Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Change page

Miundo ya data na usimbaji

Ethereum huunda, kuhifadhi na kuhamisha viwango vikubwa vya data. Data hii lazima iumbizwe kwa njia sanifu na zinazotumia kumbukumbu vizuri ili kuruhusu mtu yeyote kuendesha nodi kwenye maunzi ya kawaida ya kiwango cha mtumiaji. Ili kufanikisha hili, miundo kadhaa maalum ya data inatumika kwenye staki ya Ethereum.

Masharti

Unapaswa kuelewa misingi ya Ethereum na programu ya mteja. Uelewa wa tabaka la mtandao na waraka mweupe wa Ethereum unapendekezwa.

Miundo ya data

Trie za Patricia merkle

Trie za Patricia Merkle ni miundo inayosimba jozi za ufunguo-thamani kwenye trie thabiti na iliyothibitishwa kwa njia ya kificho. Hizi hutumika sana katika tabaka la utekelezaji la Ethereum.

Zaidi kuhusu Trie za Patricia Merkle

Recursive Length Prefix

Recursive Length Prefix (RLP) ni mbinu ya usanjari inayotumika sana katika tabaka la utekelezaji la Ethereum.

Zaidi kuhusu RLP

Simple Serialize

Simple Serialize (SSZ) ni umbizo kuu la usanjari kwenye tabaka la mwafaka la Ethereum kwa sababu ya utangamano wake na merklelization.

Zaidi kuhusu SSZ