Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jinsi ya kuvusha tokeni kwenye tabaka la 2 (l2)

Ikiwa kuna msongamano mkubwa kwenye Ethereum, inaweza kuwa ghali. Suluhisho moja la hili ni kuunda "matabaka" mapya: yaani, mitandao tofauti ambayo inafanya kazi kwa njia sawa na Ethereum yenyewe. Haya yanayoitwa matabaka ya 2 (l2) husaidia kupunguza msongamano na gharama kwenye Ethereum kwa kuchakata miamala mingi zaidi kwa ada za chini, na kuhifadhi tu matokeo ya haya kwenye Ethereum mara kwa mara. Kwa hivyo, matabaka haya ya 2 (l2) yanatuwezesha kufanya miamala kwa kasi iliyoongezeka na gharama zilizopunguzwa. Miradi mingi maarufu ya kripto inahamia kwenye matabaka ya 2 (l2) kwa sababu ya faida hizi. Njia rahisi zaidi ya kuhamisha tokeni kutoka Ethereum hadi kwenye tabaka la 2 (l2) ni kutumia daraja.

Sharti:

1. Amua ni mtandao gani wa tabaka la 2 (l2) unaotaka kutumia

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu miradi tofauti na viungo muhimu kwenye ukurasa wetu wa tabaka la 2 (l2).

2. Nenda kwenye daraja lililochaguliwa

Baadhi ya matabaka ya 2 (l2) maarufu ni:

3. Unganisha kwenye daraja ukitumia mkoba wako

Hakikisha mkoba wako umeunganishwa kwenye Mtandao Mkuu wa Ethereum. Ikiwa haujaunganishwa, tovuti itakuuliza kiotomatiki ubadilishe mitandao.

Common interface for bridging tokens

4. Taja kiasi na uhamishe fedha

Kagua kiasi ambacho utapata kama mrejesho kwenye mtandao wa tabaka la 2 (l2) na ada ili kuepuka mshangao usiofurahisha.

Common interface for bridging tokens

5. Thibitisha muamala kwenye mkoba wako

Utalazimika kulipa ada (inayoitwa ) kwa mfumo wa ETH kwa ajili ya kuchakata muamala.

Common interface for bridging tokens

6. Subiri fedha zako zihamishwe

Mchakato huu haupaswi kuchukua zaidi ya dakika 10.

7. Ongeza mtandao wa tabaka la 2 (l2) uliochaguliwa kwenye mkoba wako (si lazima)

Unaweza kutumia chainlist.org (opens in a new tab) kupata maelezo ya RPC ya mtandao. Mara tu mtandao unapoongezwa na muamala kukamilika, unapaswa kuona tokeni kwenye mkoba wako.


Unataka kujifunza zaidi?
Tazama miongozo yetu mingine

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Vipi ikiwa nina fedha kwenye soko la kubadilishia fedha?

Unaweza kutoa fedha kwenda kwenye baadhi ya matabaka ya 2 (l2) moja kwa moja kutoka kwenye soko la kubadilishia fedha. Angalia sehemu ya “Hamia kwenye tabaka la 2 (l2)” ya ukurasa wetu wa Tabaka la 2 (l2) kwa maelezo zaidi.

Je, ninaweza kurudi kwenye Mtandao Mkuu wa Ethereum baada ya kuvusha tokeni zangu kwenda kwenye tabaka la 2 (l2)?

Ndiyo, unaweza kuhamisha fedha zako kurudi kwenye Mtandao Mkuu wakati wowote ukitumia daraja lile lile.

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 15 Aprili 2026