Utabiri wa masoko hutumia ujuzi na faida za kifedha wa umati kwa matukio yajayo. Wao hutoa taarifa mbalimbali za hali ya juu na walipata umaarufu Marekani 2024. chaguzi.
Jinsi masoko ya utabiri yanavyofanya kazi
Tofauti na mbinu za kitamaduni za utabiri zinazotegemea maoni ya wataalamu, sampuli ndogo za utafiti au data ya kihistoria, soko la utabiri hutumia fursa za kifedha za wakati halisi na hekima ya umma kutoa utabiri kuhusu tukio fulani kama vile uchaguzi, bei za fedha za kidijitali, matokeo ya michezo miongoni mwa mambo mengine
Hii inaruhusu yoyote kutoa ushirikiano kwa matokeo maalumu kwa kufanya ahadi ya kifedha. Kwa kuwezesha kamari kuhusu matukio ya ulimwengu halisi na kurekebisha bei kadri taarifa mpya zinapotokea, maoni yenye msingi madhubuti yanathaminiwa zaidi, na usahihi unaweza kulipwa.
Kiurahisi, sababu wanaokamari wanaweza kufaidi kwa kuwa sahihi, soko la utabiri linaweza kutabiri matokeo kwa usahihi mkubwa. Soko la utabiri lililojengwa juu ya Blockchain linaonyesha mwonekano zaidi mwenye kusisimua, kwa sababu karibu mtu yeyote anaweza kushiriki katika utabiri na kupokea malipo ya sarafu thabiti au fedha za kidijitali.
Kwanini hili ni la muhimu?
Tofauti na utabiri wa kienyeji masoko ya utabiri hutumia teknolojia ya mnyororo wa vizuizi ni:
Ina vivutio
Washiriki huweka fedha halisi, jambo linaloleta ubashiri wa hali ya juu.
Ugatuaji
Kutumia blockchain na mikataba janja huhakikisha malipo ya wazi na ya kiotomatiki.
Odds zinazoamuliwa na soko
Bei huwekwa na wafanyabiashara wanaonunua na kuuza hisa za matokeo, badala ya kupangwa na bookmaker asiyegatuliwa.
Hata kama ni mchunguzi soko, unaweza changanua taarifa ambazo vinginevyo ni ngumu kupata. Fikiria hivi:
- Ubashiri huhusishwa na tukio maalum (k.m., Je, Beam Chain itapelekwa ifikapo 2030?).
- Washiriki wa soko wana nunua na kuuza hisa kulingana na kujiamini matokeo yoyote.
- Bei hubadilika washiriki wengi zaidi huwa na imani zao, kwa maarifa ya papo hapo.
- Yoyote atakae bashiri sahihi hupata mapato kulingana na kiasi alichowekeza
- Waangalizi wa soko wanaweza tumia taarifa wazi kutoa msingi wa utafiti au majadiliano.
Tafuta utabiri wa soko
Kuna masoko kadhaa ya utabiri yenye mfumo wa Ethereum yanayopatikana. Kuna baadhi ya utabiri wa masoko unaojulikana sana leo:
PolymarketA popular forecasting market with real-time trading.
AugurA fully decentralized prediction market protocol used for predicting price trends. Disclaimer: you will need some technical expertise to start using Augur.
Kalshia CFTC-compliant platform using Ethereum for USDC deposits. (USA only)
Kuwa makini na hatari
Bashiri kile kilicho ndani ya uwezo wako na uwe makini na uraibu mbaya.
Vikwazo na madhara
Masoko ya utabiri kwenye mnyororo wa vizuizi hupata vikwazo athiri haki, kisheria, na usahihi.
⚠️ Udanganyifu wa Soko – Wachezaji matajiri wanaweza kubadilisha matokeo kwa kufanya biashara bandia.
💧Matatizo ya kifedha – watumiaji kidogo (uwezo mdogo wa kugharamia (opens in a new tab)) yanaweza kupunguza kuaminika kwa soko.
🏛Kukosa uwazi wa Kisheria –Mamlaka za Serikali kuweka vikwazo kwenye baadhi ya majukwaa.
Ili kupunguza matatizo haya, watengenezaji wa Ethereum wanafanya majaribio kwa suluhisho kama (utawala kwa masharti ya masoko ya utabiri) na uthibitishaji wa utambulisho usio na makao makuu.
Kufanya majaribio na utabiri wa masoko
Utabiri masoko umeleta mageuzi wa maamuzi kwenye wakati wa enzi ya kisasa. Kwa kutumia uwezo wa Ethereum, wao hutoa njia za haki, wazi, na zenye malipo ya kutabiri mustakabali.
Kuna njia nyingi za kutumia zana za utabiri nje ya kupata faida ya kifedha. Kwa mfano, katika DevCon Improvement Proposal (DIP) ilipendekezwa kwamba waandaaji wa DevCon watumie masoko ya utabiri (prediction markets) ili kutarajia idadi ya mahudhurio ya matukio yao ya baadaye.
Hii ingesaidia waandaaji kubaini ni eneo gani lingesababisha tukio lenye mahudhurio makubwa zaidi, ikilinganishwa na eneo gani lingekuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufikiwa kimataifa. Aida za haya humaanisha kwamba waandaaji wa DevCon wanaweza kuharakisha muda unaohitajika kuchuja sera nyingi za visa, upatikanaji wa uwanja wa ndege, na gharama ya maisha katika eneo hilo, huku wakikusanya data kuhusu maeneo ambayo walio na uwezekano wa kuhudhuria wangependa kwenda.
Masomo zaidi
Kutoka masoko ya ubashiri hadi info finance (opens in a new tab) - Vitalik Buterin
Ustawishaji wa Soko la Ubashiri Lililogatuliwa kwenye Ethereum (opens in a new tab)
Karatasi Nyeupe ya Mradi wa Augur (opens in a new tab)
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 22 Oktoba 2025
