Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jinsi ya kutafsiri

Mwongozo wa kuona

Kwa wale wanaojifunza vizuri kwa kuona, mtazame Luka akielekeza jinsi ya kuanza kutumia Crowdin. Vinginevyo, unaweza kupata hatua hizo hizo katika muundo wa maandishi katika sehemu inayofuata.

Mwongozo wa maandishi

Jiunge na mradi wetu kwenye Crowdin

Utahitaji kuingia kwenye akaunti yako ya Crowdin au kujisajili ikiwa bado huna. Kinachohitajika ili kujisajili ni akaunti ya barua pepe na nenosiri.

Jiunge na mradi (opens in a new tab)

Fungua lugha yako

Baada ya kuingia kwenye Crowdin, utaona maelezo ya mradi na orodha ya lugha zote zinazopatikana. Kila lugha pia ina maelezo kuhusu jumla ya maneno yanayoweza kutafsiriwa na muhtasari wa kiasi cha maudhui ambayo yametafsiriwa na kuidhinishwa katika lugha mahususi.

Fungua lugha unayotaka kutafsiri ili kuona orodha ya faili, zinazopatikana kwa ajili ya kutafsiriwa.

List of languages in Crowdin

Tafuta hati ya kufanyia kazi

Maudhui ya tovuti yamegawanywa katika idadi ya hati na makundi ya maudhui. Unaweza kuangalia maendeleo ya kila hati upande wa kulia – ikiwa maendeleo ya tafsiri yako chini ya 100%, tafadhali changia!

Huoni lugha yako imeorodheshwa? Fungua suala (opens in a new tab) au uliza kwenye Discord (opens in a new tab) yetu

Translated and untranslated files in Crowdin

Dokezo kuhusu makundi ya maudhui: tunatumia 'makundi ya maudhui' ndani ya Crowdin ili kupata maudhui yenye kipaumbele cha juu zaidi kutolewa kwanza. Unapoangalia lugha, kwa mfano, Kifilipino (opens in a new tab) utaona folda za kundi la maudhui ("1. Homepage", "2. Essentials", "3. Exploring", n.k.).

Tunakuhimiza utafsiri katika mpangilio huu wa namba (1 → 2 → 3 → ⋯) ili kuhakikisha kurasa zenye athari kubwa zaidi zinatafsiriwa kwanza.

Tafsiri

Baada ya kuchagua faili unayotaka kutafsiri, itafunguka katika kihariri cha mtandaoni. Ikiwa hujawahi kutumia Crowdin hapo awali, unaweza kutumia mwongozo huu wa haraka kupitia mambo ya msingi.

Crowdin online editor

1 – Utepe wa kushoto

  • Haijatafsiriwa (nyekundu) – maandishi ambayo hayajafanyiwa kazi bado. Hizi ndizo tungo unazopaswa kuwa unatafsiri.
  • Imetafsiriwa (kijani) – maandishi ambayo tayari yametafsiriwa, lakini bado hayajakaguliwa. Unakaribishwa kupendekeza tafsiri mbadala, au kupiga kura kwenye zile zilizopo kwa kutumia vitufe vya ‘’+’’ na ‘’-‘‘ katika kihariri.
  • Imeidhinishwa (alama ya tiki) – maandishi ambayo tayari yamekadiriwa na kwa sasa yapo moja kwa moja kwenye tovuti.

Unaweza pia kutumia vitufe vilivyo juu kutafuta tungo mahususi, kuzichuja kwa hali au kubadilisha mwonekano.

2 – Eneo la kihariri

Eneo kuu la kutafsiri – maandishi ya chanzo yanaonyeshwa juu, pamoja na muktadha wa ziada na picha za skrini, ikiwa zinapatikana. Ili kupendekeza tafsiri mpya, weka tafsiri yako katika sehemu ya ‘’Enter translation here’’ (Weka tafsiri hapa) na ubofye Hifadhi.

Unaweza pia kupata tafsiri zilizopo za tungo na tafsiri katika lugha nyingine katika sehemu hii, pamoja na zinazolingana na kumbukumbu ya tafsiri na mapendekezo ya tafsiri ya mashine.

3 – Utepe wa kulia

Hapa ndipo unapoweza kupata maoni, maingizo ya kumbukumbu ya tafsiri na maingizo ya faharasa. Mwonekano chaguomsingi unaonyesha maoni na kuruhusu watafsiri kuwasiliana, kuibua masuala au kuripoti tafsiri zisizo sahihi.

Kwa kutumia vitufe vilivyo juu, unaweza pia kubadili kwenda kwenye Kumbukumbu ya Tafsiri (Translation Memory), ambapo unaweza kutafuta tafsiri zilizopo, au kwenye Faharasa (Glossary), ambayo ina maelezo na tafsiri sanifu za maneno muhimu.

Unataka kujifunza zaidi? Jisikie huru kuangalia nyaraka kuhusu kutumia kihariri cha mtandaoni cha Crowdin (opens in a new tab)

Mchakato wa ukaguzi

Mara tu unapokamilisha tafsiri (yaani, faili zote za kundi la maudhui zinaonyesha 100%), huduma yetu ya kitaalamu ya kutafsiri itakagua (na ikiwezekana kuhariri) maudhui. Pindi ukaguzi utakapokamilika (yaani, maendeleo ya ukaguzi ni 100%), tutayaongeza kwenye tovuti.

Tafadhali usitumie tafsiri ya mashine kutafsiri mradi. Tafsiri zote zitakaguliwa kabla ya kuongezwa kwenye tovuti. Ikiwa tafsiri zako zilizopendekezwa zitagundulika kuwa zimetafsiriwa na mashine, zitatupiliwa mbali na wachangiaji wanaotumia tafsiri ya mashine mara kwa mara wataondolewa kwenye mradi.

Wasiliana nasi

Je, una maswali yoyote? Au unataka kushirikiana na timu yetu na watafsiri wengine? Tafadhali chapisha katika chaneli ya #translations ya seva yetu ya Discord ya ethereum.org (opens in a new tab)

Unaweza pia kuwasiliana nasi kupitia translations@ethereum.org (opens email client)

Asante kwa ushiriki wako katika Mpango wa Kutafsiri wa ethereum.org!