Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Saidia kusasisha ukurasa huu

๐ŸŒ

Kuna toleo jipya la ukurasa huu ila liko kwenye Kiingereza tu hivi sasa. Tusaidie kutafsiri toleo jipya zaidi.

Tafsiri ukurasa
Angalia Kiingereza

Hapana hitilafu hapa!๐Ÿ›

Ukurasa huu hautafsiriwi. Tumeuacha ukurasa huu kwa Kiingereza kwa sasa.

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 18 Machi 2023

Ninaweza kushiriki vipi?

Jumuiya ya Ethereum inahusisha watu wa asili tofauti na wenye ujuzi wa kila aina. Endapo wewe ni msanii, msimbuaji au mhasibu, kuna njia za kujihusisha. Hii ni orodha ya mapendekezo yanayoweza kukusaidia.

Wasimbuaji ๐Ÿ’ป

  • Jifunze kuhusu Ethereum na ijaribishe kwenye etehereum.org/developers/
  • Tafuta fadhila kwenye Gitcoin, fanyia kazi itilafu ndogo ama kubwa na ujipatie kripto!
  • Shiriki kwenyeETHGlobalhackathon iliyokaribu nawe!
  • Vinjari juu ya miradi inayohusiana na taaluma yako au lugha ya usimbuajiutakayochagua.
  • Tazama au shiriki kwenye mikutano ya wasimbuaji wa ndani
  • Orodha pendekezwa ya kuunga mkono Ikolojia ya Ethereum - maeneo amabayo Ikolojia ya Ethereum inatafuta maombi ya fedha kwa ajili ya vifaa, nyaraka, na miundombinu
  • Daraja la Web3 - jiunge na wapenzi wa web3 kwenye mpango wa kutambua, kujifunza, na kuunga mkono mamia ya wasanidi programu na wanachama Afrika

Watafiti & Taaluma ๐Ÿ”

Una taaluma ya hisabati, kriptografia ama uchumi? Unaweza kupenda kazi za viwango vya juu, zilizofanywa na ikolojia ya Ethereum

Seti zisizo za kiufundi ๐Ÿ’ผ

Kama wewe sio msanidi programu, inaweza kua vigumu kujua ni wapi unapaswa kuanzia kwenye Ethereum. Kuna mapendekezo kadhaa, pamoja nayo ni vyanzo maalumu kwa kila asili ya taaluma.

Panga kikao kwenye mji wako

Andika maudhui kuhusu Ethereum

  • Ethereum inahitaji waandishi wazuri wanaoweza kuelezea thamani yake kwa kutumia lugha rahisi
  • Hauko tayari kuchapisha makala yako pekee? Zingattia kuchangia kwenye maudhui yaliopo kwenye vyanzo vya jumuiya kama EthHub, ama pendekeza maudhui mapya kwa ajili ya ethereum.org!

Toa msaada wa kuandika muhtasari kwenye mikutano ya jumuiya

Tafsiri maudhui ya Etjereum kwenda kwenye lugha mama, ama lugha uliozaliwa ukizungumza

  • ethereum.org husimamia programu ya ufasiri inayo fasiri tovuti, na vyanzo vingine, kwenda kwenye lugha zingine tofauti
  • Jifunze jinsi ya kuchangiahapa

Endesha nodi

Jiunge na maelefu ya waendesha nodi kwa ugatuzi mkubwa zaidi wa Ethereum.

Weka hisa za ETH

Kwa kusimamisha hisa zako za ETH unaweza kupata zawadi huku ukisaidia kulinda mtandao wa Ethereum.

Unga mkono miradi

Ikolojia ya Ethereum iko njiani katika kufadhili bidhaa za umma na miradi inayoleta tofauti katika Ethereum. Kwa mchango mdigo tu unaweza kuunga mkono na kuruhsu kazi muhimu kutekelezwa.

Wataalamu wa Kifedha & Akaunti ๐Ÿ“ˆ

  • Ethereum ni mji wa ikolojia ya "feddha zilizogatuliwa" - mtandao wa itifaki na programu zinatoa huduma mbadala za kifedha. Kama wewe ni unataaluma ya uchumi, tazama app za DeFi kwenye DeFi Llama ama DeFiprime
  • Mhasibu? Mali za Ethereum - ETH, tokeni, DeFi, nk - tambulisha masuala mengi ya riwaya. Unaweza kuanza kwa kutazama baadhi ya miradi inayolenga kusaidia watumiaji wa sarafu ya kripto na kupanga vitabu vyao & changamoto za uhasibu, kama Rotki

Wasimamizi wa bidhaa ๐Ÿ–‹

  • Ikolijia ya Ethereum inahitaji talanta zako! Makampuni mengi yanatoa ajira kwa wasimsmizi wa bidhaa. Kama unataka kuanza kwa kuchangia kwenye mradi wa vyanzo huria, wasiliana na Wafugaji wa Paka wa Ethereum ama MetaCartel

Masoko ๐Ÿ“ฃ

  • Kuna nafasi nyingi za masoko na mawasiliano kwenye ikolojia ya Ethereum!

Ajira za Ethereum

Unataka kupata ajira kwenye Ethereum?

Jiunge na DAO

"DAOs" ni mashirika huru yaliogatuliwa. Haya makundi yanainua teknolojia ya Ethereum ili kuwezesha ushirikiano. Kwa mfano, kudhibiti uanachama, upigaji kura wa mapendekezo, ama kusimamia mali zilizokusanywa. Huku DAO bado ziko kwenye majaribio, zinatoa fursa ya kupata makundi unayofanana nayo, utapata washiriki na kukuza mchango wako kwenye jumuiya ya Ethereum. Zaidi juu ya DAOs

Was this article helpful?