Ruka kwenda kwenye maudhui makuu
Mfano wa mji wa baadaye, unaowakilisha ikolojia ya Ethereum.

Karibu Ethereum

Ethereum ni teknolojia inayoendeshwa na jamii inayoipa nguvu ether ya sarafu ya kripto (ETH) na maelfu ya programu zisizotegemea benki za kiserikali.

Chunguza Ethereum

Anza

ethereum.org ni mlango wako wa kuingia katika ulimwengu wa Ethereum. Teknolojia hii ni mpya na inayoendelea kubadilika – ni vizuri kuwa na mwongozo. Haya hapa ndiyo tunayopendekeza ufanye ikiwa unataka kuzama ndani.
Kielelezo cha mtu anayefanya kazi kwenye tarakilishi.

Ethereum ni nini?

Ethereum ni teknolojia ambayo ni nyumbani kwa hela ya kidijitali, malipo ya kimataifa, na programu. Jamii hii imejenga uchumi wa kidijitali unaoongezeka kwa kasi, njia mpya za kijasiri zinazowawezesha waundaji kupata kipato mtandaoni na mengine mengi. Jamii hii iko wazi kwa kila mtu, popote ulipo ulimwenguni - unachohitaji ni mtandao.
Ethereum ni nini?Zaidi juu ya pesa za dijitali
Kielelezo cha mtu akichungulia ndani ya duka, lenye malengo ya kuwakilisha Ethereum.

Mfumo wenye haki za kifedha

Leo hii, mabilioni ya watu hawawezi kufungua akaunti za benki, wengine wamefungiwa malipo yao. Mfumo wa ethereum usiotegemea benki wala serikali ya nchi (DeFi) haulali wala haubagui. Ukiwa umeunganishwa mtandaoni tu, unaweza kutuma, kupokea, kukopa, kupata riba na hata kuweka hela katika mikondo mbalimbali popote ulimwenguni.
Kielelezo cha mikono ikitoa alama ya ETH.

Mtandao wa mali

Ethereum sii kwa ajili ya pesa za dijiti peke yake. Chochote unachoweza kumiliki kinaweza kuwakilishwa, kuuzwa/kununua, na kutumika ipasvyo kama ishara isiyo ya kuvu.(NFTs). Unaweza ukaweka sanaa yako kama ishara na kupata mrabaha moja kwa moja kila inapouzwa tena. Au tumia ishara hio kwa kitu unachomiliki na kupewa mkopo. Uwezekano unakua kila wakati.
Nembo ya Eth ikionyeshwa kwa kupitia hologramu.

Mtandao ulio wazi

Leo, tunapata huduma ya mtandao ya "bure" kwa kutoa udhibiti wa data yetu ya binafsi. Huduma za Ethereum zimefunguliwa kwa msingi - unahitaji pochi tu. Pochi hizi ni za bure na rahisi kuanzisha, kudhibitiwa na wewe, na kufanya kazi bila maelezo yoyote binafsi.
Kielelezo cha tarakilishi ya baadaye, inayowezeshwa na vifuwele vya Ethereum.
Mifano ya misimbo
Benki unayomiliki
Unaweza kujenga benki inayoendeshwa na mantiki uliyoprogramu.
Fedha unayoimiliki
Unaweza kuunda ishara ambayo unaweza kuisafirisha na kuitumia kutoka upande mmoja hadi mwingine wa programu tofauti.
Pochi ya JavaScript Ethereum
Unaweza kutumia lugha zilizopo kuwasiliana na Ethereum na programu nyingine.
Mfumo wa jina la kikoa ulio huru, wala hauhitaji ruhusa
Unaweza kufikiria tena huduma zilizopo kama matumizi yaliyowekwa wazi katika programu mbalimbali.

Mpaka mpya wa maendeleo

Ethereum na programu zake ni huria na zinapatikana katika vyanzo vinavyofunguka. Unaweza kutengeneza msimbo mpya na kutumia vipengele ambavyo wengine waliunda. Kama hutaki kujifunza lugha mpya unaweza kupitia msimbo huria kwa JavaScript na lugha nyingine zilizopo.

Leo katika Ethereum

Takwimu za hivi karibuni za mtandao

Total ETH staked

Jumla ya kiasi cha ETH inayowekwa kwenye hisa kwa sasa na kulinda mtandao.

31.66M

Shughuli za leo

Idadi ya shughuli zilizofanikwa kusindikwa kwenye mtandao ndani ya saa 24 zilizopita.

1.178M

Thamani iliofungwa kwenye DeFi(USD)

Kiasi cha pesa kilichopo kwenye programu zisizotegemea madaraka (DeFi), uchumi wa dijiti wa Ethereum.

US$ 122.5B

Nodi

Ethereum inawezeshwa na maelfu ya watu wanaojitolea ulimwenguni kote, wajulikanao kama nodi.

7,596

Jiunge na jumuiya ya ethereum.org

Jiunge na karibu wanachama 40 000 kwenye seva yetu ya Discord(opens in a new tab).

Jiunge kila mwezi na jumuiya yetu kupata taarifa za kusisimua kuhusu maendeleo na habari muhimu za ikolojia kuhusu Ethereum.org. Pata nafasi ya kuuliza maswali, kutoa mawazo na kutoa maoni. Hii ni fursa kamili ya kuwa sehemu ya jumuiya inayoshamiri ya Ethereum.

☎️ Ethereum.org Community Call - April 2024

25 Aprili 2024, 16:00

(UTC)

Join Discord(opens in a new tab)Ongeza kwenye kalenda(opens in a new tab)

Mkutano ujao


24 Apr 2024

Mikutano iliyopita


Chunguza ethereum.org