Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Change page

Kiwango cha Tokeni Isiyo Mbadala cha ERC-721

Utangulizi

Tokeni Isiyo Mbadala ni nini?

Tokeni Isiyo Mbadala (NFT) hutumika kutambua kitu au mtu kwa njia ya kipekee. Aina hii ya Tokeni ni kamilifu kutumika kwenye majukwaa yanayotoa vikusanywa, funguo za ufikiaji, tiketi za bahati nasibu, viti vilivyo na nambari kwa ajili ya matamasha na mechi za michezo, n.k. Aina hii maalum ya Tokeni ina uwezekano wa kushangaza kwa hivyo inastahili Kiwango kinachofaa, ERC-721 ilikuja kutatua hilo!

ERC-721 ni nini?

ERC-721 inaleta kiwango cha NFT, kwa maneno mengine, aina hii ya Tokeni ni ya kipekee na inaweza kuwa na thamani tofauti na Tokeni nyingine kutoka kwenye Mkataba Mahiri ule ule, labda kutokana na umri wake, uhaba au hata kitu kingine kama mwonekano wake. Subiri, mwonekano?

Ndiyo! NFTs zote zina kigezo cha uint256 kinachoitwa tokenId, kwa hivyo kwa Mkataba wowote wa ERC-721, jozi ya contract address, uint256 tokenId lazima iwe ya kipekee ulimwenguni. Kwa kusema hivyo, programu tumizi iliyogatuliwa (dapp) inaweza kuwa na "kigeuzi" kinachotumia tokenId kama ingizo na kutoa picha ya kitu kizuri, kama vile mazombi, silaha, ujuzi au paka wa kushangaza!

Mahitaji ya awali

Mwili

ERC-721 (Ethereum Request for Comments 721), iliyopendekezwa na William Entriken, Dieter Shirley, Jacob Evans, Nastassia Sachs mnamo Januari 2018, ni Kiwango cha Tokeni Isiyo Mbadala kinachotekeleza API kwa ajili ya tokeni ndani ya Mikataba Mahiri.

Inatoa utendaji kama vile kuhamisha tokeni kutoka akaunti moja hadi nyingine, kupata salio la sasa la tokeni la akaunti, kupata mmiliki wa tokeni mahususi na pia jumla ya usambazaji wa tokeni inayopatikana kwenye mtandao. Kando na haya pia ina utendaji mwingine kama vile kuidhinisha kwamba kiasi cha tokeni kutoka kwenye akaunti kinaweza kuhamishwa na akaunti ya mtu mwingine.

Ikiwa Mkataba Mahiri utatekeleza mbinu na matukio yafuatayo unaweza kuitwa Mkataba wa Tokeni Isiyo Mbadala wa ERC-721 na, ukishasambazwa, utawajibika kufuatilia tokeni zilizoundwa kwenye Ethereum.

Kutoka EIP-721 (opens in a new tab):

Mbinu

Matukio

    event Transfer(address indexed _from, address indexed _to, uint256 indexed _tokenId);
    event Approval(address indexed _owner, address indexed _approved, uint256 indexed _tokenId);
    event ApprovalForAll(address indexed _owner, address indexed _operator, bool _approved);

Mifano

Hebu tuone jinsi Kiwango kilivyo muhimu sana kurahisisha mambo kwetu kukagua Mkataba wowote wa Tokeni wa ERC-721 kwenye Ethereum. Tunahitaji tu Kiolesura cha Uwili cha Programu Tumizi ya Mkataba (ABI) ili kuunda kiolesura cha Tokeni yoyote ya ERC-721. Kama unavyoona hapa chini tutatumia ABI iliyorahisishwa, ili kuifanya iwe mfano usio na msuguano mkubwa.

Mfano wa Web3.py

Kwanza, hakikisha umesakinisha maktaba ya Python ya Web3.py (opens in a new tab):

pip install web3

Mkataba wa CryptoKitties una Matukio ya kuvutia zaidi ya yale ya Kiwango.

Hebu tuangalie mawili kati yao, Pregnant na Birth.

Usomaji zaidi

Mafunzo: Jenga kwa kutumia tokeni zisizo mbadala (ERC-721) kwenye Ethereum