Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Jinsi ya Kuona NFT Yako katika Pochi Yako (Sehemu ya 3/3 ya Mfululizo wa Mafunzo ya NFT)

ERC-721
Alchemy
Solidity
Beginner
Sumi Mudgil
22 Aprili 2021
2 minute read

Mafunzo haya ni Sehemu ya 3/3 katika mfululizo wa Mafunzo ya NFT, ambapo tunaona NFT yetu mpya iliyotengenezwa. Hata hivyo, unaweza kutumia mafunzo ya jumla kwa tokeni yoyote ya ERC-721 ukitumia MetaMask, ikiwemo kwenye Mtandao Mkuu au testnet yoyote. Ikiwa ungependa kujifunza jinsi ya kutengeneza NFT yako mwenyewe kwenye Ethereum, unapaswa kuangalia Sehemu ya 1 kuhusu Jinsi ya Kuandika na Kupeleka mkataba-erevu wa NFT!

Hongera! Umefika kwenye sehemu fupi na rahisi zaidi ya mfululizo wetu wa mafunzo ya NFT — jinsi ya kuona NFT yako iliyotengenezwa hivi punde kwenye pochi pepe. Tutatumia MetaMask kwa mfano huu kwa kuwa ndiyo tuliyoitumia katika sehemu mbili zilizopita.

Kama sharti, unapaswa kuwa tayari umesakinisha MetaMask kwenye simu ya mkononi, na inapaswa kujumuisha akaunti ambayo ulitengenezea NFT yako — unaweza kupata programu bila malipo kwenye iOSopens in a new tab au Androidopens in a new tab.

Hatua ya 1: Weka mtandao wako kuwa Sepolia

Juu ya programu, bonyeza kitufe cha “Pochi”, baada ya hapo utaambiwa uchague mtandao. Kwa kuwa NFT yetu ilitengenezwa kwenye mtandao wa Sepolia, utataka kuchagua Sepolia kama mtandao wako.

Jinsi ya kuweka Sepolia kama mtandao wako kwenye MetaMask Mobile

Hatua ya 2: Ongeza mkusanyiko wako kwenye MetaMask

Ukishakuwa kwenye mtandao wa Sepolia, chagua kichupo cha “Vikusanywa” upande wa kulia na ongeza anwani ya mkataba-erevu wa NFT na ID ya tokeni ya ERC-721 ya NFT yako — ambayo unapaswa kuipata kwenye Etherscan kulingana na hashi ya muamala kutoka kwa NFT yako iliyopelekwa katika Sehemu ya II ya mafunzo yetu.

Jinsi ya kupata hashi ya muamala wako na ID ya tokeni ya ERC-721

Huenda ukahitaji kuonyesha upya mara kadhaa ili kuona NFT yako — lakini itakuwepo !

Jinsi ya kupakia NFT yako kwenye MetaMask

Hongera! Umetengeneza NFT kwa mafanikio, na sasa unaweza kuiona! Tuna hamu ya kuona jinsi utakavyoutikisa ulimwengu wa NFT!

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 4 Desemba 2023

Umesaidika na mafunzo haya?