Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 19 Julai 2024

Kuongeza rasilimali za maudhui

Hatutarajii kuelezea kila kitu kwenye Ethereum hivyo tunajaribu kuonesha baadhi ya makala bora, mafunzo, barua za taarifa, mbao za matangazo ya kazi na rasilimali mbalimbali za maudhui ambazo zimetengenezwa na jamii. Hii hutoa maelezo zaidi mara kwa mara kuhusu mada ambazo watumiaji wanaweza kuvutiwa nazo.

Kama kuna rasilimali ya maudhui ambayo unahisi inatakiwa iongezwe kwenye ukurasa, jisikie huru kutoa mapendekezo sehemu husika.

Jinsi tunavyoamua

Rasilimali za kujifunzia zitafanyiwa tathmini kwa vigezo vifuatavyo:

  • Je, maudhui ni ya kisasa?
  • Je, maudhui yana kizuizi cha malipo?
  • Je, taarifa ni sahihi? Je, ni ya ukweli au ni ya maoni?
  • Je, mwandishi ni wa kuaminika? ''Je wanafanya vyanzo vyao?
  • Je, maudhui haya yanaongeza thamani mpya ambayo rasilimali/viungo vilivyopo havina?
  • Je, maudhui haya yanahudumia mmoja wa wasifu wetu wa watumiaji (opens in a new tab)?

Ongeza rasilimali yako ya maudhui

Kama unataka kuongeza rasilimali ya maudhui kwenye ethereum.org na imekidhi vigezo, tengeneza suala kwenye GitHub.

Unda suala (opens in a new tab)

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 19 Julai 2024

Je! makala haya yamekusaidia?