DAOs ni nini?
Mashirika huru gatuzi (DAO) ni mashirika yanayomilikiwa kwa pamoja kufanya kazi kuelekea malengo ya kushirikishana.
Mashirika huru yaliogatuliwa (DAOs) yanaturuhusu kufanya kazi na watu wenye mielekeo kama yetu ulimwenguni kote pasipokuwepo kuamini kiongozi mwema atakae simamia fedha au operesheni zetu. Hakuna mkurugenzi mtendaji ambaye atatumia fedha kwa mpigo wala afisa mkuu wa fedha wakuharibu vitabu vya fesha. Badala yake, sheria za minyororo ya bloku zilizookwa kwenye kanunu, zinafafanua vile shirika linafanya kazi na vile fedha zinatumika.
Wana hazina zilizojengwa ndani ambazo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuzipata bila idhini ya kikundi. Maamuzi hutawaliwa na mapendekezo na upigaji kura ili kuhakikisha kila mtu katika shirika ana sauti, na kila kitu hutokea kwa uwazi .
Kwanini tunahitaji DAO?
Kuanzisha shirika na mtu anayehusisha ufadhili na pesa kunahitaji uaminifu mkubwa kwa watu unaofanya kazi nao. Lakini ni vigumu kumwamini mtu ambaye umesiliana naye mtandaoni tu. Ukiwa na DAO huhitaji kumwamini mtu mwingine yeyote kwenye kikundi, ila msimbo wa DAO pekee, ambao uko wazi 100% na unaweza kuthibitishwa na mtu yeyote.
Hii inafungua fursa nyingi mpya za ushirikiano na uratibu wa kimataifa.
Ulinganisho
| DAO | Shirika la jadi |
|---|---|
| Huwa ni tambarare, na iliyo na demokrasia kamili. | Kwa kawaida huwa na madaraja. |
| Ili mabadilioko yoyote yafanyike wanachama lazima wapige kura. | Mabadiliko yanaweza kuhitajika kutoka chama pekee, ama upigaji wa kura utakuwepo, kwa kutegemea muundo. |
| Kura zitahesabiwa, na matokeo yatatekelezwa kwa njia ya otomatiki bila kutumia mpatanishi. | Kama upigaji kura utaruhusiwa, kura zitahesabiwa ndani, na matokeo ya upigaji kura lazima yashughulikiwe kwa mikono. |
| Huduma zinazotolewa zinatekelwza kwa njia ya otomatiki kwa namna iliogatuliwa (kwa mfano ugawanyaji wa pesa za hisani). | Inahitaji kutekelezwa na binandamu, ama mfumo wa otomatiki wa kiserikali, ambao unakua hatarini kufanyiwa ghiliba. |
| Shughuli zote ziko wazi kwa jamii. | Shughuli zote zinafanywa kwa siri, na hazitolewi kwa umma. |
Mifano ya DAO
Ili kuongeza uelewa juu ya haya, angalia mifano kadhaa ya DAO ambayo ungeweza kutumia:
- Shirika la hisani – unaweza kukubali michango kutoka kwa mtu yeyote duniani na kupiga kura ni sababu zipi za kufadhili.
- Umiliki wa pamoja – unaweza kununua mali halisi au za kidijitali na wanachama wanaweza kupiga kura jinsi ya kuzitumia.
- Ubia na ruzuku – unaweza kuunda mfuko wa ubia unaokusanya mtaji wa uwekezaji na kupiga kura kuhusu ubia gani wa kuunga mkono. Malipo yanaweza kugawanya baadae miongoni mwa wanachama wa DAO.
DAO zinafanyaje kazi?
Uti wa mgongo wa DAO ni , unaofafanua sheria za shirika na kushikilia hazina ya kikundi. Pale mkataba unapokua hai kwenye Ethereum, hakuna anaeweza kubadili sheria ila kwa kupiga kura tu. Kama mtu yeyote atajaribu kufanya kitu kinyume na sheria na mantiki ya msimbo, hatafanikiwa. Kwasababu mkataba erevu hufafanua hazina, inamaana kwamba hamna mtu anayeweza kutumia pesa bila kuruhusiwa na kundi. Hii inamaana DAO hazihitaji mamlaka ya kati. Badala yake, kundi hutoa maamuzi kwa pamoja, na malipo yanaruhusiwa kwa automatiki pale kura zinapopigwa.
Hii inawezekana kwasababu mikataba erevu ina ngao-ya-uvamizi mara inapokua hai kwenye Ethereum. Huwezi kuhariri msimbo (sheria za DAO) bila watu kugundua kwasababu kila kitu kiko wazi kwa umma.
Ethereum na DAOs
Ethereum ndio msingi thabiti wa DAO kwasababu kadhaa:
- Makubaliano ya Ethereum yamesambazwa na yenye nguvu ya kutosha mpaka mashirika kuamini mtandao.
- Msimbo wa mkataba erevu hauwezi kubadilishwa pale unapokua hai, hata na wamiliki wake. Hii huruhusu DAO kujiendesha na masharti yaliowekwa kwenye msimbo toka mwanzo.
- Mikataba erevu inaweza kutuma/kupokea fedha. Bila hii ungehitaji mpatanishi unaemuamini ili asimamie fedha za kundi.
- Jamii ya Ethereum imethibitishwa kuwa ya ushirikiano zaidi kuliko ushindani, na hii imeruhusu utendaji mzuri na mifumo ya usaidizi kuvumbuliwa haraka zaidi.
Utawala wa DAO
Kuna mambo mengi ya kuzingatia unapo tawala DAO, kama vile upigaji kura na kazi ya mapendekezo.
Uwakilishi
Ujumbe ni kama DAO toleo la wajumbe kidemokrasia. Wamiliki tokeni hukabidhi kura kwa watumizi amabao hujiteua wenyewe na kujitolea kuwakili programu and kukaa kujulishwa.
Mfano maarufu {#governance-example}ENSopens in a new tab – Wamiliki wa ENS wanaweza kukabidhi kura zao kwa wanajamii wanaoshiriki kikamilifu ili kuwawakilisha.
Utawala wa muamala wa kiotomatiki
Kwa mikataba ya DAO, makubaliano hutekelezwa moja kwa moja kama kiwango cha kura za wanachama zinakubaliana.
Mfano maarufu
Nounsopens in a new tab – Katika Nouns DAO, muamala hutekelezwa kiotomatiki ikiwa akidi ya kura itafikiwa na walio wengi wakipiga kura ya ndiyo, mradi tu haijapingwa na waanzilishi.
Utawala wa Multisig
Ingawa DAOs zinaweza kuwa na maelfu ya wanachama wapigakura, fedha zinaweza kuwekwa kwenye unaotumiwa na wanajamii 5-20 hai wanaoaminika na kwa kawaida utambulisho wao ni wa umma (utambulisho wa umma unaojulikana na jamii). Baada ya kura, watia sahihi wa hutekeleza matakwa ya jamii.
Sheria za DAO
Mwaka wa 1977, eneo la wyoming ilivumbua dhima yenye kikomo (LLC) amabayo hukinga waekezaji na kuweka kikomo cha madeni. Hivi majuzi, walianzisha sheria za DAO ambazo ziliweka kisheria hali ya DAO. Kwa sasa wyoming, vermont na kisiwa cha virgin wana sheria za DAO kwa njia moja ama nyingine.
Mfano maarufu
CityDAOopens in a new tab – CityDAO ilitumia sheria ya DAO ya Wyoming kununua ekari 40 za ardhi karibu na Hifadhi ya Taifa ya Yellowstone.
Uanachama wa DAO
Kuna mifano tofauti tofauti ya uanachama wa DAO. Uanachama unaweza kuamua jinsi upigaji kura utafanya kazi na sehemu nyingine kuu za DAO husika.
Uanachama unaotegemea tokeni
Kwa kawaida kikamilifu, kulingana na tokeni inayotumika. Mara nyingi tokeni hizi za utawala zinaweza kuuzwa bila ruhusa kwenye . Tokeni nyingine zitapatikana kwa kutoa ukwasi au baadhi ya 'uthibitisho-wa-kazi'. Kwa vyovyote vile, ukishikilia ruzuku za tokeni zinahukupa nafasi ya kupiga kura.
Kwa kawaida hutumika kutawala itifaki pana zilizogatuliwa na/au tokeni zenyewe.
Mfano maarufu
MakerDAOopens in a new tab – Tokeni ya MakerDAO, MKR, inapatikana kwa wingi kwenye exchange zisizogatuliwa, na mtu yeyote anaweza kuinunua ili awe na uwezo wa kupiga kura kuhusu mustakabali wa itifaki ya Maker.
Uanachama unaotegemea hisa
DAO za-hisa zinahitaji ruhusa, ila bado ziko wazi. Mwanachama mtarajiwa yeyote anaweza akatoa pendekezo kujiunga na DAO, mara nyingi hutoa kodi ya thamani fulani katika mfumo wa tokeni au kazi. Hisa hutoa nguvu ya kupiga kura moja kwa moja na umiliki. Washiriki wanaweza kutoka mda wowote na uwiano wao wa sehemu ya hazina.
Hua inatumika kwa ajili ya muunganiko wa karibu, mashirika yanayozingatia binadamu kama vile misaada, mikusanyiko ya wafanyakazi na vilabu vya uwekezaji. Inaweza kutawala itifaki na tokeni.
Mfano maarufu
MolochDAOopens in a new tab – MolochDAO imejikita katika kufadhili miradi ya Ethereum. Inahitaji pendekezo kwenye chama ili kundi lifanye tathmini kama unavigezo vinavyokidhi mahitaji na mtaji kufanya maamuzi sahihi kuhusu wafadhili watarajiwa. Huwezi kununua ufikiaji wa DAO kwenye soko la wazi.
Uanachama unaotegemea sifa
Sifa za uanachama zinatoa ushahidi wa ushirika wao na kukupatia nguvu ya upigaji kura kwenye DAO. Kinyume cha tokeni ama uanachama wa msingi wa hisa, uanachama wa msingi wa sifa wa DAO hauhamishi umiliki kwende kwa wachangiaji. Sifa haziwezi kununuliwa, kuhamishwa au kukabidhiwa; wanachama wa DAO lazima wafanye kazi ya kupata sifa hizo kwa kushiriki. Upigaji kura kwenye mnyororo hauhitaji ruhusa na wanachama watarajiwa wanaweza kuwasilisha mapendekezo kwa uhuru ili kujiunga na DAO na kuomba kupokea sifa na tokeni kama zawadi kwa kubadilishana na michango yao.
Kwa kawaida hutumika kwa maendeleo yaliyogatuliwa na utawala wa itifaki na , lakini pia inafaa kwa mashirika mbalimbali kama vile mashirika ya hisani, jumuiya za wafanyakazi, vilabu vya uwekezaji, n.k.
Mfano maarufu
DXdaoopens in a new tab – DXdao ilikuwa kundi huru la kimataifa linalojenga na kutawala itifaki na programu zilizogatuliwa tangu 2019. Ilitumia utawala unaotegemea sifa na ili kuratibu na kusimamia fedha, ikimaanisha hakuna mtu angeweza kununua ushawishi wa kuathiri mustakabali wake au utawala.
Jiunge na / anzisha DAO
Jiunge na DAO
- DAOs za jumuiya ya Ethereum
- Orodha ya DAOs ya DAOHausopens in a new tab
- Orodha ya DAOs ya Tally.xyzopens in a new tab
- Orodha ya DAOs ya DeGov.AIopens in a new tab
Anzisha DAO
- Anzisha DAO na DAOHausopens in a new tab
- Anzisha Governor DAO na Tallyopens in a new tab
- Unda DAO inayoendeshwa na Aragonopens in a new tab
- Anzisha colonyopens in a new tab
- Unda DAO kwa kutumia makubaliano ya holografia ya DAOstackopens in a new tab
- Zindua DAO ukitumia DeGov Launcheropens in a new tab
Masomo zaidi
Makala za DAO
- DAO ni nini?opens in a new tab – Aragonopens in a new tab
- House of DAOsopens in a new tab – Metagameopens in a new tab
- DAO ni nini na inatumika kwa nini?opens in a new tab – DAOhausopens in a new tab
- Jinsi ya Kuanzisha Jumuiya ya Kidijitali Inayoendeshwa na DAOopens in a new tab – DAOhausopens in a new tab
- DAO ni nini?opens in a new tab – Coinmarketcapopens in a new tab
- Makubaliano ya Holografia ni Nini?opens in a new tab - DAOstackopens in a new tab
- DAOs si mashirika: ambapo ugatuzi katika mashirika yanayojitawala ni muhimu, na Vitalikopens in a new tab
- DAOs, DACs, DAs na Zaidi: Mwongozo Usiokamilika wa Istilahiopens in a new tab - Blogu ya Ethereumopens in a new tab
Video
- DAO ni nini katika crypto?opens in a new tab
- Je, DAO Inaweza Kujenga Jiji?opens in a new tab – TEDopens in a new tab
Test your Ethereum knowledge
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 14 Februari 2026
