Kutumia Ethereum kunahitaji kurahisishwa; kuanzia kudhibiti na hadi kuanzisha miamala. Ili kuwezesha matumizi makubwa, Ethereum lazima iongeze kwa kiasi kikubwa urahisi wa matumizi, ikiruhusu watumiaji kupata ufikiaji bila ruhusa na unaostahimili udhibiti kwenye Ethereum kwa uzoefu usio na msuguano wa kutumia programu za .
Zaidi ya vifungu vya maneno vya mbegu
Akaunti za Ethereum zinalindwa na jozi ya vifunguo vinavyotumika kutambua akaunti (ufunguo wa umma) na kutia saini jumbe (ufunguo wa siri). Ufunguo wa siri ni kama nenosiri kuu; unaruhusu ufikiaji kamili wa akaunti ya Ethereum. Hii ni njia tofauti ya kufanya kazi kwa watu waliozoea zaidi benki na programu za Web2 ambazo husimamia akaunti kwa niaba ya mtumiaji. Ili Ethereum ifikie matumizi makubwa bila kutegemea wahusika wengine waliowekwa kati, lazima kuwe na njia ya moja kwa moja, isiyo na msuguano kwa mtumiaji kuchukua ulinzi wa rasilimali zao na kudhibiti data zao bila kulazimika kuelewa kriptografia ya ufunguo wa umma na siri na usimamizi wa ufunguo.
Suluhisho la hili ni kutumia pochi za kuingiliana na Ethereum. Pochi za mkataba mahiri huunda njia za kulinda akaunti ikiwa vifunguo vitapotea au kuibiwa, fursa za utambuzi bora wa udanganyifu na ulinzi, na kuruhusu pochi kupata utendaji mpya. Ingawa pochi za mkataba mahiri zipo leo, ni ngumu kuziunda kwa sababu itifaki ya Ethereum inahitaji kuzisaidia vizuri zaidi. Usaidizi huu wa ziada unajulikana kama udhanifu wa akaunti.
Zaidi kuhusu udhanifu wa akauntiNodi kwa kila mtu
Watumiaji wanaoendesha hawapaswi kuamini wahusika wengine kuwapa data, na wanaweza kuingiliana haraka, kwa faragha, na bila ruhusa na wa Ethereum. Hata hivyo, kuendesha nodi sasa hivi kunahitaji ujuzi wa kiufundi na nafasi kubwa ya diski, ikimaanisha watu wengi lazima waamini waamuzi badala yake.
Kuna maboresho kadhaa ambayo yatafanya kuendesha nodi kuwa rahisi zaidi na kutumia rasilimali chache zaidi. Njia ambayo data inahifadhiwa itabadilishwa ili kutumia muundo unaotumia nafasi vizuri zaidi unaojulikana kama Mti wa Verkle. Pia, kwa ubilahali au kuisha muda wa data, nodi za Ethereum hazitahitaji kuhifadhi nakala ya data nzima ya hali ya Ethereum, na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa mahitaji ya nafasi ya diski kuu. Nodi nyepesi zitatoa faida nyingi za kuendesha nodi kamili lakini zinaweza kuendeshwa kwa urahisi kwenye simu za mkononi au ndani ya programu rahisi za kivinjari.
Soma kuhusu Miti ya VerkleKwa maboresho haya, vizuizi vya kuendesha nodi vinapunguzwa hadi kufikia sifuri. Watumiaji watafaidika na ufikiaji salama, bila ruhusa kwenye Ethereum bila kulazimika kutoa nafasi kubwa ya diski au CPU kwenye kompyuta au simu zao za mkononi, na hawatalazimika kutegemea wahusika wengine kwa data au ufikiaji wa mtandao wanapotumia programu.
Maendeleo ya sasa
Pochi za mkataba mahiri tayari zinapatikana, lakini maboresho zaidi yanahitajika ili kuzifanya ziwe zilizogatuliwa na bila ruhusa iwezekanavyo. EIP-4337 ni pendekezo lililokomaa ambalo halihitaji mabadiliko yoyote kwenye itifaki ya Ethereum. Mkataba mahiri mkuu unaohitajika kwa EIP-4337 ulisambazwa mnamo Machi 2023.
Ubilahali kamili bado uko katika awamu ya utafiti na huenda ikachukua miaka kadhaa kabla ya kutekelezwa. Kuna hatua kadhaa muhimu kwenye njia ya kuelekea ubilahali kamili, ikiwa ni pamoja na kuisha muda wa data, ambazo zinaweza kutekelezwa mapema zaidi. Vipengee vingine vya ramani ya njia, kama vile Miti ya Verkle na utengano wa mpendekezaji na mjengaji (PBS) vinahitaji kukamilishwa kwanza.
Mitandao ya majaribio ya Miti ya Verkle tayari inafanya kazi, na awamu inayofuata ni kuendesha wateja waliowezeshwa na Miti ya Verkle kwenye mitandao ya majaribio ya kibinafsi, kisha ya umma. Unaweza kusaidia kuharakisha maendeleo kwa kusambaza mikataba kwenye mitandao ya majaribio au kuendesha wateja wa mtandao wa majaribio.
