Mlolongo wa matukio ya hatua kuu zote, michepuo, na masasisho kwenye mnyororo wa vitalu wa Ethereum.
Michepuo ni wakati ambapo masasisho makuu ya kiufundi au mabadiliko yanahitaji kufanywa kwenye mtandao – kwa kawaida yanatokana na Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs) na kubadilisha "sheria" za itifaki.
Wakati masasisho yanapohitajika katika programu za kitamaduni zinazodhibitiwa na kituo kimoja, kampuni itachapisha tu toleo jipya kwa mtumiaji wa mwisho. Minyororo ya vitalu hufanya kazi tofauti kwa sababu hakuna umiliki wa kati. Wateja wa Ethereum lazima wasasishe programu zao ili kutekeleza sheria mpya za mchepuo. Pia waundaji wa vitalu (wachimbaji katika ulimwengu wa Uthibitisho wa Kazi (PoW), wathibitishaji katika ulimwengu wa Uthibitisho wa Dau (PoS)) na nodi lazima waunde vitalu na kuthibitisha dhidi ya sheria mpya. Zaidi kuhusu taratibu za makubaliano
Mabadiliko haya ya sheria yanaweza kuunda mgawanyiko wa muda katika mtandao. Vitalu vipya vinaweza kuzalishwa kulingana na sheria mpya au zile za zamani. Michepuo kwa kawaida hukubaliwa mapema ili wateja wakubali mabadiliko kwa pamoja na mchepuo wenye masasisho unakuwa mnyororo mkuu. Hata hivyo, katika matukio nadra, kutokubaliana juu ya michepuo kunaweza kusababisha mtandao kugawanyika kabisa – hasa uundaji wa Ethereum Asilia kupitia mchepuo wa DAO.
Programu inayoendesha Ethereum inaundwa na nusu mbili, zinazojulikana kama na .
Upeaji majina wa masasisho ya utekelezaji
Tangu 2021, masasisho kwenye tabaka la utekelezaji yanapewa majina kulingana na majina ya miji ya maeneo ya awali ya Devcon na Devconnect (inafunguka katika kichupo kipya) kwa mpangilio wa matukio:
| Jina la Sasisho | Mwaka wa Devcon(nect) | Nambari ya Devcon | Tarehe ya Sasisho |
|---|---|---|---|
| Berlin | 2014 | 0 | 15 Apr 2021 |
| London | 2015 | I | 5 Ago 2021 |
| Shanghai | 2016 | II | 12 Apr 2023 |
| Cancun | 2017 | III | 13 Mac 2024 |
| Prague | 2018 | IV | 7 Mei 2025 |
| Osaka | 2019 | V | 3 Des 2025 |
| Amsterdam | 2022 | Devconnect | Bado - Inayofuata |
| Bogotá | 2022 | VI | Bado |
| Istanbul | 2023 | Devconnect | Bado |
| Bangkok | 2024 | VII | Bado |
| Buenos Aires | 2025 | Devconnect | Bado |
| Mumbai | 2026 | VIII | Bado |
Upeaji majina wa masasisho ya mwafaka
Tangu kuzinduliwa kwa , masasisho kwenye tabaka la mwafaka yanapewa majina ya nyota za angani kuanzia na herufi zinazofuatana kwa mpangilio wa alfabeti:
| Jina la Sasisho | Tarehe ya Sasisho |
|---|---|
| Mwanzo wa Mnyororo wa Beacon | 1 Des 2020 |
| Altair (inafunguka katika kichupo kipya) | 27 Okt 2021 |
| Bellatrix (inafunguka katika kichupo kipya) | 6 Sep 2022 |
| Capella (inafunguka katika kichupo kipya) | 12 Apr 2023 |
| Deneb (inafunguka katika kichupo kipya) | 13 Mac 2024 |
| Electra (inafunguka katika kichupo kipya) | 7 Mei 2025 |
| Fulu (inafunguka katika kichupo kipya) | 3 Des 2025 |
| Gloas (inafunguka katika kichupo kipya) | Bado - Inayofuata |
| Heze (inafunguka katika kichupo kipya) | Bado |
Upeaji majina uliounganishwa
Masasisho ya utekelezaji na mwafaka awali yalizinduliwa kwa nyakati tofauti, lakini baada ya Unganisho mnamo 2022 haya yamekuwa yakitekelezwa kwa wakati mmoja. Kwa hivyo, maneno ya kawaida yameibuka ili kurahisisha marejeleo ya masasisho haya kwa kutumia neno moja lililounganishwa. Hili lilianza na sasisho la Shanghai-Capella, ambalo kwa kawaida hujulikana kama "Shapella", na linaendelezwa na masasisho yanayofuata.
| Sasisho la Utekelezaji | Sasisho la Mwafaka | Jina Fupi |
|---|---|---|
| Shanghai | Capella | "Shapella" |
| Cancun | Deneb | "Dencun" |
| Prague | Electra | "Pectra" |
| Osaka | Fulu | "Fusaka" |
| Amsterdam | Gloas | "Glamsterdam" |
| Bogotá | Heze | "Hegotá" |
Ruka moja kwa moja hadi kwenye taarifa kuhusu baadhi ya masasisho muhimu sana ya zamani: Mnyororo wa Beacon; Unganisho; na EIP-1559
Unatafuta masasisho ya itifaki ya baadaye? Jifunze kuhusu masasisho yajayo kwenye ramani ya njia ya Ethereum.
2025
Fulu-Osaka ("Fusaka")
3 Des 2025, 21:49:11 UTC
7 Mei 2025, 10:05:11 UTC
Sasisho la Prague-Electra ("Pectra") lilijumuisha maboresho kadhaa kwenye itifaki ya Ethereum yaliyolenga kuboresha uzoefu kwa watumiaji wote, mitandao ya tabaka la 2 (l2), waweka dhamana na waendeshaji wa nodi.
Uwekaji dhamana ulipata sasisho kwa akaunti za mthibitishaji zinazojilimbikiza, na udhibiti ulioboreshwa wa fedha zilizowekwa dhamana kwa kutumia anwani ya utoaji ya utekelezaji. EIP-7251 iliongeza salio tendaji la juu zaidi kwa mthibitishaji mmoja hadi 2048, na kuboresha ufanisi wa mtaji kwa waweka dhamana. EIP-7002 iliwezesha akaunti ya utekelezaji kuanzisha kwa usalama vitendo vya mthibitishaji, ikiwa ni pamoja na kujitoa, au kutoa sehemu ya fedha, kuboresha uzoefu kwa waweka dhamana wa ETH, huku ikisaidia kuimarisha uwajibikaji kwa waendeshaji wa nodi.
Sehemu nyingine za sasisho zililenga kuboresha uzoefu kwa watumiaji wa kawaida. EIP-7702 ilileta uwezo kwa akaunti ya kawaida isiyo ya mkataba mahiri () kutekeleza msimbo sawa na mkataba mahiri. Hili lilifungua utendaji mpya usio na kikomo kwa akaunti za kitamaduni za Ethereum, kama vile ukusanyaji wa mafungu wa muamala, ufadhili wa gesi, uthibitishaji mbadala, udhibiti wa matumizi unaoweza kupangwa, mbinu za kurejesha akaunti na zaidi.
Uzoefu bora wa mtumiaji:
- EIP-7702 - Weka msimbo wa akaunti ya EOA
- EIP-7691 - Ongezeko la uwezo wa upitishaji wa blobu
- EIP-7623 - Ongeza gharama ya data za mwito
- EIP-7840 - Ongeza ratiba ya blobu kwenye faili za usanidi za EL
Uzoefu bora wa uwekaji dhamana:
- EIP-7251 - Ongeza
MAX_EFFECTIVE_BALANCE - EIP-7002 - Kujitoa kunakoanzishwa na tabaka la utekelezaji
- EIP-7685 - Maombi ya tabaka la utekelezaji ya matumizi ya jumla
- EIP-6110 - Toa amana za mthibitishaji mnyororoni
Ufanisi wa itifaki na maboresho ya usalama:
- Jinsi Pectra itakavyoboresha uzoefu wa uwekaji dhamana (inafunguka katika kichupo kipya)
- Soma vipimo vya sasisho la Electra (inafunguka katika kichupo kipya)
- Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Prague-Electra ("Pectra")
2024
Cancun-Deneb ("Dencun")
13 Mac 2024, 13:55:35 UTC
Muhtasari wa Cancun
Sasisho la Cancun lina seti ya maboresho kwenye utekelezaji wa Ethereum yanayolenga kuboresha uwezo wa kuongezeka, sambamba na masasisho ya mwafaka ya Deneb.
Hasa hii inajumuisha EIP-4844, inayojulikana kama Proto-Danksharding, ambayo inapunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya uhifadhi wa data kwa mikusanyiko ya tabaka la 2 (l2). Hili linafikiwa kupitia kuanzishwa kwa "mablobu" ya data ambayo inawezesha mikusanyiko kuchapisha data kwenye Mtandao Mkuu kwa muda mfupi. Hii inasababisha ada za muamala kuwa chini sana kwa watumiaji wa mikusanyiko ya tabaka la 2 (l2).
- EIP-1153 - Misimbo ya operesheni ya uhifadhi wa muda
- EIP-4788 - Shina la kitalu cha kinara katika EVM
- EIP-4844 - Miamala ya blobu ya shadi (Proto-Danksharding)
- EIP-5656 -
MCOPY- Maagizo ya kunakili kumbukumbu - EIP-6780 -
SELFDESTRUCTtu katika muamala huo huo - EIP-7516 - msimbo wa operesheni wa
BLOBBASEFEE
- Mikusanyiko ya tabaka la 2 (l2)
- Proto-Danksharding
- danksharding
- Soma vipimo vya sasisho la Cancun (inafunguka katika kichupo kipya)
Muhtasari wa Deneb
Sasisho la Deneb lina seti ya maboresho kwenye mwafaka wa Ethereum yanayolenga kuboresha uwezo wa kuongezeka. Sasisho hili linakuja sambamba na masasisho ya utekelezaji ya Cancun ili kuwezesha Proto-Danksharding (EIP-4844), pamoja na maboresho mengine kwenye Mnyororo wa Beacon.
"Ujumbe wa kujitoa kwa hiari" uliotiwa saini na kuzalishwa mapema hauishi muda wake tena, hivyo kutoa udhibiti zaidi kwa watumiaji wanaoweka dhamana fedha zao kwa mwendeshaji wa nodi wa tatu. Kwa ujumbe huu wa kujitoa uliotiwa saini, waweka dhamana wanaweza kukaimisha uendeshaji wa nodi huku wakidumisha uwezo wa kujitoa kwa usalama na kutoa fedha zao wakati wowote, bila kuhitaji kuomba ruhusa kutoka kwa mtu yeyote.
EIP-7514 inaleta udhibiti mkali kwenye utoaji wa ETH kwa kuweka kikomo cha kiwango cha "upokezanaji" ambacho wathibitishaji wanaweza kujiunga na mtandao hadi nane (8) kwa kila kipindi. Kwa kuwa utoaji wa ETH unalingana na jumla ya ETH iliyowekwa dhamana, kupunguza idadi ya wathibitishaji wanaojiunga kunaweka kikomo kwenye kiwango cha ukuaji cha ETH mpya inayotolewa, huku pia ikipunguza mahitaji ya maunzi kwa waendeshaji wa nodi, kusaidia ugatuzi.
- Soma vipimo vya sasisho la Deneb (inafunguka katika kichupo kipya)
- Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Cancun-Deneb ("Dencun")
2023
Shanghai-Capella ("Shapella")
12 Apr 2023, 22:27:35 UTC
Muhtasari wa Shanghai
Sasisho la Shanghai lilileta utoaji wa uwekaji dhamana kwenye tabaka la utekelezaji. Sambamba na sasisho la Capella, hii iliwezesha vitalu kukubali operesheni za utoaji, jambo ambalo linaruhusu waweka dhamana kutoa ETH zao kutoka kwenye Mnyororo wa Beacon hadi kwenye tabaka la utekelezaji.
Muhtasari wa Capella
Sasisho la Capella lilikuwa sasisho kuu la tatu kwenye tabaka la mwafaka (Mnyororo wa Beacon) na liliwezesha utoaji wa uwekaji dhamana. Capella ilifanyika kwa wakati mmoja na sasisho la tabaka la utekelezaji, Shanghai, na kuwezesha utendaji wa utoaji wa uwekaji dhamana.
Sasisho hili la tabaka la mwafaka lilileta uwezo kwa waweka dhamana ambao hawakutoa vitambulisho vya uondoaji wakati wa kuweka amana yao ya awali kufanya hivyo, na hivyo kuwezesha utoaji.
Sasisho hili pia lilitoa utendaji wa kufagia akaunti kiotomatiki, ambao huchakata mfululizo akaunti za wathibitishaji kwa malipo yoyote ya tuzo yanayopatikana au utoaji kamili.
- Zaidi kuhusu utoaji wa uwekaji dhamana.
- Soma vipimo vya sasisho la Capella (inafunguka katika kichupo kipya)
2022
Paris (Unganisho)
15 Sep 2022, 6:42:42 UTC
Muhtasari
Sasisho la Paris lilianzishwa na mnyororo wa vitalu wa Uthibitisho wa Kazi kupita wa 58750000000000000000000. Hili lilitokea kwenye kitalu cha 15537393 mnamo tarehe 15 Septemba 2022, na kuanzisha sasisho la Paris kwenye kitalu kilichofuata. Paris ilikuwa mpito wa Unganisho - kipengele chake kikuu kilikuwa kuzima algoriti ya uchimbaji ya Uthibitisho wa Kazi na mantiki ya mwafaka inayohusiana na badala yake kuwasha Uthibitisho wa Dau. Paris yenyewe ilikuwa sasisho kwa wateja wa utekelezaji (sawa na Bellatrix kwenye tabaka la mwafaka) ambalo liliwawezesha kupokea maagizo kutoka kwa wateja wao wa mwafaka waliounganishwa. Hili lilihitaji seti mpya ya mbinu za ndani za API, zinazojulikana kwa pamoja kama API ya Injini (inafunguka katika kichupo kipya), kuwezeshwa. Hili bila shaka lilikuwa sasisho muhimu zaidi katika historia ya Ethereum tangu Homstedi!
Bellatrix
6 Sep 2022, 11:34:47 UTC
Muhtasari
Sasisho la Bellatrix lilikuwa sasisho la pili lililopangwa kwa ajili ya Mnyororo wa Beacon, likiandaa mnyororo kwa ajili ya Unganisho. Linaleta adhabu za mthibitishaji kwa viwango vyake kamili kwa kutofanya kazi na makosa yanayoweza kukatwa. Bellatrix pia inajumuisha sasisho la sheria za uchaguzi wa mchepuo ili kuandaa mnyororo kwa ajili ya Unganisho na mpito kutoka kitalu cha mwisho cha Uthibitisho wa Kazi hadi kitalu cha kwanza cha Uthibitisho wa Dau. Hii inajumuisha kuwafanya wateja wa mwafaka kufahamu wa 58750000000000000000000.
Gray Glacier
30 Jun 2022, 10:54:04 UTC
Muhtasari
Sasisho la mtandao la Gray Glacier lilisogeza mbele kwa miezi mitatu. Hili ndilo badiliko pekee lililoletwa katika sasisho hili, na linafanana kiasili na masasisho ya Arrow Glacier na Muir Glacier. Mabadiliko sawa yamefanywa kwenye masasisho ya mtandao ya Bizantiamu, Konstantinopoli na London.
- EIP-5133 – inachelewesha Bomu la ugumu hadi Septemba 2022
2021
Arrow Glacier
9 Des 2021, 19:55:23 UTC
Muhtasari
Sasisho la mtandao la Arrow Glacier lilisogeza mbele kwa miezi kadhaa. Hili ndilo badiliko pekee lililoletwa katika sasisho hili, na linafanana kiasili na sasisho la Muir Glacier. Mabadiliko kama haya yamefanywa kwenye masasisho ya mtandao ya Bizantiamu, Konstantinopoli na London.
- Blogu ya EF - Tangazo la Sasisho la Arrow Glacier (inafunguka katika kichupo kipya)
- Ethereum Cat Herders - Sasisho la Arrow Glacier la Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-4345 – inachelewesha Bomu la ugumu hadi Juni 2022
Altair
27 Okt 2021, 10:56:23 UTC
Muhtasari
Sasisho la Altair lilikuwa sasisho la kwanza lililopangwa kwa ajili ya Mnyororo wa Beacon. Liliongeza usaidizi kwa "kamati za usawazishaji"—kuwezesha wateja wepesi, na kuongeza adhabu za kutofanya kazi kwa mthibitishaji na ukataji kadiri maendeleo yalivyokuwa yakielekea kwenye Unganisho.
Ukweli wa kufurahisha!
Altair lilikuwa sasisho kuu la kwanza la mtandao ambalo lilikuwa na muda kamili wa kutolewa. Kila sasisho la awali lilitegemea nambari ya kitalu iliyotangazwa kwenye mnyororo wa Uthibitisho wa Kazi, ambapo nyakati za kitalu hutofautiana. Mnyororo wa Beacon hauhitaji kutatua Uthibitisho wa Kazi, na badala yake hufanya kazi kwenye mfumo wa kipindi unaotegemea wakati unaojumuisha "sloti" 32 za sekunde kumi na mbili za wakati ambapo wathibitishaji wanaweza kupendekeza vitalu. Hii ndiyo sababu tulijua haswa ni lini tungefikia kipindi cha 74,240 na Altair kuanza kufanya kazi!
London
5 Ago 2021, 12:33:42 UTC
Muhtasari
Sasisho la London lilianzisha EIP-1559 (inafunguka katika kichupo kipya), ambalo lilifanyia mabadiliko soko la ada ya muamala, pamoja na mabadiliko ya jinsi marejesho ya gesi yanavyoshughulikiwa na ratiba ya .
Sasisho la London / EIP-1559 lilikuwa nini?
Kabla ya Sasisho la London, Ethereum ilikuwa na vitalu vyenye ukubwa uliowekwa. Katika nyakati za mahitaji makubwa ya mtandao, vitalu hivi vilifanya kazi kwa uwezo kamili. Kutokana na hili, watumiaji mara nyingi walilazimika kusubiri mahitaji yapungue ili kujumuishwa kwenye kitalu, jambo ambalo lilisababisha uzoefu mbaya kwa mtumiaji. Sasisho la London lilianzisha vitalu vyenye ukubwa unaobadilika kwenye Ethereum.
Njia ambayo ada za muamala kwenye mtandao wa Ethereum zilikokotolewa ilibadilika na Sasisho la London la Agosti 2021. Kabla ya sasisho la London, ada zilikokotolewa bila kutenganisha ada za base na priority, kama ifuatavyo:
Tuseme Alice alipaswa kumlipa Bob 1 ETH. Katika muamala huo, kikomo cha gesi ni uniti 21,000, na bei ya gesi ni Gwei 200.
Jumla ya ada ingekuwa: Gas units (limit) * Gas price per unit yaani 21,000 * 200 = 4,200,000 gwei au 0.0042 ETH
Utekelezaji wa EIP-1559 (inafunguka katika kichupo kipya) katika Sasisho la London ulifanya utaratibu wa ada ya muamala kuwa mgumu zaidi, lakini ulifanya ada za gesi kutabirika zaidi, na kusababisha soko la ada ya muamala lenye ufanisi zaidi. Watumiaji wanaweza kuwasilisha miamala yenye maxFeePerGas inayoendana na kiasi wanachokuwa tayari kulipa ili muamala utekelezwe, wakijua kwamba hawatalipa zaidi ya bei ya soko kwa gesi (baseFeePerGas), na kupata kiasi chochote cha ziada, ukiondoa ada yao ya kipaumbele, kurejeshwa.
Video hii inaelezea EIP-1559 na faida inazoleta: EIP-1559 Imefafanuliwa (inafunguka katika kichupo kipya)
- Je, wewe ni msanidi wa programu tumizi iliyogatuliwa (dapp)? Hakikisha unasasisha maktaba na zana zako. (inafunguka katika kichupo kipya)
- Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- Soma ufafanuzi wa Ethereum Cat Herders (inafunguka katika kichupo kipya)
Berlin
15 Apr 2021, 10:07:03 UTC
Muhtasari
Sasisho la Berlin liliboresha gharama ya gesi kwa vitendo fulani vya EVM, na kuongeza usaidizi kwa aina nyingi za muamala.
- Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- Soma ufafanuzi wa Ethereum Cat Herders (inafunguka katika kichupo kipya)
2020
Mwanzo wa Mnyororo wa Beacon
1 Des 2020, 12:00:23 UTC
Muhtasari
Mnyororo wa Beacon ulihitaji amana 16384 za ETH 32 zilizowekwa dhamana ili kuzinduliwa kwa usalama. Hili lilifanyika mnamo Novemba 27, na Mnyororo wa Beacon ulianza kuzalisha vitalu mnamo Desemba 1, 2020.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
Mnyororo wa Beacon
Mkataba wa amana ya uwekaji dhamana ulisambazwa
14 Okt 2020, 9:22:52 UTC
Muhtasari
Mkataba wa amana ya uwekaji dhamana ulileta kwenye mfumo wa ikolojia wa Ethereum. Ingawa ni mkataba wa , ulikuwa na athari ya moja kwa moja kwenye ratiba ya kuzindua Mnyororo wa Beacon, sasisho muhimu la Ethereum.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
Uwekaji dhamana
Muir Glacier
2 Jan 2020, 8:30:49 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa Muir Glacier ulileta ucheleweshaji kwenye . Ongezeko la ugumu wa kitalu kwenye utaratibu wa makubaliano wa Uthibitisho wa Kazi (PoW) lilitishia kushusha ubora wa matumizi ya Ethereum kwa kuongeza muda wa kusubiri wakati wa kutuma miamala na kutumia programu tumizi zilizogatuliwa (dapps).
- Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- Soma maelezo ya Ethereum Cat Herders (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-2384 – inachelewesha Bomu la ugumu kwa vitalu vingine 4,000,000, au takriban siku 611.
2019
Istanbuli
8 Des 2019, 0:25:09 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa Istanbuli:
- Iliboresha gharama ya kwa baadhi ya vitendo katika EVM.
- Iliboresha ustahimilivu dhidi ya mashambulizi ya kunyima huduma.
- Ilifanya suluhu za upanuzi wa tabaka la 2 (l2) zinazotegemea SNARKs na STARKs kuwa na utendaji bora zaidi.
- Iliwezesha Ethereum na Zcash kufanya kazi pamoja.
- Iliruhusu mikataba kuanzisha kazi za ubunifu zaidi.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-152 – kuruhusu Ethereum kufanya kazi na sarafu inayolinda faragha kama Zcash.
- EIP-1108 – kriptografia ya bei nafuu ili kuboresha gharama za .
- EIP-1344 – inailinda Ethereum dhidi ya mashambulizi ya kurudiwa kwa kuongeza
CHAINIDmsimbo wa operesheni. - EIP-1884 – kuboresha bei za gesi za msimbo wa operesheni kulingana na matumizi.
- EIP-2028 – inapunguza gharama ya data za mwito kuruhusu data zaidi katika vitalu – nzuri kwa upanuzi wa tabaka la 2 (l2).
- EIP-2200 – mabadiliko mengine ya bei ya gesi ya msimbo wa operesheni.
Konstantinopoli
28 Feb 2019, 19:52:04 UTC
Muhtasari
Mchepuko wa Constantinople:
- Ilipunguza tuzo za uchimbaji wa kitalu kutoka ETH 3 hadi 2.
- Ilihakikisha mnyororo wa vitalu haugandi kabla ya Uthibitisho wa Dau (PoS) kutekelezwa.
- Iliboresha gharama ya kwa baadhi ya vitendo katika EVM.
- Iliongeza uwezo wa kuingiliana na anwani ambazo bado hazijaundwa.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-145 – inaboresha gharama ya baadhi ya vitendo mnyororoni.
- EIP-1014 – inakuruhusu kuingiliana na anwani ambazo bado hazijaundwa.
- EIP-1052 – inaanzisha maagizo ya
EXTCODEHASHili kupata heshi ya msimbo wa mkataba mwingine. - EIP-1234 – inahakikisha mnyororo wa vitalu haugandi kabla ya Uthibitisho wa Dau (PoS) na kupunguza tuzo ya bloku kutoka ETH 3 hadi 2.
2017
Bizantiamu
16 Okt 2017, 5:22:11 UTC
Muhtasari
Mchepuko wa Byzantium:
- Imepunguza tuzo za uchimbaji wa kitalu kutoka ETH 5 hadi 3.
- Imechelewesha kwa mwaka mmoja.
- Imeongeza uwezo wa kufanya miito isiyobadilisha hali kwa mikataba mingine.
- Imeongeza mbinu fulani za kriptografia ili kuruhusu upanuaji wa tabaka la 2.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-140 – inaongeza msimbo wa operesheni wa
REVERT. - EIP-658 – sehemu ya hali imeongezwa kwenye stakabadhi za muamala ili kuonyesha mafanikio au kufeli.
- EIP-196 – inaongeza tao la duaradufu na uzidishaji wa skali ili kuruhusu ZK-Snarks.
- EIP-197 – inaongeza tao la duaradufu na uzidishaji wa skali ili kuruhusu ZK-Snarks.
- EIP-198 – inawezesha uthibitishaji wa sahihi wa RSA.
- EIP-211 – inaongeza usaidizi kwa thamani za kurejesha zenye urefu unaobadilika.
- EIP-214 – inaongeza msimbo wa operesheni wa
STATICCALL, ikiruhusu miito isiyobadilisha hali kwa mikataba mingine. - EIP-100 – inabadilisha fomula ya kurekebisha ugumu.
- EIP-649 – inachelewesha kwa mwaka 1 na kupunguza tuzo ya bloku kutoka ETH 5 hadi 3.
2016
Spurious Dragon
22 Nov 2016, 16:15:44 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa Spurious Dragon ulikuwa jibu la pili kwa mashambulizi ya kunyimwa huduma (DoS) kwenye mtandao (Septemba/Oktoba 2016) ikijumuisha:
- kurekebisha bei za msimbo wa operesheni ili kuzuia mashambulizi ya baadaye kwenye mtandao.
- kuwezesha "kupunguza mzigo" wa hali ya mnyororo wa vitalu.
- kuongeza ulinzi dhidi ya shambulio la kurudia.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-155 – inazuia miamala kutoka kwenye mnyororo mmoja wa Ethereum isitangazwe tena kwenye mnyororo mbadala, kwa mfano muamala wa mtandao wa majaribio kurudiwa kwenye mnyororo mkuu wa Ethereum.
- EIP-160 – inarekebisha bei za msimbo wa operesheni wa
EXP– inafanya iwe vigumu zaidi kupunguza kasi ya mtandao kupitia operesheni za mkataba zenye gharama kubwa za kikokotoo. - EIP-161 – inaruhusu kuondolewa kwa akaunti tupu zilizoongezwa kupitia mashambulizi ya DOS.
- EIP-170 – inabadilisha ukubwa wa juu zaidi wa msimbo ambao mkataba kwenye mnyororo wa vitalu unaweza kuwa nao – hadi baiti 24576.
Tangerine Whistle
18 Okt 2016, 13:19:31 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa Tangerine Whistle ulikuwa jibu la kwanza kwa mashambulizi ya kunyimwa huduma (DoS) kwenye mtandao (Septemba/Oktoba 2016) ikijumuisha:
- kushughulikia masuala ya dharura ya afya ya mtandao kuhusu misimbo ya operesheni iliyopangiwa bei ya chini.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- EIP-150 – inaongeza gharama za gesi za misimbo ya operesheni inayoweza kutumika katika mashambulizi ya barua taka.
- EIP-158 – inapunguza ukubwa wa hali kwa kuondoa idadi kubwa ya akaunti tupu zilizowekwa kwenye hali kwa gharama ya chini sana kutokana na kasoro katika matoleo ya awali ya itifaki ya Ethereum.
Mchepuo wa DAO
20 Jul 2016, 13:20:40 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa DAO ulikuwa jibu kwa shambulio la DAO la 2016 (inafunguka katika kichupo kipya) ambapo usio salama ulipoteza zaidi ya ETH milioni 3.6 katika udukuzi. Mchepuo huo ulihamisha fedha kutoka kwenye mkataba wenye kasoro kwenda kwenye mkataba mpya (inafunguka katika kichupo kipya) wenye kazi moja: kutoa. Yeyote aliyepoteza fedha angeweza kutoa ETH 1 kwa kila tokeni 100 za DAO kwenye pochi zao.
Hatua hii ilipigiwa kura na jamii ya Ethereum. Mmiliki yeyote wa ETH aliweza kupiga kura kupitia muamala kwenye jukwaa la kupiga kura (inafunguka katika kichupo kipya). Uamuzi wa kuchepuka ulifikia zaidi ya 85% ya kura.
Baadhi ya wachimbaji walikataa kuchepuka kwa sababu tukio la DAO halikuwa kasoro katika itifaki. Waliendelea na kuunda Ethereum Asilia (inafunguka katika kichupo kipya).
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
Homstedi
14 Mac 2016, 18:49:53 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa Homstedi ambao uliangalia siku zijazo. Ulijumuisha mabadiliko kadhaa ya itifaki na mabadiliko ya mtandao ambayo yaliipa Ethereum uwezo wa kufanya masasisho zaidi ya mtandao.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
2015
Kuyeyuka kwa Eneo Jipya
7 Sep 2015, 21:33:09 UTC
Muhtasari
Mchepuo wa kuyeyuka kwa Eneo Jipya uliondoa kikomo cha 5,000 kwa kila na kuweka bei chaguo-msingi ya gesi kuwa 51. Hii iliruhusu miamala – miamala inahitaji gesi 21,000. lilianzishwa ili kuhakikisha mchepuo mgumu wa baadaye kwenda kwenye .
- Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
- Soma Sasisho la 1 la Itifaki ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
Eneo Jipya
30 Jul 2015, 15:26:13 UTC
Muhtasari
Eneo Jipya lilikuwa utekelezaji wa moja kwa moja, lakini wa kimsingi sana wa mradi wa Ethereum. Lilifuatia awamu ya majaribio ya Olympic iliyofanikiwa. Lilikusudiwa kwa watumiaji wa kiufundi, haswa wasanidi programu. vilikuwa na kikomo cha cha 5,000. Kipindi hiki cha 'kuyeyuka' kiliwawezesha wachimbaji kuanza shughuli zao na kwa watumiaji wa mapema kusakinisha wateja wao bila kulazimika 'kuharakisha'.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
2014
Mauzo ya Etha
22 Jul 2014, 0:00:00 UTC
Etha iliuzwa rasmi kwa siku 42. Ungeweza kuinunua kwa BTC.
Soma tangazo la Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya)
Waraka wa manjano watolewa
1 Apr 2014, 0:00:00 UTC
Waraka wa Manjano, ulioandikwa na Dkt. Gavin Wood, ni ufafanuzi wa kiufundi wa itifaki ya Ethereum.
Tazama Waraka wa Manjano (inafunguka katika kichupo kipya)
2013
Waraka mweupe umetolewa
27 Nov 2013, 0:00:00 UTC
Waraka wa utangulizi, uliochapishwa mwaka wa 2013 na Vitalik Buterin, mwanzilishi wa Ethereum, kabla ya uzinduzi wa mradi mnamo 2015.
Waraka mweupe