi kuchukua zaidi ya dakika 10.

Utapokea kiotomatiki tokeni zilizobadilishwa kwenye mkoba wako mara tu muamala utakapochakatwa.
<br />

<Alert variant="update">
<AlertEmoji text=":eyes:"/>
<AlertContent className="justify-between flex-row items-center">
  <div>Unataka kujifunza zaidi?</div>
  <ButtonLink href="/guides/">
    Tazama miongozo yetu mingine
  </ButtonLink>
</AlertContent>
</Alert>

## Maswali yanayoulizwa mara kwa mara {#frequently-asked-questions}

### Je, ninaweza kubadilisha ETH kwa BTC kutoka kwenye mkoba wangu? {#can-i-swap-eth-for-btc-from-my-wallet}

Hapana, unaweza tu kubadilisha tokeni ambazo ni asili ya mtandao wa Ethereum, kama vile ETH, tokeni za ERC-20 au NFT. Unaweza tu kubadilisha aina za Bitcoin "zilizofungwa" ambazo zipo kwenye Ethereum.

### Nini maana ya tofauti ya utekelezaji? {#what-is-slippage}

Ni tofauti kati ya kiwango chako cha ubadilishaji ulichotarajia na kiwango halisi.
