Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Endesha nodi

Chukua udhibiti kamili.
Endesha nodi yako mwenyewe.

Kuwa na mamlaka kamili huku ukisaidia kulinda mtandao. Kuwa Ethereum.

Nini maana ya "kuendesha nodi"?

Endesha programu.

Inayojulikana kama 'mteja', programu hii hupakua nakala ya mnyororo wa vitalu wa Ethereum na kuthibitisha uhalali wa kila kitalu, kisha huiweka kisasisho na vitalu na miamala mipya, na kusaidia wengine kupakua na kusasisha nakala zao wenyewe.

Na vifaa.

Ethereum imeundwa kuendesha nodi kwenye kompyuta za wastani za kiwango cha watumiaji. Unaweza kutumia kompyuta yoyote ya kibinafsi, lakini watumiaji wengi huchagua kuendesha nodi yao kwenye vifaa maalum ili kuondoa athari za utendaji kwenye mashine yao na kupunguza muda wa kupumzika wa nodi.

Ukiwa mtandaoni.

Kuendesha nodi ya Ethereum kunaweza kusikika kuwa ngumu mwanzoni, lakini ni kitendo tu cha kuendesha programu ya mteja kila wakati kwenye kompyuta huku ukiwa umeunganishwa kwenye intaneti. Ukiwa nje ya mtandao, nodi yako haitafanya kazi hadi irudi mtandaoni na kupata mabadiliko ya hivi punde.

Nani anapaswa kuendesha nodi?

Kila mtu! Nodi si za wathibitishaji wa pekee. Mtu yeyote anaweza kuendesha nodi—hata huhitaji ETH.

Huhitaji ya ETH ili kuendesha nodi. Kwa kweli, ni kila nodi nyingine kwenye Ethereum inayowawajibisha wathibitishaji.

Huenda usipate zawadi za kifedha ambazo wathibitishaji hupata, lakini kuna faida nyingine nyingi za kuendesha nodi kwa mtumiaji yeyote wa Ethereum kuzingatia, ikiwa ni pamoja na faragha, usalama, kupunguza utegemezi kwa seva za wahusika wengine, ustahimilivu wa udhibiti na kuboresha afya na ugatuzi wa mtandao.

Kuwa na nodi yako mwenyewe inamaanisha huhitaji kuamini taarifa kuhusu hali ya mtandao inayotolewa na mhusika wa tatu.

Usiamini. Thibitisha.

Kwa nini uendeshe nodi?

Unapotuma miamala kwa kutumia nodi za umma, taarifa za kibinafsi zinaweza kuvuja kwa huduma hizi za wahusika wengine kama vile anwani yako ya IP na anwani zipi za Ethereum unazomiliki.

Kwa kuelekeza mikoba inayooana kwenye nodi yako mwenyewe unaweza kutumia mkoba wako kuingiliana kwa faragha na kwa usalama na mnyororo wa vitalu.

Pia, ikiwa nodi hasidi inasambaza muamala batili, nodi yako itaupuuza tu. Kila muamala unathibitishwa ndani ya mashine yako mwenyewe, kwa hivyo huhitaji kumwamini mtu yeyote.

Nodi ya mhusika wa tatu inaweza kuchagua kukataa miamala kutoka kwa anwani mahususi za IP, au miamala inayohusisha akaunti mahususi, na hivyo kukuzuia kutumia mtandao unapouhitaji.

Kuwa na nodi yako mwenyewe ya kuwasilisha miamala kunahakikisha kwamba unaweza kutangaza muamala wako kwa mtandao mwingine wa rika-kwa-rika wakati wowote.

Kwa kuendesha nodi unakuwa sehemu ya harakati za kimataifa za kugatua udhibiti na nguvu juu ya ulimwengu wa habari.

Ikiwa wewe ni mmiliki, leta thamani kwa ETH yako kwa kusaidia afya na ugatuzi wa mtandao, na uhakikishe una sauti katika mustakabali wake.

Seva kuu za wingu zinaweza kutoa nguvu nyingi za kompyuta, lakini hutoa lengo kwa mataifa au washambuliaji wanaotaka kuvuruga mtandao.

Ustahimilivu wa mtandao unapatikana kwa nodi zaidi, katika maeneo tofauti ya kijiografia, zinazoendeshwa na watu wengi wa asili tofauti. Kadiri watu wengi wanavyoendesha nodi zao wenyewe, utegemezi wa pointi kuu za kushindwa hupungua, na kufanya mtandao kuwa na nguvu zaidi.

Katika tukio la mchepuo wa mnyororo, ambapo minyororo miwili inaibuka na seti mbili tofauti za sheria, kuendesha nodi yako mwenyewe kunahakikisha uwezo wako wa kuchagua ni seti gani ya sheria unayounga mkono. Ni juu yako kusasisha kwa sheria mpya na kuunga mkono mabadiliko yaliyopendekezwa, au la.

Ikiwa unaweka dhamana ya ETH, kuendesha nodi yako mwenyewe hukuruhusu kuchagua mteja wako mwenyewe, ili kupunguza hatari yako ya ukataji na kukabiliana na mahitaji yanayobadilika ya mtandao kwa wakati. Kuweka dhamana na mhusika wa tatu kunapoteza kura yako kuhusu mteja yupi unayefikiri ni chaguo bora zaidi.

Mkoba wa Ethereum hukuruhusu kuchukua ulinzi na udhibiti kamili wa mali zako za kidijitali kwa kushikilia funguo za faragha za anwani zako, lakini funguo hizo hazikuambii hali ya sasa ya mnyororo wa vitalu, kama vile salio la mkoba wako.

Kwa chaguo-msingi, mikoba ya Ethereum kwa kawaida hufikia nodi ya mhusika wa tatu, kama vile Infura au Alchemy, unapotafuta salio lako. Kuendesha nodi yako mwenyewe hukuruhusu kuwa na nakala yako mwenyewe ya mnyororo wa vitalu wa Ethereum.


Kuanza

Katika siku za awali za mtandao, watumiaji walihitaji kuwa na uwezo wa kuingiliana na mstari wa amri ili kuendesha nodi ya Ethereum.

Ikiwa hili ndilo pendeleo lako, na una ujuzi, jisikie huru kuangalia hati zetu za kiufundi.

Anzisha nodi ya Ethereum 

Sasa tuna DAppNode, ambayo ni programu ya bure na ya chanzo wazi inayowapa watumiaji uzoefu unaofanana na programu wakati wa kusimamia nodi yao.

Kwa kugonga mara chache tu unaweza kuwa na nodi yako inafanya kazi.

DAppNode hurahisisha watumiaji kuendesha nodi kamili, pamoja na na mitandao mingine ya , bila hitaji la kugusa mstari wa amri. Hii inafanya iwe rahisi kwa kila mtu kushiriki na kuunda mtandao uliogatuliwa zaidi.

Chagua tukio lako

Utahitaji baadhi ya vifaa ili kuanza. Ingawa kuendesha programu ya nodi kunawezekana kwenye kompyuta ya kibinafsi, kuwa na mashine maalum kunaweza kuongeza sana utendaji wa nodi yako huku ukipunguza athari zake kwenye kompyuta yako kuu.

Wakati wa kuchagua vifaa, zingatia kwamba mnyororo unakua kila wakati, na matengenezo yatahitajika bila shaka. Kuongeza vipimo kunaweza kusaidia kuchelewesha hitaji la matengenezo ya nodi.

Nunua iliyosheheni kikamilifu

Agiza chaguo la kuchomeka na kutumia kutoka kwa wachuuzi kwa uzoefu rahisi zaidi wa uingizaji.

  • Hakuna ujenzi unaohitajika.
  • Usanidi unaofanana na programu na GUI.
  • Hakuna mstari wa amri unaohitajika.

Jenga yako mwenyewe

Chaguo la bei nafuu na linaloweza kubinafsishwa zaidi kwa watumiaji wa kiufundi zaidi.

  • Tafuta sehemu zako mwenyewe.
  • Sakinisha DAppNode.
  • Au, chagua mfumo wako wa uendeshaji na wateja.

Jenga yako mwenyewe

Hatua ya 1 – Vifaa

Vipimo vya chini

Inayopendekezwa

  • Intel NUC, kizazi cha 7 au cha juu zaidi

    Kichakataji cha x86

  • Muunganisho wa intaneti wa waya

    Sio lazima, lakini hutoa usanidi rahisi na muunganisho thabiti zaidi

  • Skrini ya kuonyesha na kibodi

    Isipokuwa unatumia DAppNode, au usanidi wa ssh/bila skrini

Hatua ya 2 – Programu

Chaguo la 1 – DAppNode

Ukiwa tayari na vifaa vyako, mfumo wa uendeshaji wa DAppNode unaweza kupakuliwa kwa kutumia kompyuta yoyote na kusakinishwa kwenye SSD mpya kupitia hifadhi ya USB.

Chaguo la 2 – Mstari wa amri

Kwa udhibiti wa juu zaidi, watumiaji wenye uzoefu wanaweza kupendelea kutumia mstari wa amri badala yake.

Tazama hati zetu za wasanidi programu kwa maelezo zaidi kuhusu kuanza na uteuzi wa mteja.

Tafuta wasaidizi

Mifumo ya mtandaoni kama vile Discord au Reddit ni nyumbani kwa idadi kubwa ya wajenzi wa jamii walio tayari kukusaidia kwa maswali yoyote unayoweza kukutana nayo.

Usiifanye peke yako. Ikiwa una swali kuna uwezekano mtu hapa anaweza kukusaidia kupata jibu.

Usomaji zaidi


Unapanga kuweka dhamana?

Ili kuongeza ufanisi wa mthibitishaji wako, kiwango cha chini cha GB 16 za RAM kinapendekezwa, lakini GB 32 ni bora zaidi, na alama ya kipimo cha CPU ya 6667+ kwenye cpubenchmark.net (opens in a new tab). Inapendekezwa pia kwamba waweka dhamana wawe na ufikiaji wa kipimo data cha intaneti cha kasi ya juu kisicho na kikomo, ingawa hili si hitaji la lazima.

EthStaker inaingia kwa undani zaidi katika kipindi hiki maalum cha saa moja - Jinsi ya kununua vifaa vya mthibitishaji wa Ethereum (opens in a new tab)

Dokezo kuhusu Raspberry Pi (kichakataji cha ARM)

Raspberry Pi ni kompyuta nyepesi na za bei nafuu, lakini zina mapungufu ambayo yanaweza kuathiri utendaji wa nodi yako. Ingawa hazipendekezwi kwa sasa kwa uwekaji dhamana, hizi zinaweza kuwa chaguo bora na la bei nafuu la kuendesha nodi kwa matumizi ya kibinafsi, zikiwa na RAM ndogo kama GB 4 - 8.

Pima ujuzi wako wa Ethereum