Ethereum kwa wasanidi wa Dart
Kuanza na mikataba mahiri na lugha ya Solidity
Mafunzo
- Flutter na Mnyororo wa vitalu – Dapp ya Hello World (inafunguka katika kichupo kipya) inakupeleka kupitia hatua zote ili kuanza:
- Kuandika mkataba mahiri katika Solidity (inafunguka katika kichupo kipya)
- Kuandika kiolesura cha mtumiaji katika Dart
- Kujenga dapp ya Simu na Flutter (inafunguka katika kichupo kipya) ni fupi zaidi, ambayo inaweza kuwa bora ikiwa tayari unajua mambo ya msingi
- Ikiwa unapendelea kujifunza kwa kutazama video, unaweza kutazama Jenga Programu Yako ya Kwanza ya Flutter ya Mnyororo wa vitalu (inafunguka katika kichupo kipya), ambayo ina urefu wa takriban saa moja
- Ikiwa huna subira, unaweza kupendelea Kujenga Programu tumizi iliyogatuliwa ya Mnyororo wa vitalu na Flutter na Dart kwenye Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya), ambayo ni takriban dakika ishirini tu
- Kuunganisha MetaMask katika programu ya Flutter na Web3Modal na WalletConnect (inafunguka katika kichupo kipya) - video hii fupi inakupeleka kupitia hatua za kuunganisha MetaMask kwenye programu zako za Flutter na maktaba ya Web3Modal (inafunguka katika kichupo kipya) ya WalletConnect
- Kozi ya Kambi ya Mafunzo ya Msanidi wa Mnyororo wa vitalu wa Simu na Solidity & Flutter (inafunguka katika kichupo kipya) - orodha ya kucheza ya kozi ya msanidi wa mnyororo wa vitalu wa simu wa full stack
Kufanya kazi na wateja wa Ethereum
Unaweza kutumia Ethereum kuunda programu tumizi zilizogatuliwa (au "dapps") zinazotumia faida za sarafu-fiche na teknolojia ya mnyororo wa vitalu. Kuna angalau maktaba mbili zinazodumishwa kwa sasa za Dart ili kutumia JSON-RPC API kwa ajili ya Ethereum.
- Web3dart kutoka pwa.ir (inafunguka katika kichupo kipya)
- Ethereum 5.0.0 kutoka darticulate.com (inafunguka katika kichupo kipya)
Pia kuna maktaba za ziada zinazokuruhusu kudhibiti anwani maalum za Ethereum, au zinazokuruhusu kupata bei za sarafu-fiche mbalimbali. Unaweza kuona orodha kamili hapa (inafunguka katika kichupo kipya).