Kuongeza zana za wasanidi programu
Tunataka kuhakikisha tunaorodhesha rasilimali bora zaidi za wasanidi programu iwezekanavyo ili watu waweze kujenga kwa kujiamini na kupata usaidizi wanaohitaji.
Kama kuna zana muhimu ya msanidi programu ambayo tumeikosa, jisikie huru kuipendekeza mahali panapofaa.
Kwa sasa tunaorodhesha zana za wasanidi programu katika tovuti yetu ya wasanidi programu.
Jisikie huru kupendekeza nyongeza mpya kwenye kurasa zinazofaa.
Jinsi tunavyoamua
Mapendekezo ya zana za wasanidi programu yatatathminiwa kwa vigezo vifuatavyo:
Je, imetofautishwa kwa njia ya maana kutoka kwa zana zilizokwisha orodheshwa?
- Aina au kategoria mpya za zana
- Vipengele vipya vikilinganishwa na zana zilizopo zinazofanana
- Inalenga matumizi maalum ambayo hayajashughulikiwa na zana zilizopo zinazofanana
Je, zana ina nyaraka nzuri?
- Je, nyaraka zipo?
- Je, inatosha kutumia zana hiyo?
- Je, imesasishwa hivi karibuni?
Je, zana inatumika sana?
- Tutazingatia vipimo kama vile nyota za GitHub, takwimu za upakuaji, na iwapo inatumiwa na kampuni au miradi inayojulikana
Je, zana ina ubora wa kutosha?
- Je, kuna hitilafu zinazojirudia?
- Je, zana ni ya kuaminika?
- Je, zana inatunzwa kikamilifu?
Je, zana ni ya chanzo wazi?
Miradi mingi katika mfumo wa Ethereum ni ya chanzo wazi. Tuna uwezekano mkubwa wa kuorodhesha miradi ya chanzo wazi inayoruhusu wasanidi programu wa jumuiya kukagua msimbo na kuchangia humo.
Kuagiza Bidhaa
Isipokuwa bidhaa zimepangwa kwa utaratibu maalum, kama vile kialfabeti, bidhaa zitaonyeshwa kuanzia ile iliyoongezwa zamani zaidi hadi ile mpya zaidi kwenye ukurasa. Kwa maneno mengine, bidhaa mpya zaidi huongezwa chini ya orodha.
Ongeza zana yako ya msanidi programu
Kama unataka kuongeza zana ya msanidi programu kwenye ethereum.org na inakidhi vigezo, fungua suala kwenye GitHub.
Unda suala (opens in a new tab)Ukurasa ulihaririwa mwisho: 19 Julai 2024