Jinsi ya kuunda na kujaribu dapp kwenye mtandao wa majaribio wa ndani, wa wateja wengi
Utangulizi
Mwongozo huu unakuelekeza katika mchakato wa kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum unaoweza kusanidiwa, kusambaza mkataba mahiri kwake, na kutumia mtandao wa majaribio kuendesha majaribio dhidi ya programu tumizi iliyogatuliwa (dapp) yako. Mwongozo huu umeundwa kwa ajili ya wasanidi wa dapp wanaotaka kuunda na kujaribu dapp zao ndani ya nchi dhidi ya usanidi tofauti wa mtandao kabla ya kusambaza kwenye mtandao wa majaribio wa moja kwa moja au Mtandao Mkuu.
Katika mwongozo huu, uta:
- Kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum na
eth-network-package(opens in a new tab) ukitumia Kurtosis (opens in a new tab), - Kuunganisha mazingira yako ya uundaji wa dapp ya Hardhat kwenye mtandao wa majaribio wa ndani ili kukusanya, kusambaza, na kujaribu dapp, na
- Kusanidi mtandao wa majaribio wa ndani, ikijumuisha vigezo kama vile idadi ya nodi na uoanishaji maalum wa wateja wa EL/CL, ili kuwezesha mtiririko wa kazi wa uundaji na majaribio dhidi ya usanidi mbalimbali wa mtandao.
Kurtosis ni nini?
Kurtosis (opens in a new tab) ni mfumo wa ujenzi unaoweza kuunganishwa ulioundwa kwa ajili ya kusanidi mazingira ya majaribio ya kontena nyingi. Huwawezesha wasanidi programu haswa kuunda mazingira yanayoweza kuzalishwa tena ambayo yanahitaji mantiki ya usanidi inayobadilika, kama vile mitandao ya majaribio ya mnyororo wa vitalu.
Katika mwongozo huu, kifurushi cha mtandao cha eth cha Kurtosis kinaanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum kwa usaidizi wa mteja wa tabaka la utekelezaji (EL) wa geth (opens in a new tab), pamoja na wateja wa tabaka la mwafaka (CL) wa teku (opens in a new tab), lighthouse (opens in a new tab), na lodestar (opens in a new tab). Kifurushi hiki hutumika kama mbadala unaoweza kusanidiwa na unaoweza kuunganishwa kwa mitandao katika mifumo kama vile Hardhat Network, Ganache, na Anvil. Kurtosis inawapa wasanidi udhibiti mkubwa na unyumbufu juu ya mitandao ya majaribio wanayotumia, ambayo ni sababu kuu kwa nini Taasisi ya Ethereum ilitumia Kurtosis kujaribu Unganisho (opens in a new tab) na inaendelea kuitumia kwa majaribio ya uboreshaji wa mtandao.
Kusanidi Kurtosis
Kabla ya kuendelea, hakikisha una:
- Umesakinisha na kuanzisha injini ya Docker (opens in a new tab) kwenye mashine yako ya ndani
- Umesakinisha Kurtosis CLI (opens in a new tab) (au umeiboresha hadi toleo la hivi punde, ikiwa tayari umesakinisha CLI)
- Umesakinisha Node.js (opens in a new tab), yarn (opens in a new tab), na npx (opens in a new tab) (kwa mazingira yako ya dapp)
Kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum
Ili kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum, endesha:
kurtosis --enclave local-eth-testnet run github.com/kurtosis-tech/eth-network-package
Kumbuka: Amri hii inaupa jina mtandao wako: "local-eth-testnet” kwa kutumia alama ya --enclave.
Kurtosis itachapisha hatua inazochukua kiufundi inapofanya kazi kutafsiri, kuthibitisha, na kisha kutekeleza maagizo. Mwishoni, unapaswa kuona matokeo yanayofanana na yafuatayo:
INFO[2023-04-04T18:09:44-04:00] ======================================================
INFO[2023-04-04T18:09:44-04:00] || Created enclave: local-eth-testnet ||
INFO[2023-04-04T18:09:44-04:00] ======================================================
Name: local-eth-testnet
UUID: 39372d756ae8
Status: RUNNING
Creation Time: Tue, 04 Apr 2023 18:09:03 EDT
========================================= Files Artifacts =========================================
UUID Name
d4085a064230 cl-genesis-data
1c62cb792e4c el-genesis-data
bd60489b73a7 genesis-generation-config-cl
b2e593fe5228 genesis-generation-config-el
d552a54acf78 geth-prefunded-keys
5f7e661eb838 prysm-password
054e7338bb59 validator-keystore-0
========================================== User Services ==========================================
UUID Name Ports Status
e20f129ee0c5 cl-client-0-beacon http: 4000/tcp -> <http://127.0.0.1:54261> RUNNING
metrics: 5054/tcp -> <http://127.0.0.1:54262>
tcp-discovery: 9000/tcp -> 127.0.0.1:54263
udp-discovery: 9000/udp -> 127.0.0.1:60470
a8b6c926cdb4 cl-client-0-validator http: 5042/tcp -> 127.0.0.1:54267 RUNNING
metrics: 5064/tcp -> <http://127.0.0.1:54268>
d7b802f623e8 el-client-0 engine-rpc: 8551/tcp -> 127.0.0.1:54253 RUNNING
rpc: 8545/tcp -> 127.0.0.1:54251
tcp-discovery: 30303/tcp -> 127.0.0.1:54254
udp-discovery: 30303/udp -> 127.0.0.1:53834
ws: 8546/tcp -> 127.0.0.1:54252
514a829c0a84 prelaunch-data-generator-1680646157905431468 <none> STOPPED
62bd62d0aa7a prelaunch-data-generator-1680646157915424301 <none> STOPPED
05e9619e0e90 prelaunch-data-generator-1680646157922872635 <none> STOPPED
Hongera! Umetumia Kurtosis kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum, ukiwa na mteja wa CL (lighthouse) na EL (geth), kupitia Docker.
Mapitio
Katika sehemu hii, ulitekeleza amri iliyoelekeza Kurtosis kutumia eth-network-package iliyopangishwa kwa mbali kwenye GitHub (opens in a new tab) ili kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum ndani ya Enclave (opens in a new tab) ya Kurtosis. Ndani ya enclave yako, utapata "file artifacts" na "user services".
File Artifacts (opens in a new tab) katika enclave yako inajumuisha data yote iliyozalishwa na kutumika kuanzisha wateja wa EL na CL. Data iliundwa kwa kutumia huduma ya prelaunch-data-generator iliyojengwa kutoka kwa taswira hii ya Docker (opens in a new tab)
Huduma za mtumiaji zinaonyesha huduma zote zilizowekwa kwenye kontena zinazofanya kazi katika enclave yako. Utagundua kuwa nodi moja, inayoangazia mteja wa EL na mteja wa CL, imeundwa.
Unganisha mazingira yako ya uundaji wa dapp kwenye mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum
Sanidi mazingira ya uundaji wa dapp
Kwa kuwa sasa una mtandao wa majaribio wa ndani unaofanya kazi, unaweza kuunganisha mazingira yako ya uundaji wa dapp ili kutumia mtandao wako wa majaribio wa ndani. Mfumo wa Hardhat utatumika katika mwongozo huu kusambaza dapp ya blackjack kwenye mtandao wako wa majaribio wa ndani.
Ili kusanidi mazingira yako ya uundaji wa dapp, nakili hazina iliyo na sampuli yetu ya dapp na usakinishe vitegemezi vyake, endesha:
git clone https://github.com/kurtosis-tech/awesome-kurtosis.git && cd awesome-kurtosis/smart-contract-example && yarn
Folda ya smart-contract-example (opens in a new tab) inayotumika hapa ina usanidi wa kawaida kwa msanidi wa dapp anayetumia mfumo wa Hardhat (opens in a new tab):
contracts/(opens in a new tab) ina mikataba mahiri michache rahisi kwa dapp ya Blackjackscripts/(opens in a new tab) ina hati ya kusambaza mkataba wa tokeni kwenye mtandao wako wa ndani wa Ethereumtest/(opens in a new tab) ina jaribio rahisi la .js kwa mkataba wako wa tokeni ili kuthibitisha kila mchezaji katika dapp yetu ya Blackjack ana 1000 zilizotengenezwa kwa ajili yaohardhat.config.ts(opens in a new tab) inasanidi usanidi wako wa Hardhat
Sanidi Hardhat kutumia mtandao wa majaribio wa ndani
Ukiwa na mazingira yako ya uundaji wa dapp yaliyosanidiwa, sasa utaunganisha Hardhat ili kutumia mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum uliotengenezwa kwa kutumia Kurtosis. Ili kukamilisha hili, badilisha <$YOUR_PORT> katika muundo wa localnet kwenye faili yako ya usanidi ya hardhat.config.ts na lango la matokeo ya rpc uri kutoka kwa huduma yoyote ya el-client-<num>. Katika sampuli hii, lango litakuwa 64248. Lango lako litakuwa tofauti.
Mfano katika hardhat.config.ts:
localnet: {
url: 'http://127.0.0.1:<$YOUR_PORT>',// TODO: BADILISHA $YOUR_PORT NA LANGO LA URI YA NODI ILIYOZALISHWA NA KIFURUSHI CHA KURTOSIS CHA MTANDAO WA ETH
// Hizi ni funguo za siri zinazohusiana na akaunti za majaribio zilizowekewa fedha mapema zilizoundwa na eth-network-package
// <https://github.com/kurtosis-tech/eth-network-package/blob/main/src/prelaunch_data_generator/genesis_constants/genesis_constants.star>
accounts: [
"ef5177cd0b6b21c87db5a0bf35d4084a8a57a9d6a064f86d51ac85f2b873a4e2",
"48fcc39ae27a0e8bf0274021ae6ebd8fe4a0e12623d61464c498900b28feb567",
"7988b3a148716ff800414935b305436493e1f25237a2a03e5eebc343735e2f31",
"b3c409b6b0b3aa5e65ab2dc1930534608239a478106acf6f3d9178e9f9b00b35",
"df9bb6de5d3dc59595bcaa676397d837ff49441d211878c024eabda2cd067c9f",
"7da08f856b5956d40a72968f93396f6acff17193f013e8053f6fbb6c08c194d6",
],
},
Mara tu unapohifadhi faili yako, mazingira yako ya uundaji wa dapp ya Hardhat sasa yameunganishwa kwenye mtandao wako wa majaribio wa ndani wa Ethereum! Unaweza kuthibitisha kuwa mtandao wako wa majaribio unafanya kazi kwa kuendesha:
npx hardhat balances --network localnet
Matokeo yanapaswa kuonekana kama hivi:
0x878705ba3f8Bc32FCf7F4CAa1A35E72AF65CF766 has balance 10000000000000000000000000
0x4E9A3d9D1cd2A2b2371b8b3F489aE72259886f1A has balance 10000000000000000000000000
0xdF8466f277964Bb7a0FFD819403302C34DCD530A has balance 10000000000000000000000000
0x5c613e39Fc0Ad91AfDA24587e6f52192d75FBA50 has balance 10000000000000000000000000
0x375ae6107f8cC4cF34842B71C6F746a362Ad8EAc has balance 10000000000000000000000000
0x1F6298457C5d76270325B724Da5d1953923a6B88 has balance 10000000000000000000000000
Hii inathibitisha kuwa Hardhat inatumia mtandao wako wa majaribio wa ndani na inatambua akaunti zilizofadhiliwa mapema zilizoundwa na eth-network-package.
Sambaza na ujaribu dapp yako ndani ya nchi
Huku mazingira ya uundaji wa dapp yakiwa yameunganishwa kikamilifu kwenye mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum, sasa unaweza kuendesha mtiririko wa kazi wa uundaji na majaribio dhidi ya dapp yako ukitumia mtandao wa majaribio wa ndani.
Ili kukusanya na kusambaza mkataba mahiri wa ChipToken.sol kwa ajili ya uundaji wa mfano na uundaji wa ndani, endesha:
npx hardhat compile
npx hardhat run scripts/deploy.ts --network localnet
Matokeo yanapaswa kuonekana kama:
ChipToken deployed to: 0xAb2A01BC351770D09611Ac80f1DE076D56E0487d
Sasa jaribu kuendesha jaribio la simple.js dhidi ya dapp yako ya ndani ili kuthibitisha kila mchezaji katika dapp yetu ya Blackjack ana 1000 zilizotengenezwa kwa ajili yao:
Matokeo yanapaswa kuonekana kama hivi:
npx hardhat test --network localnet
Matokeo yanapaswa kuonekana kama hivi:
ChipToken
mint
✔ should mint 1000 chips for PLAYER ONE
1 passing (654ms)
Mapitio
Kufikia hapa, sasa umesanidi mazingira ya uundaji wa dapp, ukayaunganisha kwenye mtandao wa ndani wa Ethereum ulioundwa na Kurtosis, na umekusanya, kusambaza, na kuendesha jaribio rahisi dhidi ya dapp yako.
Sasa hebu tuchunguze jinsi unavyoweza kusanidi mtandao wa msingi kwa ajili ya kujaribu dapp zetu chini ya usanidi tofauti wa mtandao.
Kusanidi mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum
Kubadilisha usanidi wa mteja na idadi ya nodi
Mtandao wako wa majaribio wa ndani wa Ethereum unaweza kusanidiwa kutumia jozi tofauti za wateja wa EL na CL, pamoja na idadi tofauti ya nodi, kulingana na hali na usanidi maalum wa mtandao unaotaka kuunda au kujaribu. Hii inamaanisha kuwa, ukishasanidiwa, unaweza kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani uliobinafsishwa na kuutumia kuendesha mtiririko wa kazi sawa (usambazaji, majaribio, n.k.) chini ya usanidi mbalimbali wa mtandao ili kuhakikisha kila kitu kinafanya kazi kama inavyotarajiwa. Ili kujifunza zaidi kuhusu vigezo vingine unavyoweza kurekebisha, tembelea kiungo hiki.
Ijaribu! Unaweza kupitisha chaguo mbalimbali za usanidi kwa eth-network-package kupitia faili ya JSON. Faili hii ya JSON ya vigezo vya mtandao hutoa usanidi maalum ambao Kurtosis itatumia kusanidi mtandao wa ndani wa Ethereum.
Chukua faili ya usanidi chaguomsingi na uihariri ili kuanzisha nodi mbili zilizo na jozi tofauti za EL/CL:
- Nodi 1 yenye
geth/lighthouse - Nodi 2 yenye
geth/lodestar - Nodi 3 yenye
geth/teku
Usanidi huu unaunda mtandao tofauti wa utekelezaji wa nodi za Ethereum kwa ajili ya kujaribu dapp yako. Faili yako ya usanidi sasa inapaswa kuonekana kama:
{
"participants":
[
{
"el_client_type": "geth",
"el_client_image": "",
"el_client_log_level": "",
"cl_client_type": "lighthouse",
"cl_client_image": "",
"cl_client_log_level": "",
"beacon_extra_params": [],
"el_extra_params": [],
"validator_extra_params": [],
"builder_network_params": null,
},
{
"el_client_type": "geth",
"el_client_image": "",
"el_client_log_level": "",
"cl_client_type": "lodestar",
"cl_client_image": "",
"cl_client_log_level": "",
"beacon_extra_params": [],
"el_extra_params": [],
"validator_extra_params": [],
"builder_network_params": null,
},
{
"el_client_type": "geth",
"el_client_image": "",
"el_client_log_level": "",
"cl_client_type": "teku",
"cl_client_image": "",
"cl_client_log_level": "",
"beacon_extra_params": [],
"el_extra_params": [],
"validator_extra_params": [],
"builder_network_params": null,
},
],
"network_params":
{
"preregistered_validator_keys_mnemonic": "giant issue aisle success illegal bike spike question tent bar rely arctic volcano long crawl hungry vocal artwork sniff fantasy very lucky have athlete",
"num_validator_keys_per_node": 64,
"network_id": "3151908",
"deposit_contract_address": "0x4242424242424242424242424242424242424242",
"seconds_per_slot": 12,
"genesis_delay": 120,
"capella_fork_epoch": 5,
},
}
Kila muundo wa participants unalingana na nodi katika mtandao, kwa hivyo miundo 3 ya participants itaiambia Kurtosis kuanzisha nodi 3 katika mtandao wako. Kila muundo wa participants utakuruhusu kubainisha jozi ya EL na CL inayotumika kwa nodi hiyo maalum.
Muundo wa network_params unasanidi mipangilio ya mtandao inayotumika kuunda faili za mwanzo kwa kila nodi pamoja na mipangilio mingine kama vile sekunde kwa kila sloti ya mtandao.
Hifadhi faili yako ya vigezo iliyohaririwa katika saraka yoyote unayotaka (katika mfano hapa chini, imehifadhiwa kwenye eneo-kazi) na kisha uitumie kuendesha kifurushi chako cha Kurtosis kwa kuendesha:
kurtosis clean -a && kurtosis run --enclave local-eth-testnet github.com/kurtosis-tech/eth-network-package "$(cat ~/eth-network-params.json)"
Kumbuka: amri ya kurtosis clean -a inatumika hapa kuelekeza Kurtosis kuharibu mtandao wa majaribio wa zamani na yaliyomo kabla ya kuanzisha mpya.
Tena, Kurtosis itafanya kazi kwa muda na kuchapisha hatua za kibinafsi zinazofanyika. Hatimaye, matokeo yanapaswa kuonekana kama:
Starlark code successfully run. No output was returned.
INFO[2023-04-07T11:43:16-04:00] ==========================================================
INFO[2023-04-07T11:43:16-04:00] || Created enclave: local-eth-testnet ||
INFO[2023-04-07T11:43:16-04:00] ==========================================================
Name: local-eth-testnet
UUID: bef8c192008e
Status: RUNNING
Creation Time: Fri, 07 Apr 2023 11:41:58 EDT
========================================= Files Artifacts =========================================
UUID Name
cc495a8e364a cl-genesis-data
7033fcdb5471 el-genesis-data
a3aef43fc738 genesis-generation-config-cl
8e968005fc9d genesis-generation-config-el
3182cca9d3cd geth-prefunded-keys
8421166e234f prysm-password
d9e6e8d44d99 validator-keystore-0
23f5ba517394 validator-keystore-1
4d28dea40b5c validator-keystore-2
========================================== User Services ==========================================
UUID Name Ports Status
485e6fde55ae cl-client-0-beacon http: 4000/tcp -> http://127.0.0.1:65010 RUNNING
metrics: 5054/tcp -> http://127.0.0.1:65011
tcp-discovery: 9000/tcp -> 127.0.0.1:65012
udp-discovery: 9000/udp -> 127.0.0.1:54455
73739bd158b2 cl-client-0-validator http: 5042/tcp -> 127.0.0.1:65016 RUNNING
metrics: 5064/tcp -> http://127.0.0.1:65017
1b0a233cd011 cl-client-1-beacon http: 4000/tcp -> 127.0.0.1:65021 RUNNING
metrics: 8008/tcp -> 127.0.0.1:65023
tcp-discovery: 9000/tcp -> 127.0.0.1:65024
udp-discovery: 9000/udp -> 127.0.0.1:56031
validator-metrics: 5064/tcp -> 127.0.0.1:65022
949b8220cd53 cl-client-1-validator http: 4000/tcp -> 127.0.0.1:65028 RUNNING
metrics: 8008/tcp -> 127.0.0.1:65030
tcp-discovery: 9000/tcp -> 127.0.0.1:65031
udp-discovery: 9000/udp -> 127.0.0.1:60784
validator-metrics: 5064/tcp -> 127.0.0.1:65029
c34417bea5fa cl-client-2 http: 4000/tcp -> 127.0.0.1:65037 RUNNING
metrics: 8008/tcp -> 127.0.0.1:65035
tcp-discovery: 9000/tcp -> 127.0.0.1:65036
udp-discovery: 9000/udp -> 127.0.0.1:63581
e19738e6329d el-client-0 engine-rpc: 8551/tcp -> 127.0.0.1:64986 RUNNING
rpc: 8545/tcp -> 127.0.0.1:64988
tcp-discovery: 30303/tcp -> 127.0.0.1:64987
udp-discovery: 30303/udp -> 127.0.0.1:55706
ws: 8546/tcp -> 127.0.0.1:64989
e904687449d9 el-client-1 engine-rpc: 8551/tcp -> 127.0.0.1:64993 RUNNING
rpc: 8545/tcp -> 127.0.0.1:64995
tcp-discovery: 30303/tcp -> 127.0.0.1:64994
udp-discovery: 30303/udp -> 127.0.0.1:58096
ws: 8546/tcp -> 127.0.0.1:64996
ad6f401126fa el-client-2 engine-rpc: 8551/tcp -> 127.0.0.1:65003 RUNNING
rpc: 8545/tcp -> 127.0.0.1:65001
tcp-discovery: 30303/tcp -> 127.0.0.1:65000
udp-discovery: 30303/udp -> 127.0.0.1:57269
ws: 8546/tcp -> 127.0.0.1:65002
12d04a9dbb69 prelaunch-data-generator-1680882122181135513 <none> STOPPED
5b45f9c0504b prelaunch-data-generator-1680882122192182847 <none> STOPPED
3d4aaa75e218 prelaunch-data-generator-1680882122201668972 <none> STOPPED
Hongera! Umefanikiwa kusanidi mtandao wako wa majaribio wa ndani kuwa na nodi 3 badala ya 1. Ili kuendesha mtiririko wa kazi sawa na uliofanya hapo awali dhidi ya dapp yako (kusambaza na kujaribu), fanya shughuli sawa na tulizofanya hapo awali kwa kubadilisha <$YOUR_PORT> katika muundo wa localnet kwenye faili yako ya usanidi ya hardhat.config.ts na lango la matokeo ya rpc uri kutoka kwa huduma yoyote ya el-client-<num> katika mtandao wako mpya wa majaribio wa ndani wa nodi 3.
Hitimisho
Na ndivyo hivyo! Ili kurejelea mwongozo huu mfupi, wewe:
- Umeunda mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum kupitia Docker ukitumia Kurtosis
- Umeunganisha mazingira yako ya uundaji wa dapp ya ndani kwenye mtandao wa ndani wa Ethereum
- Umesambaza dapp na kuendesha jaribio rahisi dhidi yake kwenye mtandao wa ndani wa Ethereum
- Umesanidi mtandao wa msingi wa Ethereum kuwa na nodi 3
Tungependa kusikia kutoka kwako kuhusu kile kilichokwenda vizuri kwako, kile kinachoweza kuboreshwa, au kujibu maswali yako yoyote. Usisite kuwasiliana kupitia GitHub (opens in a new tab) au tutumie barua pepe (opens email client)!
Mifano na miongozo mingine
Tunakuhimiza uangalie mwongozo wetu wa kuanza haraka (opens in a new tab) (ambapo utajenga hifadhidata ya Postgres na API juu yake) na mifano yetu mingine katika hazina yetu ya awesome-kurtosis (opens in a new tab) ambapo utapata mifano mizuri, ikijumuisha vifurushi vya:
- Kuanzisha mtandao wa majaribio wa ndani wa Ethereum sawa (opens in a new tab), lakini ukiwa na huduma za ziada zilizounganishwa kama vile mtumaji taka wa miamala (ili kuiga miamala), kichunguzi cha mchepuo, na mfano uliounganishwa wa Grafana na Prometheus
- Kufanya jaribio la mtandao mdogo (opens in a new tab) dhidi ya mtandao wa ndani wa Ethereum sawa