Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jinsi ya kuunda akaunti ya Ethereum

Mtu yeyote anaweza kuunda akaunti ya Ethereum bila malipo. Unahitaji tu kusakinisha programu ya mkoba wa kripto. Mikoba huunda na kudhibiti akaunti yako ya Ethereum. Inaweza kutuma miamala, kuangalia salio lako na kukuunganisha kwenye programu zingine zilizojengwa kwenye Ethereum.

Ukiwa na mkoba unaweza pia kuingia kwenye ubadilishaji wowote wa tokeni, michezo, masoko ya papo hapo. Hakuna haja ya usajili wa mtu binafsi, akaunti moja inashirikiwa kwa programu zote zilizojengwa kwenye Ethereum.

Hatua ya 1: Chagua mkoba

Mkoba ni programu inayokusaidia kudhibiti akaunti yako ya Ethereum. Kuna makumi ya mikoba tofauti ya kuchagua: ya simu, ya kompyuta, au hata viendelezi vya kivinjari.

Orodha ya mikoba

Ikiwa wewe ni mgeni, unaweza kuchagua kichujio cha "Mgeni kwenye kripto" kwenye ukurasa wa "tafuta mkoba" ili kutambua mikoba inayopaswa kujumuisha vipengele vyote muhimu vinavyofaa kwa wanaoanza.

Filter selection on 'find a wallet' page

Pia kuna vichujio vingine vya wasifu ili kukidhi mahitaji yako. Hii ni mifano ya mikoba inayotumiwa sana - unapaswa kufanya utafiti wako mwenyewe kabla ya kuamini programu yoyote.

Hatua ya 2: Pakua na usakinishe programu yako ya mkoba

Mara tu unapoamua kuhusu mkoba maalum, tembelea tovuti yao rasmi au duka la programu, upakue na uusakinishe. Yote inapaswa kuwa bila malipo.

Hatua ya 3: Fungua programu na uunde akaunti yako ya Ethereum

Mara ya kwanza unapofungua mkoba wako mpya unaweza kuulizwa kuchagua kati ya kuunda akaunti mpya au kuleta iliyopo. Bofya kwenye uundaji wa akaunti mpya. Hii ndiyo hatua ambayo programu ya mkoba inazalisha akaunti yako ya Ethereum.

Hatua ya 4: Hifadhi kirai chako cha kurejesha

Baadhi ya programu zitakuomba uhifadhi "kirai cha kurejesha" cha siri (wakati mwingine huitwa "kirai cha mbegu" au "nimoniki"). Kuweka kirai hiki salama ni muhimu sana! Hiki kinatumika kuzalisha akaunti yako ya Ethereum na kinaweza kutumika kuwasilisha miamala.

Mtu yeyote anayejua kirai hicho anaweza kuchukua udhibiti wa fedha zote. Usishiriki hiki na mtu yeyote. Kirai hiki kinapaswa kuwa na maneno 12 hadi 24 yaliyozalishwa kwa nasibu (mpangilio wa maneno ni muhimu).

Umesakinisha mkoba?
Jifunze jinsi ya kuutumia.
Jinsi ya kutumia mkoba

Unavutiwa na miongozo mingine? Angalia: Miongozo yetu ya hatua kwa hatua

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, mkoba wangu na akaunti yangu ya Ethereum ni sawa?

Hapana. Mkoba ni zana ya usimamizi inayokusaidia kudhibiti akaunti. Mkoba mmoja unaweza kufikia akaunti kadhaa, na akaunti moja inaweza kufikiwa na mikoba mingi. Kirai cha kurejesha kinatumika kuunda akaunti na kutoa ruhusa kwa programu ya mkoba kudhibiti rasilimali.

Je, ninaweza kutuma bitcoin kwenye anwani ya Ethereum, au Etha kwenye anwani ya Bitcoin?

Hapana, huwezi. Bitcoin na Etha zipo kwenye mitandao miwili tofauti (yaani, minyororo ya kitalu tofauti), kila moja ikiwa na uwekaji hesabu wake na miundo ya anwani. Kumekuwa na majaribio mbalimbali ya kuvusha kati ya mitandao hiyo miwili tofauti, ambayo inayoendelea zaidi kwa sasa ni Wrapped Bitcoin au WBTC (opens in a new tab). Hili si idhinisho, kwa kuwa WBTC ni suluhisho la uhifadhi (ikimaanisha kundi moja la watu hudhibiti utendaji fulani muhimu) na inatolewa hapa kwa madhumuni ya taarifa pekee.

Ikiwa ninamiliki anwani ya ETH, je, ninamiliki anwani sawa kwenye minyororo mingine ya kitalu?

Unaweza kutumia sawa kwenye minyororo yote ya kitalu inayotumia programu ya msingi sawa na Ethereum (inayojulikana kama 'inayoendana na EVM'). Orodha (opens in a new tab) hii itakuonyesha ni minyororo ipi ya kitalu unayoweza kutumia na anwani sawa. Baadhi ya minyororo ya kitalu, kama Bitcoin, hutekeleza seti tofauti kabisa ya sheria za mtandao na utahitaji anwani tofauti yenye muundo tofauti. Ikiwa una mkoba wa mkataba mahiri unapaswa kuangalia tovuti ya bidhaa yake kwa maelezo zaidi kuhusu ni minyororo ipi ya kitalu inayotumika kwa sababu kwa kawaida hiyo ina upeo mdogo lakini salama zaidi.

Je, kuwa na mkoba wangu mwenyewe ni salama zaidi kuliko kuweka fedha zangu kwenye ubadilishaji?

Kuwa na mkoba wako mwenyewe kunamaanisha unachukua jukumu la usalama wa rasilimali zako. Kwa bahati mbaya kuna mifano mingi ya ubadilishaji uliofeli ambao ulipoteza pesa za wateja wao. Kumiliki mkoba (wenye kirai cha kurejesha) kunaondoa hatari inayohusishwa na kuamini taasisi fulani kushikilia rasilimali zako. Hata hivyo, inabidi uulinde wewe mwenyewe na uepuke ulaghai wa kuhadaa ili kupata maelezo ya kibinafsi, kuidhinisha miamala kimakosa au kufichua kirai cha kurejesha, kuingiliana na tovuti feki na hatari zingine za uhifadhi binafsi. Hatari na faida ni tofauti.

Ikiwa nitapoteza simu/mkoba wangu wa maunzi, je, ninahitaji kutumia programu sawa ya mkoba tena ili kurejesha fedha zilizopotea?

Hapana, unaweza kutumia mkoba tofauti. Mradi una kirai cha mbegu unaweza kukiingiza kwenye mikoba mingi na itarejesha akaunti yako. Kuwa mwangalifu ikiwa utawahi kuhitaji kufanya hivi: ni vyema kuhakikisha kuwa hujaunganishwa kwenye intaneti unapourejesha mkoba wako ili kirai chako cha mbegu kisivuje kimakosa. Mara nyingi haiwezekani kurejesha fedha zilizopotea bila kirai cha kurejesha.

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 3 Aprili 2026