Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Tokeni zisizoweza kubadilishwa(NFTs)

  • Njia ya kuwakilisha kitu chochote cha kipekee kilicho na msingi wa Ethereum.
  • NFT zinawapatia waundaji wa maudhui nguvu zaidi kuliko zamani.
  • Inaendeshwa na mikataba erevu kwenye mnyororo wa bloku wa Ethereum.

Nini ni NFTs?

Tokeni zisizoweza kubadilishwa(NFTs) ni tokeni ambazo kila moja ni ya kipekee. Kila NTF ina sifa tofauti (haziwezi kubadilishwa) na ni chache. Hii ni tofauti kutokana na tokeni kama au Ethereum nyinginezo ukizingatia tokeni kama USDC ambapo kila tokeni ni sawa na ina vipengele sawa('ya kujirudia'). Hutojali ni noti gani ya dola (au ETH) unayo kwenye pochi lako, kwa sababu zote zinafanana na zina thamani sawa. Hata hivyo, unajali NFT unayomiliki, kwa sababu zote huwa na sifa zao za binafsi na unaweza kuzitofautisha kutoka kwa nyingine ('haziwezi kuigwa').

Upekee wa kila NFT ni kuwezesha ishara ya vitu kama sanaa, vitu vinavyokusanywa ama mali isiyohamishika, ambapo kila NFT huwakilisha ulimwengu halisi ama bidhaa ya kidijitali. Umiliki wa mali uko wazi kuhakikishwa na umma kwenye cha Ethereum.

Mtandao wa mali

Tokeni zisizoweza kuigwa na Ethereum husuluhisha shida zinazokuwepo kwenye mtandao leo. Kwa kuwa kila kitu kinakuwa cha kidijitali, kuna haja ya kuiga sifa za vitu halisi kama uhaba, upekee na ushahidi wa umiliki kwa njia ambayo umiliki audhibitiwi na shirika la kati. Kwa mfano, ukiwa na NFTs unaweza kumiliki faili la muziki wa mp3 kupitia programu mahususi kwa ajili ya Ethereum na isiyo shikana na kampuni ya aina yoyote ya muziki kama Spotify au Apple music. Unaweza kumiliki kishiriki-jina cha mtandao wa kijamii ambacho unaweza kuuza au kubadilisha, lakini aiwezi chukuliwa moja kwa moja kutoka kwako na mtoa jukwa.

Hivi ndivyo mtandao wa NFT unafanya kazi ukilinganisha na mtandao ambao wengi wengi tunatumia leo...

Ulinganisho

Mtandao wa NFTIntaneti ya leo
Unamiliki mali zako! Wewe pekee ndio unaweza kuuza au kuzibadilisha.Ukikodisha mali zako kwa baadhi ya mashirika na inaweza ikachukuliwa mja kwa moja kutoka kwako.
NFT zina sifa za kipekee za kidijitlai, hakuna NFT mbili zitakazofanana.Mara nyingi nakala haiwezi kutofautishwa na ya asili.
Umiliki wa NFT unawekwa kwenye blockchain ili kila mtu kuwezathibitisha hadharani.Upatikanaji wa rekodi za umiliki wa vitu vya kidijitali unadhibitiwa na taasisi - unapaswa kuamini wnachosema.".
NFT ni Ethereum. Hii inamaana kuwa zinaweza kutumika kwenye mikataba erevu mingine na programu kwenye Ethereum!Kampuni zenye bidhaa za kidigitali kawaida huhitaji kuwa na "ukingo imara wa ulinzi wa miundo mbinu".
Waunda maudhui wanaweza kuuza kazi zao sehemu yoyote na kufikia soko la ulimwengu mzima.Waundaji wanategemea miundombinu na usambazaji wa majukwaa wanayotumia. Mara nyingi hili hufuata sheria na masharti na vizuizi vya kijiografia.
Watengenezaji wa NFT wanaweza kuhifadhi haki za kazi na mirabaha ya programu zao moja kwa moja kwenye mkataba wa tokeni zisizojirudia.Majukwaa kama ya huduma za kusikiliza muziki, yanapata faida nyingi kutoka kwenye mauzo.

NFT zinatumika kufanya nini?

NFT hutumika kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na:

  • kuthibitisha kwamba ulihudhuria tukio
  • kuthibitisha kwamba ulimaliza kozi
  • umiliki wa vitu vya michezo
  • sanaa ya kidigitali
  • kugeuza mali za kidunia kuwa tokeni
  • kuthibitisha utambulisho wako kwenye mtandao
  • kuzuia ufikiaji wa maudhui
  • ukataji tiketi
  • majina ya kikoa kwenye intaneti iliyogatuliwa
  • dhamana katika

Labda wewe ni msanii amabaye angependa kushiriki kazi yake kupitia NFT bila wewe kupoteza udhibiti ama kuwapa waamuzi faida zako. Wewe unaweza kutengeneza mkataba mpya na kuweka bayana hesabu ya NFT, vipengele vyao na kiungo chao kwa kazi mahususi ya sanaa. Kama msanii, unaweza kuprogramu ndani ya mkataba-erevu mrabaha unaofaa kulipwa (kwa mfano hamisha 5% ya bei ya mauzo kwa mwenye mkataba kila wakati tokeni inapohamishwa). Vile vile unaweza kuthibitisha kwamba wewe ndiwe umetengeneza NFT kwa sababu wewe ndiwe mmiliki wa iliyotuma mkataba huo. Wanunuzi wako wanaweza kuthibitisha kwa urahisi kwamba wao ndio wamiliki wa NFT halisi kutoka kwenye mkusanyiko wako kwa sababu pochi yao ya ya mkoba zao inashirikishwa na tokeni kutoka kwenye mkataba wako. Wanaweza kuitumia katika mfumo wa ikologia ya Ethereum, inayoaminika kwa uhalisi wake.

Chunguza, nunu au tengeneza sanaa ya NFT...
Chunguza sanaa ya NFT

Ama zingatia tiketi ya tukio ya mechi ijayo. Kama mratibu wa matukio anavyoweza kuamua idadi ya tiketi za kuuza, muundaji wa NFT anaweza kuamua idadi ya kuwepo kwa nakala za kazi yake. Wakati mwingine huwa na nakala za ziada, kama vile Tiketi 5000 za Kiingilio cha Jumla. Wakati mwingine nyingine zinachapishwa zinazofanana, ila kila moja ina tofauti ndogo na yenzake, kama vile tiketi yeneye nambari ya kiti. Hizi zinaweza kununuliwa na kuuzwa kutoka kwa mshirika mmoja mpaka kwa mwingine kusipokuwepo na ulipaji wa washikaji tiketi na wanunuzi watakuwa na uhakika wa tiketi halisi kwa kuangalia anwani ya mkataba huo.

Kwenye ethereum.org tokeni zisizojirudia zinatumika kuonyesha kuwa watu wana maana nzuri ya kuchangia kupitia ripositi ya Github (programu tovuti, maandiko au kurekebisha chapisho...), tafsiri maudhui yetu, au uzuria simu za jamii yetu, na pia hata tunayo jina la tovuti yetu la tokeni zisizojirudia. Ukichangia kwenye ethereum.org, unaweza kuchukua tokeni isiyojirudia ya . Mikutano mingine ya sarafu za kidijitali imetumia POAPs kama tiketi. Zaidi juu ya uchangiaji.

POAP za ethereum.org

Tovuti hii pia inatumia jina mbadala la kikoa linaloendeshwa na NFT, ethereum.eth. Anwani yetu ya .org inasimamiwa na mfumo wa majina wa kati/jadi(DNS), wakati ethereum.eth imesajiliwa kwenye huduma za majina ya Ethereum (ENS). Na hii linamilikiwa na kuendeshwa na sisi. Angalia rekodi zetu za ENS(opens in a new tab)

Zaidi juu ya ENS(opens in a new tab)

NFT zinafanyaje kazi?

NFT, kama vitu vyovyote vya kidijitali kwenye kiambajengo cha Ethereum, zinatengenezwa kupitia programu ya kompyuta maalumu ya Ethereum inayoitwa "mkataba erevu" Mikataba hii inafuata sheria fulani, kama viwango vya au , ambayo inaamua mikataba hii nini inaweza kufanya.

Mikataba erevu ya NFT zinaweza kufanya vitu vichache:

  • Unda NFT: Inaweza kuunda NFTs.
  • Weka umiliki: Itaendelea kufuatilia mtu anayemiliki NFT kwa kuunganisha na anwani maalumu ya Ethereum.
  • Ipe kila NFT namba ya utambulisho: NFT ina namba ambayo inaifanya kuwa ya kipeee. Cha ziada, kikawaida kuna kuwa na baadhi ya taarifa (metadata) zinazo ambatanishwa nayo, inaelezea kitu kinachoiwakilisha tokeni isiyojirudia.

Wakati mtu "anatengeneza" au "kuunda" NFT, kimsingi wanaiambia mkataba erevu kuwapa wao umiliki wa NFT husika. Taarifa hii inalindwa kwa usalama na kuhifadiwa na umma kwenye blockchain.

Zaidi, muundaji wa mkataba anaweza ongeza sheria nyingine za ziada. Wanaweza dhibiti kiasi cha NFT kuweza kuundwa au kuamaua kwamba wanaweza pata ada ya mrabaha pale ambapo NFT inabadilisha mmiliki.

Usalama wa NFT

Usalama wa Ethereum unakuja kutokana na . Mfumo huu umebuniwa ili uweze kuondoa vitendo ya kihasidi kiuchumi na basi kuifanya Ethereum sugu kwa uharibifu. Hii ndiyo inayofanya NFT kuwezekana. Mara tu yenye muamala wako wa NFT , inaweza kugharimu mshambulizi mamilioni ya ETH kuibadilisha. Mtu yeyote anayetumia programu ya Ethereum anaweza kujua haraka mambo yasiyofaa ya kuhitilafiana na NFT, na mtu huyu mbaya atatozwa malipo na kuondolewa.

Maswala ya usalama yanayohusiana na NFT sana sana yanahusiana na utapeli wa kutumia barua pepe, hatari za mkataba-erevu au makosa ya mtumiaji (kama vile kuweka wazi funguo za siri) na hivyo kufanya usalam bora wa pochi uwe muhimu sana kwa wamiliki NFT.

Maelezo zaidi kuhusu usalama

Soma zaidi

Rasilimali nyingine

Test your Ethereum knowledge

Je! ukurasa huu umekusaidia?