What are NFTs?
NFT ni tokeni zilizo na ubinafsi wa kipekee. Kila NTF ina sifa tofauti (haziwezi kuigwa) na ni chache. Hii ni tofauti na tokeni kama ERC-20 ambapo kila tokeni kwenye kikundi hufanana na huwa na sifa sawa ('inaweza kuigwa'). Hujali bili ya dola mahususi uliyo nayo kwenye pochi yako kwa sababu zote zinafanana na thamani zao ni sawa. Hata hivyo, unajali tokeni ya kidijitali unayomiliki, kwa sababu zote huwa na sifa zao za binafsi na unaweza kuzitofautisha kutoka kwen ye nyingine ('haziwezi kuigwa').
Upekee wa kila tokeni za kidijitali zisizoweza kuigwa ni kuwezesha ishara ya vitu kama sanaa, vitu vinavyokusanywa ama mali isiyohamishika, ambapo kila tokeni maalum ya kidijitali isiyoweza kuigwa huwakilisha ulimwengu halisi ama bidhaa ya kidijitali. Umiliki wa mali unalindwa na mnyororo wa bloku wa Ethereum – hakuna anayeweza kubadili nyaraka za umiliki ama kutoa/kubandika nakala mpya za NFT.
Mtandao wa mali
Tokeni zisizoweza kuigwa na Ethereum husuluhisha shida zinazokuwepo kwenye intaneti leo. Kwa kuwa kila kitu kinakuwa cha kidijitali, kuna haja ya kuiga sifa za vitu halisi kama uhaba, upekee na ushahidi wa umiliki. kwa njia isiyoweza kudhibitiwa na mashirika yasiyogatuliwa. Kwa mfano, ukiwa na tokeni za kidijitali zisizoigwa, unaweza kumiliki muziki wa sampuli ya MP3 ambao hauko kwenye programu ya muziki maalum au unaweza kumiliki tovuti ya mtandao wa kijamii ambao unaweza kuuza ama kubadilishana lakini hauwezi kuchukuliwa kihohela kutoka kwako na mtoaji jukwaa.
Hivi ndivyo mtandao wa NFT unafanya kazi ukilinganisha na intaneti ambao wengi wengi tunatumia leo...
Ulinganisho
Intaneti/Mtandao wa NFT | Intaneti ya leo |
---|---|
Unamiliki mali yako! Ni wewe tu unayeweza kuziuza ama kuzibadilisha mwenyewe. | Unaweza kukodisha mali kutoka kwenye mashirika mengine. |
NFT zina sifa za kipekee za kidijitlai, hakuna NFT mbili zitakazofanana. | Mara nyingi nakala ya chombo haiwezi kutofautishwa na ya asili. |
Umiliki wa tokeni zisizoweza kuigwa unawekwa kwenye mnyororo wa bloku ili kila mtu aweze kuthibitisha. | Rekodi za umiliki wa vitu vya kidijitali zinahifadhiwa kwenye seva zinazodhibitiwa na taasisi – lazima uziamini. |
Tokeni zisizoigwa ni mikataba erevu kwenye Ethereum. Hii inamaana kuwa zinaweza kutumika kwenye mikataba erevu mingine na programu kwenye Ethereum! | Kampuni zenye bidhaa za kidigitali huhitaji kuwa na "hifadhi yenye ukingo". |
Waunda maudhui wanaweza kuuza kazi zao sehemu yoyote na kufikia soko la ulimwengu mzima. | Waundaji wanategemea miundombinu na usambazaji wa majukwaa wanayotumia. Mara nyingi hili hufuata sheria na masharit na vizuizi vya kijiografia. |
Watengenezaji wa tokeni zisizoigwa wanaweza kuhifadhi haki za kazi na mirabaha ya programu zao moja kwa moja kwenye mkataba wa tokeni zisizoigwa. | Majukwaa kama ya huduma za kutiririsha muziki, yanapata faida nyingi kutoka kwenye mauzo. |
NFT zinafanyaje kazi?
Kama aina yeyote ya tokeni inayotolewa kwenye Ethereum, tokeni zisizoigwa zinatolewa na mkataba erevu. Mkataba erevu hutimiza moja viwango kadhaa vya tokeni zisizoigwa (haswa ERC-721 au ERC-1155) ambavyo hufafanua kazi ya mkataba huo. Mkataba huu unaweza kuunda ('kuzalisha') tokeni zisizoigwa na kuzipa kwa mmiliki maalum. Umiliki unafafanuliwa kwenye mkataba kwa kuweka tokeni zisizoigwa kwenye anwani maalum. Tokeni isiyoigwa ina kitambulisho na kwa kawaida ina maelezo ya data ambayo hufanya tokeni hii mahususi kuwa ya kipekee.
Mtu anapotengeneza ama kuzalisha tokeni zisizoigwa, anatekeleza kazi ndani ya mkataba erevu ambao huteua tokeni isiyoigwa kwenye anwani yake. Habari hii huhifadhiwa hifadhi ya mkataba wake ambayo ni sehemu ya mnyororo wa bloku. Mtengenezaji wa mkataba anaweza kuandika mantiki zaidi kwenye mkataba, kwa mfano, kuweka kiwango cha usambazaji ama kufafanua mrabaha utakaolipwa kwa mtengenezaji kila mara tokeni zinapohamishwa.
NFT zinatumika kufanya nini?
Tokeni zisizoigwa hutumika kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na:
- kuthibitisha kwamba ulihudhuria tukio
- kuthibitisha kwamba ulimaliza kozi
- umiliki wa vitu vya michezo
- sanaa ya kidijitali
- kugeuza mali za kidunia kuwa tokeni
- kuthibitisha utambulisho wako kwenye mtandao
- kuzuia ufikiaji wa maudhui
- ukataji tiketi
- majina ya kikoa kwenye intaneti iliyogatuliwa
- dhamana kwenye mambo ya fedha yaliyogatuliwa
Labda wewe ni msanii amabaye angependa kushiriki kazi yake kupitia tokeni zisizoigwa, bila wewe kupoteza udhibiti ama kuwapa waamuzi faida zako. Wewe unaweza kutengeneza mkataba mpya na kuweka bayana hesabu ya tokeni zisizoigizwa, vipengele vyao na kiungo chao kwa kazi mahususi ya sanaa. Kama msanii, unaweza kuprogramu ndani ya mkataba-erevu mrabaha unaofaa kulipwa (kwa mfano hamisha 5% ya bei ya mauzo kwa mwenye mkataba kila wakati tokeni isiyoigwa) inapohamishwa. Vile vile unaweza kuthibitisha kwamba wewe ndiwe umetengeneza tokeni isiyoigwa kwa sababu wewe ndiwe mmiliki wa pochi iliyotuma mkataba huo. Wanunuzi wako wanaweza kuthibitisha kuthibitisha kwa urahisi kwamba wao ndio wamiliki wa tokeni isiyoigwa halisi kutoka kwenye mkusanyiko wako kwa sababu anwani ya pochi zao inashirikishwa na tokeni kutoka kwenye mkataba wako. Wanaweza kuitumia katika mfumo wa ikologia ya Ethereum, inayoaminika kwa uhalisi wake.
Ama zingatia tiketi ya mechi ijayo. Kama mratibu wa matukio anavyoweza kuamua idadi ya tiketi za kuchapisha, muundaji wa NFT anaweza kuamua idadi ya kuwepo kwa nakala za kazi yake. Wakati mwingine huwa na nakala za ziada, kama vile Tiketi 5000 za Kiingilio cha Jumla. Wakati mwingine nyingine zinachapishwa zinazofanana, ila kila moja ina tofauti ndogo na yenzake, kama vile tiketi yeneye nambari ya kiti. Hizi zinaweza kununuliwa na kuuzwa kutoka kwa mshirika mmoja mpaka kwa mwingine kusipokuwepo na ulipaji wa washikaji tiketi na wanunuzi watakuwa na uhakika wa tiketi halisi kwa kuangalia anwani ya mkataba huo.
Kwenye ethereum.org, tokeni zisizoigwa zinatumika kuonyesha kwamba watu wamechangia kwenye hazina ya GitHub ama kushiriki kwa wito uliotolewa, vile vile tuna jina la kikoa cheti cha tokeni isiyoigwa. Ukichangia kwenye ethereum.org, unaweza kudai NFT ya POAP. Mikutano mingine ya sarafu za kidijitali imetumia POAPs kama tiketi. Zaidi juu ya uchangiaji.
Tovuti hii pia inatumia jina mbadala la kikoa linaloendeshwa na NFT, ethereum.eth. Anwani yetu ya .org
inasimamiwa na mfumo wa majina wa kati/jadi(DNS), wakati ethereum.eth
imesajiliwa kwenye huduma za majina ya Ethereum (ENS). Na hii linamilikiwa na kuendeshwa na sisi. Angalia rekodi zetu za ENS(opens in a new tab)
Zaidi juu ya ENS(opens in a new tab)
Usalama wa NFT
Usalama wa Ethereum unakuja kutokana na ushahidi wa hisa. Mfumo huu umebuniwa ili uweze kuondoa vitendo ya kihasidi kiuchumi na basi kuifanya Ethereum sugu kwa uharibifu. Hii ndiyo inayofanya tokeni zisizoigwa kuwezekana. Mara tu bloku yenye muamala wako wa NFT inapokamilika, inaweza kugharimu mshambulizi mamilioni ya ETH kuibadilisha. Mtu yeyote anayetumia programu ya Ethereum anaweza kujua haraka mambo yasiyofaa ya kuhitilafiana na NFT, na mtu huyu mbaya atatozwa malipo na kuondolewa.
Maswala ya usalama yanayohusiana na NFT sana sana yanahusiana na utapeli wa kutumia barua pepe, hatari za mkataba-erevu au makosa ya mtumiaji (kama vile kuweka wazi funguo za siri) na hivyo kufanya usalam bora wa pochi uwe muhimu sana kwa wamiliki NFT.
Maelezo zaidi kuhusu usalamaSoma zaidi
- Mwongozo wa wa mwanafunzi wa NFT(opens in a new tab) – Linda Xie, Januari 2020
- Mfuatliliaji EtherscanNFT(opens in a new tab)
- Kiwango cha tokeni cha ERC-721
- Kiwango cha tokeni cha ERC-1155