Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Change page

Ethereum kwa wasanidi wa JavaScript

JavaScript ni miongoni mwa lugha maarufu zaidi katika mfumo wa ikolojia wa Ethereum. Kwa kweli, kuna timu (opens in a new tab) iliyojitolea kuleta kiasi kikubwa cha Ethereum kwenye JavaScript iwezekanavyo.

Kuna fursa za kuandika JavaScript (au kitu kinachokaribiana nayo) katika viwango vyote vya steki.

Kuingiliana na Ethereum

Maktaba za API za JavaScript

Ikiwa ungependa kuandika JavaScript ili kuuliza mnyororo wa vitalu, kutuma miamala na zaidi, njia rahisi zaidi ya kufanya hivi ni kutumia maktaba ya API ya JavaScript. API hizi huruhusu wasanidi kuingiliana kwa urahisi na nodi katika mtandao wa Ethereum.

Unaweza kutumia maktaba hizi kuingiliana na mikataba mahiri kwenye Ethereum kwa hivyo inawezekana kuunda programu tumizi iliyogatuliwa (dapp) ambapo unatumia tu JavaScript kuingiliana na mikataba iliyopo tayari.

Angalia

Mikataba mahiri

Ikiwa wewe ni msanidi wa JavaScript na unataka kuandika mkataba mahiri wako mwenyewe, unaweza kutaka kufahamiana na Solidity (opens in a new tab). Hii ndiyo lugha maarufu zaidi ya mkataba mahiri na inafanana kimuundo na JavaScript, jambo ambalo linaweza kuifanya iwe rahisi kujifunza.

Zaidi kuhusu mikataba mahiri.

Kuelewa itifaki

Mashine pepe ya Ethereum

Kuna utekelezaji wa JavaScript wa mashine pepe ya Ethereum. Inasaidia sheria za hivi punde za mchepuo. Sheria za mchepuo hurejelea mabadiliko yaliyofanywa kwenye EVM kutokana na masasisho yaliyopangwa.

Imegawanywa katika vifurushi mbalimbali vya JavaScript ambavyo unaweza kuviangalia ili kuelewa vyema:

  • Akaunti
  • Vitalu
  • Mnyororo wa vitalu wenyewe
  • Miamala
  • Na zaidi...

Hii itakusaidia kuelewa mambo kama "muundo wa data wa akaunti ni upi?".

Ikiwa unapendelea kusoma msimbo, JavaScript hii inaweza kuwa mbadala mzuri wa kusoma kupitia hati zetu.

Angalia EVM
@ethereumjs/evm (opens in a new tab)

Nodi na wateja

Mteja wa EthereumJS yuko katika usanidi unaoendelea ambao unakuruhusu kuchunguza jinsi wateja wa Ethereum wanavyofanya kazi katika lugha unayoielewa; JavaScript!

Angalia mteja
@ethereumjs/client (opens in a new tab)

Miradi mingine

Pia kuna mambo mengine mengi yanayoendelea katika ulimwengu wa JavaScript ya Ethereum, ikiwa ni pamoja na:

  • maktaba za huduma za mkoba.
  • zana za kuzalisha, kuingiza, na kuhamisha funguo za Ethereum.
  • utekelezaji wa merkle-patricia-tree – muundo wa data ulioainishwa katika waraka wa manjano wa Ethereum.

Chunguza chochote kinachokuvutia zaidi kwenye hifadhi ya EthereumJS (opens in a new tab)

Kusoma zaidi

Unajua rasilimali ya jamii iliyokusaidia? Hariri ukurasa huu na uiongeze!