Viwango vya Uendelezaji vya Ethereum
Muhtasari wa viwango
Jumuiya ya Ethereum imepitisha viwango vingi vinavyosaidia kuweka miradi (kama vile wateja wa Ethereum na pochi) inayoingiliana katika utekelezaji wote, na kuhakikisha mikataba mahiri na programu tumizi zilizogatuliwa (dapps) zinasalia kuwa zinazoweza kuunganishwa.
Kwa kawaida viwango huletwa kama Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs), ambayo hujadiliwa na wanajumuiya kupitia mchakato wa kawaida (inafunguka katika kichupo kipya).
- Utangulizi wa EIPs
- Orodha ya EIPs (inafunguka katika kichupo kipya)
- Hifadhi ya GitHub ya EIP (inafunguka katika kichupo kipya)
- Ubao wa majadiliano wa EIP (inafunguka katika kichupo kipya)
- Utangulizi wa Utawala wa Ethereum
- Muhtasari wa Utawala wa Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya) Machi 31, 2019 - Boris Mann
- Utawala wa Uendelezaji wa Itifaki ya Ethereum na Uratibu wa Uboreshaji wa Mtandao (inafunguka katika kichupo kipya) Machi 23, 2020 - Hudson Jameson
- Orodha ya kucheza ya Mikutano yote ya Wasanidi Wakuu wa Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya) (Orodha ya kucheza ya YouTube)
Aina za viwango
Kuna aina 3 za EIPs:
- Njia ya Viwango: inaelezea mabadiliko yoyote yanayoathiri utekelezaji mwingi au wote wa Ethereum
- Njia ya Meta (inafunguka katika kichupo kipya): inaelezea mchakato unaozunguka Ethereum au inapendekeza mabadiliko kwenye mchakato
- Njia ya Taarifa (inafunguka katika kichupo kipya): inaelezea suala la muundo wa Ethereum au inatoa miongozo ya jumla au taarifa kwa jumuiya ya Ethereum
Zaidi ya hayo, Njia ya Viwango imegawanywa katika makundi 4:
- Msingi (inafunguka katika kichupo kipya): maboresho yanayohitaji mchepuo wa mwafaka
- Mtandao (inafunguka katika kichupo kipya): maboresho kuhusu devp2p na Itifaki Ndogo ya Ethereum Nyepesi, pamoja na maboresho yaliyopendekezwa kwa vipimo vya itifaki ya mtandao vya whisper na Kundi.
- Kiolesura (inafunguka katika kichupo kipya): maboresho kuhusu vipimo na viwango vya API/RPC vya mteja, na viwango fulani vya kiwango cha lugha kama vile majina ya mbinu na ABIs za mkataba.
- ERC (inafunguka katika kichupo kipya): viwango na taratibu za kiwango cha programu
Taarifa za kina zaidi kuhusu aina na makundi haya tofauti zinaweza kupatikana katika EIP-1 (inafunguka katika kichupo kipya)
Viwango vya tokeni
- ERC-20 - Kiolesura cha kawaida cha tokeni zinazoweza kubadilishana, kama vile tokeni za kura, tokeni za uwekaji dhamana au sarafu za mtandaoni.
- ERC-223 - Kiwango cha tokeni zinazoweza kubadilishana kinachofanya tokeni zifanye kazi sawa na Etha na inasaidia ushughulikiaji wa uhamishaji wa tokeni upande wa wapokeaji.
- ERC-1363 - Kiolesura cha kiendelezi cha tokeni za ERC-20 kinachosaidia kutekeleza wito wa kurudi kwenye mikataba ya mpokeaji katika muamala mmoja.
- ERC-721 - Kiolesura cha kawaida cha tokeni zisizoweza kubadilishana, kama vile hati ya mchoro au wimbo.
- ERC-2309 (inafunguka katika kichupo kipya) - Tukio la kawaida linalotolewa wakati wa kuunda/kuhamisha tokeni moja, au nyingi zisizoweza kubadilishana kwa kutumia vitambulisho vya tokeni vinavyofuatana.
- ERC-4400 (inafunguka katika kichupo kipya) - Kiendelezi cha kiolesura cha jukumu la mtumiaji la EIP-721.
- ERC-4907 (inafunguka katika kichupo kipya) - Ongeza jukumu lenye ukomo wa muda na ruhusa zilizozuiliwa kwenye tokeni za ERC-721.
- ERC-777 - (HAIPENDEKEZWI) Kiwango cha tokeni kinachoboresha ERC-20.
- ERC-1155 - Kiwango cha tokeni kinachoweza kuwa na rasilimali zinazoweza kubadilishana na zisizoweza kubadilishana.
- ERC-4626 - Kiwango cha hifadhi iliyowekwa tokeni iliyoundwa ili kuboresha na kuunganisha vigezo vya kiufundi vya hifadhi zinazozalisha faida.
Jifunze zaidi kuhusu viwango vya tokeni.
Usomaji zaidi
Unajua rasilimali ya jumuiya iliyokusaidia? Hariri ukurasa huu na uiongeze!