Unaweza kupata miongozo na zana muhimu kwa watafsiri wa ethereum.org, pamoja na jamii za watafsiri na sasisho hapa chini.
Miongozo
- Mwongozo wa mtindo wa kutafsiri – maagizo na vidokezo kwa watafsiri wa ethereum.org
- Mwongozo wa kihariri cha mtandaoni cha Crowdin (inafunguka katika kichupo kipya) – mwongozo wa kina wa kutumia kihariri cha mtandaoni cha Crowdin na baadhi ya vipengele vya hali ya juu vya Crowdin
Zana
- Linguee (inafunguka katika kichupo kipya) – injini ya utafutaji ya tafsiri na kamusi inayowezesha kutafuta kwa neno au kirai
- Utafutaji wa maneno wa Proz (inafunguka katika kichupo kipya) – hifadhidata ya kamusi za tafsiri na faharasa za maneno maalum
- Eurotermbank (inafunguka katika kichupo kipya) – mikusanyiko ya istilahi za Ulaya katika lugha 42
Jamii
- Vikundi vya tafsiri vya Discord vya lugha maalum (inafunguka katika kichupo kipya) – mpango wa kuunganisha watafsiri wa ethereum.org kwenye Vikundi vya Tafsiri
- Kikundi cha watafsiri wa Kichina (inafunguka katika kichupo kipya) – Ukurasa wa Notion kwa uratibu rahisi kati ya watafsiri wa Kichina
Sasisho za hivi punde
Ili kusasishwa na maendeleo ya hivi punde ya Programu ya Kutafsiri, unaweza kufuata blogu ya Taasisi ya Ethereum (inafunguka katika kichupo kipya):
- Sasisho la hatua muhimu za Oktoba 2021 (inafunguka katika kichupo kipya)
- Sasisho la hatua muhimu za Desemba 2020 (inafunguka katika kichupo kipya)
- Sasisho la hatua muhimu za Julai 2020 (inafunguka katika kichupo kipya)
- Uzinduzi wa Programu ya Kutafsiri wa Agosti 2019 (inafunguka katika kichupo kipya)
Saa za ofisi kwa watafsiri
Tuna saa za ofisi kwa watafsiri Jumatano ya pili ya kila mwezi. Hizi hufanyika katika chaneli ya sauti ya #office-hours kwenye Discord ya ethereum.org (inafunguka katika kichupo kipya), ambapo unaweza pia kupata nyakati kamili na maelezo ya ziada.
Saa za ofisi huruhusu watafsiri wetu kuuliza maswali kuhusu mchakato wa kutafsiri, kutoa maoni kuhusu programu, kushiriki mawazo yao, au kupiga soga tu na timu kuu ya ethereum.org. Hatimaye, tunataka kutumia simu hizi kuwasiliana kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya Programu ya Kutafsiri na kushiriki vidokezo na maagizo muhimu na wachangiaji wetu.
Ikiwa wewe ni mtafsiri wa ethereum.org au ungependa kuwa mmoja, jisikie huru kujiunga nasi wakati wa mojawapo ya vipindi hivi.