Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Fedha za Kuzalisha Upya (ReFi)

  • Mfumo wa uchumi mbadala uliojengwa kwa kanuni endelevu
  • Jaribio la kutumia Ethereum kutatua migogoro ya uratibu wa kiwango cha kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi.
  • Zana ya kuongeza kwa kiasi kikubwa rasilimali za manufaa ya kiikolojia kama vile salio za kaboni zilizothibitishwa.

ReFi ni nini?

Fedha za Kuzalisha Upya (ReFi) ni seti ya zana na mawazo yaliyojengwa juu ya , ambayo yanalenga kuunda chumi ambazo zinajizalisha upya, badala ya zile za uchimbaji au unyonyaji. Hatimaye, mifumo ya uchimbaji humaliza rasilimali zilizopo na kuporomoka; bila mifumo ya kuzalisha upya, hukosa ustahimilivu. ReFi inafanya kazi kwa dhana kwamba uundaji wa thamani ya kifedha lazima utenganishwe na uchimbaji usiokuwa endelevu wa rasilimali kutoka kwenye sayari yetu na jamii zetu.

Badala yake, ReFi inalenga kutatua matatizo ya kimazingira, kijumuiya, au kijamii kwa kuunda mizunguko ya kuzalisha upya. Mifumo hii huunda thamani kwa washiriki huku ikinufaisha mifumo ikolojia na jamii kwa wakati mmoja.

Moja ya misingi ya ReFi ni dhana ya uchumi wa kuzalisha upya iliyoanzishwa na John Fullerton wa Capital Institute. Alipendekeza kanuni nane zinazohusiana (opens in a new tab) ambazo ni msingi wa afya ya kimfumo:

Kanuni nane zinazohusiana

Miradi ya ReFi hutimiza kanuni hizi kwa kutumia na programu za ili kuhimiza tabia za kuzalisha upya, k.m., kurejesha mifumo ikolojia iliyoharibika, na kuwezesha ushirikiano mkubwa katika masuala ya kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi na upotevu wa bioanuwai.

ReFi pia inaingiliana na harakati za sayansi iliyogatuliwa (DeSci), ambayo hutumia Ethereum kama jukwaa la kufadhili, kuunda, kukagua, kutambua mchango, kuhifadhi na kusambaza maarifa ya kisayansi. Zana za DeSci zinaweza kuwa muhimu kwa kuendeleza viwango na mbinu zinazoweza kuthibitishwa za kutekeleza na kufuatilia shughuli za kuzalisha upya kama vile kupanda miti, kuondoa plastiki baharini, au kurejesha mfumo ikolojia ulioharibika.

Uwekaji tokeni wa salio za kaboni

Soko la hiari la kaboni (VCM) (opens in a new tab) ni utaratibu wa kufadhili miradi inayotoa athari chanya iliyothibitishwa kwenye utoaji wa kaboni, aidha kwa kupunguza utoaji unaoendelea, au kuondoa gesi joto ambazo tayari zimetolewa angani. Miradi hii hupokea rasilimali inayoitwa "salio za kaboni" baada ya kuthibitishwa, ambazo wanaweza kuziuza kwa watu binafsi na mashirika yanayotaka kusaidia hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Mbali na VCM, pia kuna masoko kadhaa ya kaboni yaliyoagizwa na serikali ('masoko ya utiifu') ambayo yanalenga kuweka bei ya kaboni kupitia sheria au kanuni ndani ya mamlaka maalum (k.m., nchi au kanda), yakidhibiti ugavi wa vibali vitakavyogawiwa. Masoko ya utiifu huwahamasisha wachafuzi ndani ya mamlaka yao kupunguza utoaji, lakini hayawezi kuondoa gesi joto ambazo tayari zimetolewa.

Licha ya maendeleo yake katika miongo ya hivi karibuni, VCM inaendelea kukumbwa na masuala mbalimbali:

  1. Ukwasi uliogawanyika sana
  2. Taratibu za miamala zisizo wazi
  3. Ada za juu
  4. Kasi ndogo sana ya biashara
  5. Ukosefu wa uwezo wa kuongezeka

Kuhamisha VCM kwenda kwenye soko jipya la kaboni la kidijitali (DCM) lenye msingi wa mnyororo wa bloku kunaweza kuwa fursa ya kuboresha teknolojia iliyopo ya kuthibitisha, kufanya miamala na kutumia salio za kaboni. Minyororo ya bloku huruhusu data inayoweza kuthibitishwa hadharani, ufikiaji kwa watumiaji mbalimbali, na ukwasi zaidi.

Miradi ya ReFi hutumia teknolojia ya mnyororo wa bloku kupunguza matatizo mengi ya soko la jadi:

  • Ukwasi umejilimbikizia katika idadi ndogo ya mabwawa ya ukwasi ambayo yanaweza kufanyiwa biashara na yeyote kwa uhuru. Mashirika makubwa pamoja na watumiaji binafsi wanaweza kutumia mabwawa haya bila kutafuta wauzaji/wanunuzi wenyewe, ada za ushiriki, au usajili wa awali.
  • Miamala yote hurekodiwa kwenye minyororo ya bloku ya umma. Njia ambayo kila salio la kaboni hupitia kutokana na shughuli za kibiashara inaweza kufuatiliwa milele mara tu inapopatikana katika DCM.
  • Kasi ya muamala ni karibu ya papo hapo. Kupata kiasi kikubwa cha salio za kaboni kupitia masoko ya zamani kunaweza kuchukua siku au wiki, lakini hili linaweza kufanikiwa kwa sekunde chache katika DCM.
  • Shughuli za kibiashara hufanyika bila wasuluhishi, ambao hutoza ada za juu. Salio za kaboni za kidijitali zinawakilisha upungufu mkubwa wa gharama zikilinganishwa na salio za jadi.
  • DCM inaweza kuongezeka na inaweza kukidhi mahitaji ya watu binafsi na mashirika ya kimataifa kwa pamoja.

Vipengele muhimu vya DCM

Vipengele vinne vikuu vinaunda mandhari ya sasa ya DCM:

  1. Sajili kama vile Verra (opens in a new tab) na Gold Standard (opens in a new tab) huhakikisha kuwa miradi inayounda salio za kaboni ni ya kuaminika. Pia huendesha hifadhidata ambamo salio za kaboni za kidijitali hutoka na zinaweza kuhamishwa au kutumika (kustaafishwa).

Kuna wimbi jipya la miradi ya kibunifu inayojengwa kwenye minyororo ya bloku ambayo inajaribu kutoa changamoto kwa makampuni yaliyokuwepo katika sekta hii.

  1. Madaraja ya kaboni, a.k.a. viweka tokeni, hutoa teknolojia ya kuwakilisha au kuhamisha salio za kaboni kutoka kwa sajili za jadi hadi kwenye DCM. Mifano mashuhuri ni pamoja na Toucan Protocol (opens in a new tab), C3 (opens in a new tab), na Moss.Earth (opens in a new tab).
  2. Huduma zilizounganishwa hutoa salio za kuepuka na/au kuondoa kaboni kwa watumiaji wa mwisho ili waweze kudai manufaa ya kimazingira ya salio na kushiriki na ulimwengu msaada wao kwa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Baadhi kama Klima Infinity (opens in a new tab) na Senken (opens in a new tab) hutoa miradi mbalimbali iliyotengenezwa na wahusika wengine na kutolewa chini ya viwango vilivyoimarishwa kama Verra; wengine kama Nori (opens in a new tab) hutoa tu miradi maalum iliyotengenezwa chini ya kiwango chao cha salio la kaboni, ambacho wanakitoa na ambacho wana soko lao maalum.

  1. Misingi na miundombinu ya msingi inayowezesha kuongezeka kwa athari na ufanisi wa mnyororo mzima wa ugavi wa soko la kaboni. KlimaDAO (opens in a new tab) hutoa ukwasi kama manufaa ya umma (kuruhusu yeyote kununua au kuuza salio za kaboni kwa bei ya wazi), huhimiza ongezeko la uwezo wa masoko ya kaboni na ustaafishaji kwa zawadi, na hutoa zana zinazofaa kwa mtumiaji na zinazoweza kushirikiana ili kupata data kuhusu, pamoja na kupata na kustaafisha, aina mbalimbali za salio za kaboni zilizowekewa tokeni.

ReFi zaidi ya masoko ya kaboni

Ingawa kwa sasa kuna msisitizo mkubwa katika masoko ya kaboni kwa ujumla na hasa katika kuhamisha VCM kwenda DCM ndani ya eneo hili, neno "ReFi" halihusu kaboni pekee. Rasilimali zingine za kimazingira zaidi ya salio za kaboni zinaweza kuendelezwa na kuwekewa tokeni, jambo ambalo litamaanisha athari zingine hasi za nje pia zinaweza kuwekewa bei ndani ya safu za msingi za mifumo ya kiuchumi ya siku zijazo. Zaidi ya hayo, kipengele cha kuzalisha upya cha mfumo huu wa kiuchumi kinaweza kutumika katika maeneo mengine, kama vile ufadhili wa bidhaa za umma kupitia majukwaa ya ufadhili wa kipeo cha pili kama Gitcoin (opens in a new tab). Mashirika yaliyojengwa juu ya wazo la ushiriki wazi na usambazaji sawa wa rasilimali humwezesha kila mtu kuelekeza pesa kwenye miradi ya programu huria, pamoja na miradi ya kielimu, kimazingira, na inayoendeshwa na jamii.

Kwa kuhamisha mwelekeo wa mtaji kutoka kwenye vitendo vya uchimbaji kuelekea kwenye mtiririko wa kuzalisha upya, miradi na makampuni yanayotoa manufaa ya kijamii, kimazingira, au kijumuiya—na ambayo yanaweza kushindwa kupata ufadhili katika fedha za jadi—yanaweza kuanza na kuzalisha athari chanya za nje kwa jamii kwa haraka na urahisi zaidi. Kuhamia kwenye mtindo huu wa ufadhili pia hufungua mlango kwa mifumo ya kiuchumi iliyo jumuishi zaidi, ambapo watu wa demografia zote wanaweza kuwa washiriki hai badala ya kuwa watazamaji tu. ReFi inatoa maono ya Ethereum kama utaratibu wa kuratibu hatua juu ya changamoto za kuwepo zinazokabili spishi zetu na viumbe vyote kwenye sayari yetu—kama safu ya msingi ya dhana mpya ya kiuchumi, ikiwezesha mustakabali jumuishi na endelevu zaidi kwa karne zijazo.

Masomo ya ziada kuhusu ReFi

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 22 Oktoba 2025

Je! ukurasa huu umekusaidia?