Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Change page

Kiwango cha Tokeni cha ERC-777

Onyo

ERC-777 ni ngumu kutekeleza ipasavyo, kutokana na uwezekano wake wa kushambuliwa kwa njia tofauti (inafunguka katika kichupo kipya). Inapendekezwa kutumia ERC-20 badala yake. Ukurasa huu unasalia kama kumbukumbu ya kihistoria.

Utangulizi?

ERC-777 ni kiwango cha tokheni mbadala kinachoboresha kiwango kilichopo cha ERC-20.

Mahitaji ya Awali

Ili kuelewa vyema ukurasa huu, tunapendekeza usome kwanza kuhusu ERC-20.

Je, ERC-777 inapendekeza maboresho gani dhidi ya ERC-20?

ERC-777 inatoa maboresho yafuatayo dhidi ya ERC-20.

Ndoano (Hooks)

Ndoano (Hooks) ni kipengele cha utendaji kilichofafanuliwa katika msimbo wa mkataba mahiri. Ndoano huitwa wakati tokeni zinatumwa au kupokelewa kupitia mkataba. Hii inaruhusu mkataba mahiri kujibu tokeni zinazoingia au kutoka.

Ndoano hizi husajiliwa na kugunduliwa kwa kutumia kiwango cha ERC-1820 (inafunguka katika kichupo kipya).

Kwa nini ndoano ni nzuri?

  1. Ndoano zinaruhusu kutuma tokeni kwenye mkataba na kuuarifu mkataba katika muamala mmoja, tofauti na ERC-20 (inafunguka katika kichupo kipya), ambayo inahitaji wito mara mbili (approve/transferFrom) ili kufanikisha hili.
  2. Mikataba ambayo haijasajili ndoano haiendani na ERC-777. Mkataba unaotuma utakatisha muamala wakati mkataba unaopokea haujasajili ndoano. Hii inazuia uhamishaji wa bahati mbaya kwenda kwenye mikataba mahiri isiyo ya ERC-777.
  3. Ndoano zinaweza kukataa miamala.

Desimali

Kiwango hiki pia kinatatua mkanganyiko kuhusu decimals uliosababishwa katika ERC-20. Ufafanuzi huu unaboresha uzoefu wa msanidi programu.

Utangamano wa kurudi nyuma na ERC-20

Mikataba ya ERC-777 inaweza kuingiliana kana kwamba ni mikataba ya ERC-20.

Usomaji Zaidi

EIP-777: Kiwango cha Tokeni (inafunguka katika kichupo kipya)