Kuna toleo jipya la ukurasa huu ila liko kwenye Kiingereza tu hivi sasa. Tusaidie kutafsiri toleo jipya zaidi.
Ukurasa huu hautafsiriwi. Tumeuacha ukurasa huu kwa Kiingereza kwa sasa.
Kuleta Ethereum katika mkondo mkuu na kuwatumikia wanadamu wote, tunapaswa kufanya Ethereum kuwa hatari zaidi, salama na endelevu.
Ethereum inahitaji kuwa na uwezo wa kufanya miamala 1000 kwa sekundu, ili programu ifanye kazi haraka na ya bei nafuu kwa watumiaji wa mtandao.
Ethereum inahitaji kua salama zaidi. Wakati upitishwaji wa Ethereum unakua, itifaki inahitaji kua salama zadi dhidi ya mashambukizi ya aina yoyote.
Ethereum inahitaji kua nzuri zaidi kwa mazingira. Teknolojia hii leo hii inahitaji nguvu nyingi sana ya kompyuta na umeme.
Tutawezaje kuifanya Ethereum itanuke zaidi, salama, na endelevu? Vyote hivi huku tukitunza misisingi mikuu ya pesa zinazojitegemea.
Eth2 ni mkusanyiko wa masasisho ambayo yanaboresha uimara, usalama na uendelevu wa Ethereum. Ingawa kila moja inafanyiwa kazi sambamba, ina vitegemezi fulani ambavyo huamua ni lini vitaanza kazi.
Mnyororo Kioleza ulileta usimamishaji wa hisa katika Ethereum, ikaweka msingi kwa ajili ya visasisho vijavyo, na hatimaye utaratibu mfumo mpya.
Mtandao Mkuu wa Ethereum utahiatji "muungano" huu na Mnyororo Kioleza wakati fulani. Hii itawezesha uwekaji wa hisa kwenye mtandao mzima na ishara ya mwisho wa uchimbaji utumiao nguvu/umeme mkubwa.
Minyororo ya vigae itatanua ujazo wa Ethereum kuchakata miamala na kutunza data. Vigae venyewe vitapata vipengele kwa muda, vikitolewa kwa awamu mbalimbali.
Neno 'Eth2' linatolewa kwenye mfumo kwa ajili ya maadalizi ya muungano. Zaidi juu ya muungano.
Baada ya kuunga 'Eth1' na 'Eth2' kwenye cheni moja, hapatakua na mitandao miwili ya Ethereum inayojitegemea; patakuwa na Ethereum tu.
Ili kuondoa sintofahamu, jamii imesasisha haya maneno:
Visasisho vya maneno haya ni kwa ajili ya majina peke yake; hii haibadili malengo ya Ethereum au njia yake.
Jifunze zaidi juu ya jina jipya la 'Eth2'(opens in a new tab)
Suala moja muhimu juu ya chapa ya Eth2 ni kwamba inaunda mifano iliyovunjika akilini kwa watumiaji wapya wa Ethereum. Bila kutilia maanani wanafikiri kwamba Eth1 inatangulia kisha Eth2 inafuata. Ama Eth1 inaondoka pale Eth2 itakaingia. Mawazo haya sio sahihi. Kwa kuondoa msamiati Eth2, tutawaokoa watumiaji wanaokuja kutoka kwenye mfano huu unaochanganya akili.
Wakati ramani ya Ethereum inabalika, Ethereum 2.0 limekuwa neno lisilowakilisha maana sahihi ya ramani ya Ethereum. Kwa kuwa makini juu ya uchaguzi wa majina yanayotumika kufikisha maudhui ya Ethereum imeruhusu uelewa mpana zaidi kwa watazamaji wengi zaidi.
Kwa bahati mbaya walaghai wamajaribu kutumia jina lisilo sahihi kulaghai watumiajo kwa kuwaambia wabadili tokeni zao za ETH zao kwenda ETH2 ama lazima wahame toka kwenye mfumo wa ETH kabla Eth2 haijasasishwa. Tunatumaini visasisho vya majina yatasaidia kuongeza uelewa na kuondoa walaghai na kusaidia Ikolojia kuwa salama zaidi.
Waendeshaji wengine wa uwekaji wa hisa wameiwakilisha ETH iliowekwa kwenye Mnyororo Kioleza kama 'ETH2'. Hii huleta mkanganyiko, kaa ukijua watumiaji wa huduma hii hawapokei tokeni ya 'ETH2'. Hakuna tokeni ya 'ETH2' iliyoundwa mpaka sasa; inawakilisha tu sehemu yao katika hisa mahususi ya watoa huduma.
Ufunguo kwenda kwenye usasishaji wa Etheereum ni uanzilishi wa kusimama kwa hisa. Kama unataka kutumia ETH yako ili kuusaidia ulinzi wa mtandao wa Ethereum, hakikisha umefuata hatua zifuatazo.
Ili usimamishe hisa juu ya Ethereum utahitaji kutumia pedi ya uzinduzi - hii itakutembeza katika mchakato.
Tembelea pedi ya uzinduzi wa hisa simamishwa(opens in a new tab)Kabla ya kuweka ETH yako, hakikisha una anwani sahihi. Lazima uwe umepitia pedi ya uzinduzi kabla ya kufanya hivyo.
Thibitisha anwani ya mkataba wa amanaMnyororo Kioleza utaleta usimamishaji wa hisa kwenye Ethereum. Hii inamaana kama una ETH, unaweza kufanya wema kwa umma kwa kulinda mtandao na kupata ETH zaidi wakati wa mchakato huo.
Pata habari mpya kutoka kwa watafiti na wasanidi programu wanaoshughulikia uboreshwaji wa Ethereum.
Watafiti wa Ethereum na wapenzi wake wanakutana hapa kujadili jitihada za utafutaji, ikijumuisha kila kinachohusiana na maboresho ya Ethereum.
Nenda kwa ethresear.ch(opens in a new tab)