Ruka hadi maudhui makuu
Change page

Mifumo ya Uundaji wa Dapp

Utangulizi wa mifumo

Kujenga programu tumizi iliyogatuliwa (dapp) kamili kunahitaji vipande tofauti vya teknolojia. Mifumo ya programu inajumuisha vipengele vingi vinavyohitajika au hutoa mifumo rahisi ya programu-jalizi ili kuchagua zana unazotaka.

Mifumo inakuja na utendaji mwingi wa moja kwa moja, kama vile:

  • Vipengele vya kuanzisha mfano wa mnyororo wa vitalu wa ndani.
  • Huduma za kukusanya na kujaribu mikataba mahiri yako.
  • Viongezi vya uundaji wa mteja ili kujenga programu yako inayoangalia mtumiaji ndani ya mradi/hifadhi sawa.
  • Usanidi wa kuunganisha kwenye mitandao ya Ethereum na kusambaza mikataba, iwe kwa mfano unaoendeshwa ndani, au mojawapo ya mitandao ya umma ya Ethereum.
  • Usambazaji wa programu iliyogatuliwa - miunganisho na chaguzi za uhifadhi kama IPFS.

Mahitaji ya awali

Kabla ya kuzama kwenye mifumo, tunapendekeza usome kwanza utangulizi wetu wa dapps na mrundikano wa Ethereum.

Mifumo inayopatikana

Foundry - Foundry ni zana yenye kasi sana, inayobebeka na ya msimu kwa ajili ya uundaji wa programu tumizi za Ethereum

Hardhat - Mazingira ya uundaji wa Ethereum kwa wataalamu.

Ape - Zana ya uundaji wa mkataba mahiri kwa Wataalamu wa Python, Wanasayansi wa Data, na Wataalamu wa Usalama.

Web3j - Jukwaa la kuunda programu tumizi za mnyororo wa vitalu kwenye JVM.

ethers-kt - Maktaba ya Async, yenye utendaji wa juu ya Kotlin/Java/Android kwa minyororo ya vitalu inayotegemea Mashine Pepe ya Ethereum (EVM).

Create Eth App - Unda programu zinazoendeshwa na Ethereum kwa amri moja. Inakuja na ofa pana ya mifumo ya UI na violezo vya fedha zilizogatuliwa (DeFi) vya kuchagua.

Scaffold-ETH 2 - Next.js, Wagmi, Viem na RainbowKit na chaguo lako la Hardhat au Foundry: hot reload ya mkataba, ndoano maalum za React, mkoba wa muda na bomba la ndani, na moduli za ugani kwa uundaji wa programu tumizi iliyogatuliwa (dapp) wa full-stack.

Tenderly - Jukwaa la uundaji la Web3 linalowezesha waundaji wa mnyororo wa vitalu kujenga, kujaribu, kutatua, kufuatilia, na kuendesha mikataba mahiri na kuboresha UX ya dapp.

The Graph - The Graph kwa kudodosa data ya mnyororo wa vitalu kwa ufanisi.

Alchemy - Jukwaa la Uundaji la Ethereum.

NodeReal - Jukwaa la Uundaji la Ethereum.

thirdweb SDK - Jenga programu tumizi za Web3 zinazoweza kuingiliana na mikataba mahiri yako kwa kutumia SDK na CLI zetu zenye nguvu.

Chainstack - Jukwaa la Uundaji la Web3 (Ethereum na mengineyo).

Crossmint - Jukwaa la uundaji la Web3 la kiwango cha biashara, linalokuruhusu kujenga programu tumizi za tokani isiyobadilishika (NFT) kwenye minyororo yote mikuu Minyororo ya EVM (na mingineyo).

Brownie - Mazingira ya uundaji na mfumo wa majaribio unaotegemea Python.

OpenZeppelin SDK - Zana Bora Kabisa za Mkataba Mahiri: Kundi la zana za kukusaidia kuunda, kukusanya, kuboresha, kusambaza na kuingiliana na mikataba mahiri.

Catapulta - Zana ya usambazaji wa mikataba mahiri ya minyororo mingi, otomatisha uthibitishaji katika vigunduzi vya kitalu, fuatilia mikataba mahiri iliyosambazwa na ushiriki ripoti za usambazaji, plug-n-play kwa miradi ya Foundry na Hardhat.

GoldRush (inayoendeshwa na Covalent) - GoldRush inatoa kundi la Kiolesura cha Kupanga Programu Tumizi (API) la data ya mnyororo wa vitalu la kina zaidi kwa waundaji, wachambuzi, na biashara. Iwe unajenga dashibodi ya DeFi, mkoba, boti ya biashara, ajenti wa akili bandia au jukwaa la kufuata sheria, API za data hutoa ufikiaji wa haraka, sahihi, na rafiki kwa waundaji kwa data muhimu ya mnyororoni unayohitaji

Wake - Mfumo wa Python wa yote kwa moja kwa majaribio ya mikataba, fuzzing, usambazaji, uchunguzi wa udhaifu na urambazaji wa msimbo.

Veramo - Mfumo wa chanzo wazi, wa msimu na usiofungamana unaorahisisha kwa waundaji wa programu tumizi zilizogatuliwa kujenga vitambulisho vilivyogatuliwa na stakabadhi zinazoweza kuthibitishwa katika programu tumizi zao.

Moccasin - Mfumo wa haraka, wa Pythonic wa uundaji na majaribio ya mkataba mahiri kwa Vyper, uliojengwa kwenye Titanoboa.

Usomaji zaidi

Unajua rasilimali ya jamii iliyokusaidia? Hariri ukurasa huu na uiongeze!

Mafunzo: Mifumo ya uundaji kwenye Ethereum