Sarafu-imara
Hela ya kidijitali kwa matumizi ya kila siku
Sarafu-imara ni ishara za Ethereum zilizoundwa kua na thamani ya kudumu, hata pale bei ya ETH inapobadilika.
Kwanini sarafu-imara?
Sarafu-imara ni sarafu-za-kripto zisizo na utete. Zina changia nguvu sawa na ETH lakininthamani yao ni thabiti, iko kama sarafu za jadi. Kwahiyo unapata fedha imara unazoweza kutumia kwenye Ethereum. Jinsi sarafu-imara zinavopata uimara wake
Sarafu-imara ni za ulimwengu, na zinaweza kutumwa kwa mtandao. Ni rahisi kuzipokea au kuzituma pale unapokua na .
Mahitaji ya sarfu-imara ni makubwa, kwahiyo unaweza ukapat faida kwa kukopesha zako. Hakikisha unazitambua hatari kabla ya kukopesha.
Sarafu-imara zinaweza kubadilishwa kwenda kwenye ETH na tokeni zinginezo za Ethereum. nyingi zinategemea sarafu-imara.
Sarfu-imara zinalindwa na. hamna mtu atakaeweza kughushi muamala badala yako.
Pizza isiomaarufu ya Bitcoin
Mwaka 2010, jamaa fulani alinunua pizza 2 kwa bitcoin 10,000. Kwa wakati huo bitcoin ililkua na thamani ya dola ya Marekani ~$41. Kwenye soko la leo hayo ni mamilioni ya dola. Kuna miamala ya kufanana yenye majuto kwenye historia ya Ethereum. Sarafu-imara hutoa suluhisho juu ya tatizo hili, ili uweze kufurahia pizza yako na kuendelea kushikilia ETH yako.
Tafuta sarafu-imara
Kuna mamia ya sarafu-imara zinazopatikana. pata msaada hapa ili uweze kuanza. Kama wewe ni mpya kwenye Ethereum, tunashauri ufanye uchuguzi kiasi kwanza.
Chaguzi za Mhariri
Mifano ya sarafu-imara zinazojulikana zaidi hivi sasa na sarafu tulizoona zinamanufaa wakati wa kutumia dapps.
Dai
Kunauwezekano kua Dai ndio sarafu-imara maarufu iliyogatuliwa. Thamani yake ni takribani dola 1 ya kimarekani na inakubalika kwa upana kati ya dapps.
USDC
Kuna uwezekano kua USDc ndio sarafu maarufu kati ya sarafu-imara zinazobebwa na fedha ya fiat. Thamani yake kwa kukadiria ni kama dola moja hivi na inabebwa na Circle na Coinbase.
Sarafu-imara za juu katika mtaji wa soko
Mtaji wa soko ni idadi ya jumla ya ishara zilizopo mara thamani kwa ishara. Orodha hii inabadilika badilika na miradi iliyoorodheshwa hapa sio lazima ziwe zimepitishwa na timu ya ethereum.org.
Sarafu | Mtaji wa soko | Aina ya dhamana | ↗ |
---|---|---|---|
Tether | $138,253,710,469 | Fiat | Nenda kwa Tether |
USDC | $41,113,264,903 | Fiat | Nenda kwa USDC |
Dai | $3,491,975,555 | Kripto | Nenda kwa Dai |
Jinsi ya kupata sarafu-imara
Weka akiba na sarafu-imara
Sarafu-imara huwa na hutoa riba ya juu ya wastani kwasababu kuna mahitaji makubwa ya kuzikopesha. Kuna dapps zitakazokuruhusu kupewa riba kwenye sarafu-imara ulizonazo kwa wakati halisi unapoziweka kwenye bwawa la kukopesha wengine. Kama ulimwengu wa kubenki, unasambaza ishara kwa wakopeshaji lakini unaweza kutoa ishara zako na riba iliyoongezeka mda wowote.
Dapps zinazopata riba
Fanya matumizi sahihi ya sarfu-imara ulizonazo na pata pesa zaidi. Kama kila kitu kwenye kripto, Mazao ya Asilimia ya Mwaka yaliotabiriwa (APY) yanaweza yakabadilisha kutegemea ugavi/usambazaji wa kila siku.
0.05%
Kiwango cha wastani kinacholipwa na benki kwenye akaunti za akiba za msingi, zilizo na bima ya serikali, Marekani. Chanzo(opens in a new tab)Jinsi zinavyofanya kazi: Aina ya sarafu-imara
Mara zote fanya utafiti wako mwenyewe
Sarafu imara za algorithmic ni teknolojia ambayo ipo kwenye majaribio. Unatakiwa kujua hatari kabla ya kuzitumia.Inategemezwa na fedha za fiat
Faida
- Salama dhidi ya utete wa kripto.
- Mabadiliko ya bei ni ya kima cha chini.
Hasara
- Ya kati -- mtu lazima atoe ishara hizo.
- Inahiataji ukaguzi kuhakikisha kampuni ina akiba ya kutosha.
Mifano ya kazi
Inategemea Kripto
Vyuma vya thamani
Maelekezo
Jifunze zaidi juu ya sarafu-imara
Dashibodi & Elimu
- Nendato Stablecoins.wtf website(opens in a new tab)Stablecoins.wtfStablecoins.wtf hutoa ukurasa wenye historia iliojaa taarifa za masoko, takwimu, na maudhui ya elimu kwa sarafu-imara maarufu zaidi.