Msaada wa Ethereum
Msaada rasmi wa Ethereum
Je, unatafuta msaada rasmi wa Ethereum? Cha kwanza unachopaswa kujua ni kua Ethereum imegatuliwa. Hii inamaana hamna mashirika ya kati ama ya kiserikali, chombo, ama mtu anayemiliki Ethereum, na kwasababu hio, hakunana chaneli ya kutoa msaada ilio rasmi.
Ufahamu wa asili ya ugatuzi wa Ethereum ni muhimu kwa kila mmoja maana yeyote anayedai kua mtu anaeweza kutoa msaada kuhusu Ethereum anaweza kukulaghai! Ulinzi thabiti dhidi ya walaghai na kujifunza na kua makini na ulinzi.
Licha ya upungufu wa uungaji mkono, makundi mengi, jumuiya na mirandi ndani ya ikolojia ya Ethereum wanafurahi kuunga mkono, na unaweza kupata taarifa muhimu na vyanzo kwenye ukurasa huu. Bado unamswali? Jiunge na Discord ya ethereum.org(opens in a new tab), na tutajaribu kukusaidia.
Huduma za pochi
Je unapata shida na pochi yako? Pochi nyingi zina timu inayojiyuma inayoweza kukusaidia:
Hii sio orodha kamili. Unahitaji msaada kupata huduma juu ya pochi maalum? Jiunge na discord ya etehreum.org(opens in a new tab) na tutajaribu kusaidia.
Unatafuta pochi ya Ethereum? Chunguza orodha yetu yote ya Ethereum.
Jenga dapps
Ujenzi unaweza kua mgumu. Haya ni majukwaa yaliojikita kwenye uendelezaji ukiwa na wasanidi programu waliobobea wenye furaha kukuasaidia.
- Discord ya CryptoDevs(opens in a new tab)
- StackExchange ya Ethereum(opens in a new tab)
- StackOverflow(opens in a new tab)
- Chuo cha Web3(opens in a new tab)
Unaweza kupata nyarak na miongozo ya usanidi kwenye kipengele cha vyanzo vya msanidi programu wa Ethereum.
Zana
Je swali lako linahusiana na chimbo fulani maalum, mradi au maktaba? Miradi mingi ina seva za soga au vikako vilivyojikita kukusaidia wewe.
Hii ni baadhi ya mifano maalum:
- Uimara(opens in a new tab)
- ethers.js(opens in a new tab)
- web3.js(opens in a new tab)
- Hardhat(opens in a new tab)
- Alchemy(opens in a new tab)
Endesha nodi
Kama unaendesha nodi am mthibitishaji, hizi ni baadhi ya jamii zinazotoa msaada ili upate kuanza katika Ethereum.
Timu zilizo nyingi za usanidi programu za Ethereum zinajitolea kusaidia mikutano ya hadhara amabayo unaweza kupata waunga mkono na kuuliza maswaloi muhimu.
Programu za utelekezji
- Geth(opens in a new tab)
- Nethermind(opens in a new tab)
- Besu(opens in a new tab)
- Erigon(opens in a new tab)
Programu ya makubaliano
- Prysm(opens in a new tab)
- Nimbus(opens in a new tab)
- Taa ya taa(opens in a new tab)
- Teku(opens in a new tab)
- Mwangaza(opens in a new tab)
Unaweza kujifunza jinsi ya kuendesha nodi hapa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Nimetuma ETH kwenye pochi isiyo sahihi
Muamala unaofanyika kwenye Ethereum hauwezi kurudishwa ulikotoka. Kwa bahati mbaya, kama umetuma ETH kwenye pochi isiyo sahihi, hamna njia ya kupata fedha hizo. Hakuna shirika la kati, chombo ama mtu mmoja anaemiliki Ethereum, kwa maana kwamba hamna anaeweza kurudisha muamala ulikwishafanyika. Kwahiyo, ni muhimu kukagua mara kadhaa kama anauani ya pochi unayoingiza iko sahihi kabala ya kufanya muamala.
Nawezaje kudai zawadi yangu ya Ethereum?
Zawadi za Ethereum ni mitego/ulaghai unaobuniwa ili kuiba ETH zako. Usishawishike na huduma inayotanganzwa inayoonekana kua ya uwongo - ukiotuma ETH kwenye anwani ya zawadi, hautapokea zawadi, na hautaweza kupata fedha ulizotuma mwanzo.
Muamala wangu umegota
Wakati mwingine miamala hugita kwenye Ethereum kama umetoa kiwango kidogo cha malipo ya muamala kuliko kile kinachohitajika kwenye mtandao. Pochi nyingi hutoa chaguo la kutuma tena muamala huo huo kwa bei ya juu zaidi ili muamala ufanyiwe mchakato. Kwa njia mbadala unaweza kughairi muamala usio kamili kwa kutuma fedha hizo kwenye anwani yako mwenyewe, na kutumia nonce sawa na ya muamala ambao haujakamlika.
Jinsi ya kuzuia/ghairi miamala kwenye Ethereum(opens in a new tab)
Nawezaje kuchimba Ethereum?
Hatushauri kununua maunzi ya kuchimba Ethereum kama bado haujaanza kuchimba. Kwenye ~Q3. Q4 2022, Muungano utatokea, utabadilisha Ethereum kutoka kwenye uthibitisho-wa-kazi kwenda kwenye usthibitisho-wa-hisa. Haya mabadiliko yatafanya uchimbaji wa Ethereum kutowezekana tena.