Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 19 Julai 2024

Kuongeza exchange za Ethereum

Yeyote anaweza kupendekeza kuongeza masoko mapya kwenye ethereum.org.

Kwa sasa tunayaorodhesha kwenye:

Ukurasa huu unamruhusu mtumiaji kuingiza anapoishi na kuona ni masoko yapi anayoweza kutumia. Hii husaidia kubaini mapema kama kuna vizuizi vya kijiografia.

Kwa sababu ya muktadha huu, tunahitaji taarifa mahususi pale unapopendekeza soko.

KUMBUKA: Ikiwa unataka kuorodhesha exchange iliyogatuliwa, angalia sera yetu ya kuorodhesha mikoba na mfumo mtawanyo wa kimamlaka.

Tunachohitaji

  • Vizuizi vya kijiografia vinavyohusiana na soko hilo. Vizuizi vya kijiografia vinavyohusiana na soko la ubadilishaji vinapaswa kuelezwa kwa kina kwenye ukurasa au sehemu maalumu ya tovuti ya soko hilo.
  • Sarafu ambazo watumiaji wanaweza kutumia kununua ETH
  • Uthibitisho kwamba exchange ni kampuni halali ya biashara
  • Taarifa za nyongeza ulizonazo - hizi zinaweza kuwa taarifa kuhusu kampuni kama vile miaka ya kufanya kazi, msaada wa kifedha, nk.

Tunahitaji taarifa hizi ili tuweze kwa usahihi kuwasaidia watumiaji kupata exchange wanayoweza kutumia.

Na pia ili ethereum.org iwe na uhakika zaidi kwamba soko la kubadilishia fedha ni huduma halali na salama.


Ongeza exchange yako

Kama unataka kuongeza soko lako la kubadilishia fedha kwenye ethereum.org, tengeneza suala kwenye GitHub.

Unda suala (opens in a new tab)

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 19 Julai 2024

Je! makala haya yamekusaidia?