DAO ni nini?
DAO ni shirika linalomilikiwa kwa pamoja linalofanya kazi kufikia lengo la pamoja.
DAO huturuhusu kufanya kazi na watu wenye nia moja kote ulimwenguni bila kumwamini kiongozi mkarimu kusimamia fedha au shughuli. Hakuna Mkurugenzi Mtendaji (CEO) anayeweza kutumia fedha apendavyo au Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) anayeweza kuchezea vitabu vya hesabu. Badala yake, sheria zinazotegemea mnyororo wa vitalu zilizowekwa kwenye msimbo hufafanua jinsi shirika linavyofanya kazi na jinsi fedha zinavyotumika.
Zina hazina zilizojengewa ndani ambazo hakuna mtu aliye na mamlaka ya kuzifikia bila idhini ya kikundi. Maamuzi yanatawaliwa na mapendekezo na kura ili kuhakikisha kila mtu katika shirika ana sauti, na kila kitu kinafanyika kwa uwazi .
Kwa nini tunahitaji DAO?
Kuanzisha shirika na mtu ambalo linahusisha ufadhili na pesa kunahitaji uaminifu mkubwa kwa watu unaofanya nao kazi. Lakini ni vigumu kumwamini mtu ambaye umewahi kuwasiliana naye kwenye mtandao pekee. Ukiwa na DAO huhitaji kumwamini mtu mwingine yeyote katika kikundi, isipokuwa msimbo wa DAO, ambao ni wazi kwa 100% na unaweza kuthibitishwa na mtu yeyote.
Hii inafungua fursa nyingi mpya za ushirikiano na uratibu wa kimataifa.
Ulinganisho
| DAO | Shirika la kitamaduni |
|---|---|
| Kawaida ni tambarare, na la kidemokrasia kikamilifu. | Kawaida lina mfumo wa kitabaka. |
| Kura inahitajika na wanachama ili mabadiliko yoyote yatekelezwe. | Kulingana na muundo, mabadiliko yanaweza kudaiwa kutoka kwa upande mmoja, au upigaji kura unaweza kutolewa. |
| Kura huhesabiwa, na matokeo kutekelezwa kiotomatiki bila mpatanishi anayeaminika. | Ikiwa upigaji kura unaruhusiwa, kura huhesabiwa ndani, na matokeo ya upigaji kura lazima yashughulikiwe kwa mikono. |
| Huduma zinazotolewa hushughulikiwa kiotomatiki kwa njia iliyogatuliwa (kwa mfano usambazaji wa fedha za hisani). | Inahitaji ushughulikiaji wa binadamu, au otomatiki inayodhibitiwa na kituo kikuu, ambayo inaweza kuchezewa. |
| Shughuli zote ni wazi na za umma kikamilifu. | Shughuli kwa kawaida ni za faragha, na zimezuiwa kwa umma. |
Mifano ya DAO
Ili kusaidia hili kuleta maana zaidi, hapa kuna mifano michache ya jinsi unavyoweza kutumia DAO:
- Shirika la hisani – unaweza kupokea michango kutoka kwa mtu yeyote duniani na kupiga kura kuhusu malengo yapi ya kufadhili.
- Umiliki wa pamoja – mnaweza kununua rasilimali za kimwili au za kidijitali na wanachama wanaweza kupiga kura kuhusu jinsi ya kuzitumia.
- Miradi na ruzuku – unaweza kuunda mfuko wa mradi unaokusanya mtaji wa uwekezaji na kupiga kura kuhusu miradi ya kuunga mkono. Pesa zilizolipwa zinaweza kugawiwa tena baadaye miongoni mwa wanachama wa DAO.
DAO zinafanyaje kazi?
Uti wa mgongo wa DAO ni wake, ambao hufafanua sheria za shirika na kushikilia hazina ya kikundi. Pindi mkataba unapokuwa hewani kwenye Ethereum, hakuna anayeweza kubadilisha sheria isipokuwa kwa kura. Ikiwa mtu yeyote atajaribu kufanya jambo ambalo halijashughulikiwa na sheria na mantiki katika msimbo, litashindwa. Na kwa sababu hazina inafafanuliwa na mkataba mahiri pia inamaanisha hakuna anayeweza kutumia pesa bila idhini ya kikundi pia. Hii inamaanisha kuwa DAO hazihitaji mamlaka kuu. Badala yake, kikundi hufanya maamuzi kwa pamoja, na malipo huidhinishwa kiotomatiki kura zinapopita.
Hili linawezekana kwa sababu mikataba mahiri haiwezi kuchezewa pindi inapoanza kufanya kazi kwenye Ethereum. Huwezi tu kuhariri msimbo (sheria za DAO) bila watu kugundua kwa sababu kila kitu kiko wazi.
Ethereum na DAO
Ethereum ni msingi kamili wa DAO kwa sababu kadhaa:
- Mwafaka wa Ethereum wenyewe umejengwa kwa ugatuzi na umeimarika vya kutosha kwa mashirika kuamini mtandao.
- Msimbo wa mkataba mahiri hauwezi kurekebishwa pindi unapokuwa hewani, hata na wamiliki wake. Hii inaruhusu DAO kuendeshwa kwa sheria iliyopangwa nayo.
- Mikataba mahiri inaweza kutuma/kupokea fedha. Bila hili ungehitaji mpatanishi anayeaminika kusimamia fedha za kikundi.
- Jumuiya ya Ethereum imethibitisha kuwa yenye ushirikiano zaidi kuliko ushindani, ikiruhusu mbinu bora na mifumo ya usaidizi kuibuka haraka.
Utawala wa DAO
Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kutawala DAO, kama vile jinsi upigaji kura na mapendekezo yanavyofanya kazi.
Ukaimishaji
Ukaimishaji ni kama toleo la DAO la demokrasia ya uwakilishi. Wamiliki wa tokeni hukaimisha kura kwa watumiaji wanaojiteua na kujitolea kusimamia itifaki na kuendelea kufahamishwa.
Mfano maarufu
ENS (opens in a new tab) – Wamiliki wa ENS wanaweza kukaimisha kura zao kwa wanachama wa jumuiya wanaoshiriki ili kuwawakilisha.
Utawala wa muamala wa kiotomatiki
Katika DAO nyingi, miamala itatekelezwa kiotomatiki ikiwa akidi ya wanachama itapiga kura ya ndiyo.
Mfano maarufu
Nouns (opens in a new tab) – Katika Nouns DAO, muamala hutekelezwa kiotomatiki ikiwa akidi ya kura inafikiwa na wengi wanapiga kura ya ndiyo, mradi tu haijapigiwa kura ya turufu na waanzilishi.
Utawala wa saini-nyingi
Ingawa DAO zinaweza kuwa na maelfu ya wanachama wanaopiga kura, fedha zinaweza kuishi katika unaoshirikiwa na wanachama 5-20 wa jumuiya wanaofanya kazi ambao wanaaminika na kwa kawaida wanajulikana (vitambulisho vya umma vinavyojulikana kwa jumuiya). Baada ya kura, watia saini wa hutekeleza matakwa ya jumuiya.
Sheria za DAO
Mnamo 1977, Wyoming ilivumbua LLC, ambayo inalinda wajasiriamali na kupunguza dhima yao. Hivi karibuni zaidi, walianzisha sheria ya DAO ambayo inaweka hadhi ya kisheria kwa DAO. Kwa sasa Wyoming, Vermont, na Visiwa vya Virgin vina sheria za DAO kwa namna fulani.
Mfano maarufu
CityDAO (opens in a new tab) – CityDAO ilitumia sheria ya DAO ya Wyoming kununua ekari 40 za ardhi karibu na Hifadhi ya Kitaifa ya Yellowstone.
Uanachama wa DAO
Kuna miundo tofauti ya uanachama wa DAO. Uanachama unaweza kuamua jinsi upigaji kura unavyofanya kazi na sehemu nyingine muhimu za DAO.
Uanachama unaotegemea tokeni
Kawaida huwa kikamilifu, kulingana na tokeni inayotumika. Mara nyingi tokeni hizi za utawala zinaweza kuuzwa bila ruhusa kwenye . Nyingine lazima zipatikane kupitia kutoa ukwasi au 'Uthibitisho wa Kazi (PoW)' mwingine. Vyovyote vile, kushikilia tu tokeni kunatoa ufikiaji wa kupiga kura.
Kwa kawaida hutumika kutawala itifaki pana zilizogatuliwa na/au tokeni zenyewe.
Mfano maarufu
MakerDAO (opens in a new tab) – Tokeni ya MakerDAO ya MKR inapatikana kwa wingi kwenye masoko ya ubadilishanaji yaliyogatuliwa na mtu yeyote anaweza kununua ili kuwa na uwezo wa kupiga kura kuhusu mustakabali wa itifaki ya Maker.
Uanachama unaotegemea hisa
DAO zinazotegemea hisa zina ruhusa zaidi, lakini bado ziko wazi kabisa. Wanachama wowote watarajiwa wanaweza kuwasilisha pendekezo la kujiunga na DAO, kwa kawaida wakitoa mchango wa thamani fulani kwa njia ya tokeni au kazi. Hisa zinawakilisha uwezo wa moja kwa moja wa kupiga kura na umiliki. Wanachama wanaweza kujitoa wakati wowote na sehemu yao sawia ya hazina.
Kwa kawaida hutumika kwa mashirika yaliyoungana zaidi, yanayozingatia binadamu kama vile mashirika ya hisani, vikundi vya wafanyakazi, na vilabu vya uwekezaji. Pia inaweza kutawala itifaki na tokeni vilevile.
Uanachama unaotegemea sifa
Sifa inawakilisha uthibitisho wa ushiriki na inatoa uwezo wa kupiga kura katika DAO. Tofauti na uanachama unaotegemea tokeni au hisa, DAO zinazotegemea sifa hazihamishi umiliki kwa wachangiaji. Sifa haiwezi kununuliwa, kuhamishwa au kukaimishwa; Wanachama wa DAO lazima wapate sifa kupitia ushiriki. Upigaji kura mnyororoni ni bila ruhusa na wanachama watarajiwa wanaweza kuwasilisha mapendekezo kwa uhuru ya kujiunga na DAO na kuomba kupokea sifa na tokeni kama tuzo badala ya michango yao.
Kwa kawaida hutumika kwa maendeleo yaliyogatuliwa na utawala wa itifaki na , lakini pia inafaa kwa seti tofauti za mashirika kama vile mashirika ya hisani, vikundi vya wafanyakazi, vilabu vya uwekezaji, n.k.
Mfano maarufu
DXdao (opens in a new tab) – DXdao ilikuwa kikundi huru cha kimataifa kinachojenga na kutawala itifaki na programu zilizogatuliwa tangu 2019. Ilitumia utawala unaotegemea sifa na kuratibu na kusimamia fedha, ikimaanisha hakuna mtu angeweza kununua njia yake ya kushawishi mustakabali wake au utawala.
Jiunge / anza DAO
Jiunge na DAO
- DAO za jumuiya ya Ethereum
- Orodha ya DAO ya DAOHaus (opens in a new tab)
- Orodha ya DAO ya Tally.xyz (opens in a new tab)
- Orodha ya DAO ya DeGov.AI (opens in a new tab)
Anzisha DAO
- Anzisha DAO ukitumia DAOHaus (opens in a new tab)
- Anzisha DAO ya Gavana ukitumia Tally (opens in a new tab)
- Unda DAO inayoendeshwa na Aragon (opens in a new tab)
- Anzisha koloni (opens in a new tab)
- Zindua DAO ukitumia Kizinduzi cha DeGov (opens in a new tab)
Usomaji zaidi
Makala za DAO
- DAO ni nini? (opens in a new tab) – Aragon (opens in a new tab)
- Nyumba ya DAO (opens in a new tab) – Metagame (opens in a new tab)
- DAO ni nini na inatumika kwa ajili gani? (opens in a new tab) – DAOhaus (opens in a new tab)
- Jinsi ya Kuanzisha Jumuiya ya Kidijitali Inayoendeshwa na DAO (opens in a new tab) – DAOhaus (opens in a new tab)
- DAO ni nini? (opens in a new tab) – Coinmarketcap (opens in a new tab)
- Mwafaka wa Holagrafia ni nini? (opens in a new tab) - DAOstack (opens in a new tab)
- DAO sio mashirika: ambapo ugatuzi katika mashirika yanayojitegemea ni muhimu na Vitalik (opens in a new tab)
- DAO, DAC, DA na Zaidi: Mwongozo Usiokamilika wa Istilahi (opens in a new tab) - Blogu ya Ethereum (opens in a new tab)
Video
- DAO ni nini katika kripto? (opens in a new tab)
- Je, DAO Inaweza Kujenga Jiji? (opens in a new tab) – TED (opens in a new tab)
