Je, umechoka kutafuta soko la kubadilishia fedha ambalo linaorodhesha tokeni zako zote unazozipenda? Unaweza kubadilisha tokeni nyingi ukitumia .
Badilishano la tokeni linahusisha ubadilishanaji wa rasilimali mbili tofauti zilizopo kwenye mtandao wa Ethereum, kwa mfano kubadilisha ETH kwa DAI (tokeni ya ). Mchakato huu ni wa haraka sana na wa bei nafuu. Utahitaji kuwa na mkoba wa kripto ili kubadilisha tokeni.
Mahitaji ya awali:
- kuwa na ; kama huna, unaweza kufuata mwongozo huu kuhusu jinsi ya kuunda akaunti ya Ethereum
- kuongeza fedha kwenye mkoba wako
1. Unganisha mkoba wako kwenye soko lililogatuliwa (DEX) unalolipendelea
Baadhi ya masoko maarufu ni:
- Uniswap (opens in a new tab)
- Sushiswap (opens in a new tab)
- 1Inch (opens in a new tab)
- Curve (opens in a new tab)
Inavutia? Jifunze zaidi kuhusu nini maana ya fedha zilizogatuliwa (DeFi) na jinsi aina hizi mpya za masoko zinavyofanya kazi.
2. Chagua jozi ya tokeni unazotaka kubadilisha
Kwa mfano, ETH na DAI. Hakikisha una fedha katika mojawapo ya tokeni hizo mbili.

3. Weka kiasi cha tokeni unachotaka kufanyia biashara na ubofye badilisha
Soko litahesabu kiotomatiki ni tokeni ngapi utapata.
4. Thibitisha muamala
Kagua maelezo ya muamala. Angalia kiwango cha ubadilishaji na ada nyingine zozote ili kuzuia mshangao mbaya.
5. Subiri muamala uchakatwe
Unaweza kutazama maendeleo ya muamala kwenye kichunguzi chochote cha mnyororo wa vitalu. Mchakato huu haupaswi kuchukua zaidi ya dakika 10.
Utapokea kiotomatiki tokeni zilizobadilishwa kwenye mkoba wako mara tu muamala utakapochakatwa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, ninaweza kubadilisha ETH kwa BTC kutoka kwenye mkoba wangu?
Hapana, unaweza tu kubadilisha tokeni ambazo ni asili ya mtandao wa Ethereum, kama vile ETH, tokeni za ERC-20 au NFT. Unaweza tu kubadilisha aina za Bitcoin "zilizofungwa" ambazo zipo kwenye Ethereum.
Nini maana ya tofauti ya utekelezaji?
Ni tofauti kati ya kiwango chako cha ubadilishaji ulichotarajia na kiwango halisi.
Ukurasa ulisasishwa mwisho: 6 Juni 2026

