Ether ni nini (ETH)?
Sarafu kwa ajili ya ulimwengu wa dijitali wa kesho
Sarafu ya Ether (ETH) ni ya kidijitali, fedha ya kimataifa.
Ni sarafu ya programu za Ethereum.
Bei ya sasa ya ETH(USD)
ETH ni sarafu ya kripto. Ni hela adimu ya kidijitali ambayo unaweza kuitumia mtandaoni -- sawa sawa na Bitcoin. Kama wewe ni mpya kwenye kripto, maelezo haya yatakuonyesha tofauti kati ya ETH na sarfu zetu za jadi au tulizozoea kuongozwa na serikali.
Ni ya kwako kweli
ETH inafanya unakua benki yako wewe mwenyewe. Unaweza kudhibiti fedha zako na pochi yako kama kithibitisho cha umiliki hamna hitaji la mpatanishi wa kati.
Inalindwa na kriptografia
Hela ya mtandao ni mpya katika jamii ila iko salama na inalindwa na iliohakikishwa. Hii inalinda mikoba yako, ETH yako, na miamala yako.
Malipo ya rika kwa rika
Unaweza kutuma ETh bila kuhitaji huduma ya upatanishi kama benki. Ni kama kumkabidhi mtu pesa uso kwa uso, lakini unaweza kufanya hivyo na mtu yeyote, wahali popote, wakati wowote.
Hakuna udhibiti wa serikali
ETH imehatuliwa na ni ya ulimwengu. Hakuna kampuni au benki itakayoamua kuchapisha ETH zaidi, au kubalisha masharti ya matumizi.
Iko wazi kwa yeyote
Unahitaji kuwa na mtandao na pochi ili kupokea ETH. Hauhitaji kwenda benkoi ili kupokea malipo.
Inapatikana katika viwango vinavyonyumbulika
ETH inagawanyika mapaka desimali 18 kwahiyo huitaji kununua ETH 1 nzima. Unaweza kununua sehemu kila baada ya mda -unaweza kununua kidogo mpaka 0.000000000000000001 ETH kama unataka.
Ni nini cha pekee kwenye ETH?
Kuna sarafu nyingi za kripto na ishara nyingine nyingi zilizo juu ya Ethereum, lakini kuna baadhi ya vitu ETH pekee ndio inaweza kuyafanya.
ETH ni mafuta na inalinda Ethereum
ETH ni damu ya Ethereum. Unapotuma ETH ama kutumia programu za Ethereum, utalipa tozo katika ETH ili utumie mtandao wa Ethereum. Hizi tozo ni motisha kwa mzalishaji wa vitalu kufanya mchakato na kuthibitisha unachojaribu kufanya.
Wathibitishaji ni kama watunza rekodi wa Ethereum-wanakagua na kuhakikisha kwamba hakuna anayedanganya. Wanachaguliwa kwa nasibu kuchagua kundi la miamala. Wathibitishaji wanaofanya kazi hii wanazawadiwa kiwango kidogo cha ETH mpya.
Kazi ambayo wathibitishaji wanafanya, na fedha , huongeza usalama na kufanya Ethereum kua huru na kuepuka mashirika ya kati. ETH inaipa nguvu Ethereum.
Unaposimamisha hisa zako za ETH, unasaidia kulinda Ethereum na unapata riba. Kwenye mfumo huu, utete wa kupoteza ETH hufukuza wavamizi. Zaidi juu ya kusimamisha hisa
Ethereum ni nini?
Kama ungependa kujifunza zaidi juu ya Ethereum, teknolojia ilioko nyuma ya ETH, anagalia utangulizi wetu.
ETH inaimarisha mifumo ya fedha ya Ethereum
Haujridhika na malipo, Jamii ya wana-Etehreum inajenga mfumo mzima wa fedha wa na utakaopatikana kwa kila mtu.
Unaweza kutumia ETH kama dhamana kuzalisha ishara za kripto tofauti kabisa juu ya Ethereum. Pamoja na kwamba unaweza kuazima, kukopesha na kupata riba juu ya ETH na ishara zinazobebwa na ETH.
Zaidi juu ya DeFi
DeFi ni mifumo ya kifedha iliogatuliwaa iliojengwa juu ya Ethereum. Muhtasari huu unaelezea unachoweza kufanya.
Matumizi ya ETH yanakua kila siku
Kwasababu Ethereum inaweza kusanidiwa, wasanisi programu wanaweza kuiunda ETH katika njia zisizohesabika.
Ukirudi mwaka 2015, ulichokua unaweza kufanya ni kutuma ETH kutoka akaunti moja kwenda nyingine. Hivi hapa ni baadhi ya vitu unavyoweza kufanya leo hii.
- Mtiririko wa ETH(opens in a new tab) – lipa mtu au pokea fedha katika muda halisi.
- Badilisha ishara – unaweza kufanya biashara ya ETH na ishara zingine ikiwemo Bitcoin.
- Jipatie riba(opens in a new tab) – juu ya ETH na ishara zingine zilizo na misingi ya Ethereum.
- Pata sarfu-imara – fika katika ulimwengu wa sarafu za kripto kwa uthabiti, thamani iliopungua hali ya utete.
Kwanini ETH ina thamani?
ETH inathamani katika njia tofauti kwa watu tofauti.
Kwa watumiaji wa Ethereum, ETH ina thamani kwasababu inakuruhusu kulipia ada za muamala.
Wengine wanaiona kama ghala la kidijatili kwasababu ya uundaji wa ETH mpya unashuka chini taratibu mda unavyokwenda.
Hivi karibuni, ETH imekua na thamani kwa watumiaji wa programu za kifedha kwenye Ethereum. Hii ni kwasababu unaweza kutumia ETH kama dhamana kwa ajili ya mikopo ya kripto, au kama mfumo wa ulipaji.
Bila shaka wengi wanaiona kama sehemu ya uwekezaji, sawa na Bitcoin au sarafu nyingine za kripto.
ETH sio kripto pekee kwenye Ethereum
Mtu yeyote anaweza kuunda aina mpya za mali na kuziuza kwa Ethereum. Hizi zinajulikana kama 'ishara'. Watu wamegeuza sarafu za jadi kwenda kwenye ishara, mali isiohamishika, sanaa, na hata wao wenyewe!
Ethereum ni mji wa maelfu ya ishara - nyingine zinamanufaa na thamani kubwa kuliko zingine. Daima wasanidi programu huunda ishara mpya ambazo zinafungua mategemeo mapya na kufungua masoko mapya.
Zaidi juu ya ishara na kazi zake
Aina za ishara maarufu
Sarafu-imara
Ishara zinazofanana na sarfu za jadi kama vile dola. Hii inatatua hali ya tete ya sarafu za kripto.
Ishara za Utawala
Ishara zinazowakilisha nguvu ya kupiga kura kwenye mashirika yaliogatuliwa.
Sarafu zisizo na hadhi
Kwasababu kutengeneza ishara mpya ni rahisi, mtu yeyote anaweza kufanya - hata watu wenye nia mbaya. Mara zote fanya utafiti wako kabla hujazitumia!
Ishara zinazokusanyika
Ishara zinazowakilisha mchezo unaokusanyika, kipande na sanaa, au mali nyingine ya kipekee. Kwa kawaida hujulikana kama ishara zisizo-kuvu ama kwa kifupisho cha lugha ya kiingereza (NFTs).