Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 23 Februari 2026

Jinsi ya Kubatilisha mkataba erevu usifikie fedha zako za kripto

Mwongozo huu utakufundisha jinsi ya kutazama orodha ya zote ambazo umeziruhusu kufikia fedha zako na jinsi ya kuzighairi.

Wakati mwingine wasanidi programu wadanganyifu huweka milango ya siri kwenye mikataba mahiri ambayo inaruhusu kupata fedha za watumiaji wasiojua, ambao huingiliana na mkataba huo mahiri. Kinachotokea mara kwa mara ni kwamba mifumo kama hiyo humwomba mtumiaji ruhusa ya kutumia idadi isiyo na kikomo ya tokeni kwa jaribio la kuokoa kiasi kidogo cha siku zijazo, lakini hii huja na hatari iliyoongezeka.

Mara tu jukwaa linapokuwa na haki za ufikiaji zisizo na kikomo kwa tokeni kwenye yako, wanaweza kutumia tokeni hizo zote hata kama umetoa fedha zako kutoka kwenye jukwaa lao na kuzirudisha kwenye mkoba wako. Wafanya maovu bado wanaweza kufikia fedha zako na kuzitoa kuzipeleka hadi kwenye mikoba yao bila wewe kuwa na njia yoyote ya kuzirejesha.

Ulinzi pekee ni kujiepusha kutumia miradi mipya ambayo haijajaribiwa, idhinisha kile unachohitaji tu, au futa mara kwa mara ruhusa ulizozitoa awali. Sasa, jinsi gani unaweza fanya ivyo?

Hatua 1: Tumia kifaa cha kubatilisha zana ya ufikiaji

Kuna tovuti kadhaa zinazokuwezesha kuona na kubatilisha mikataba mahiri iliyounganishwa na anwani yako. Tembelea tovuti na unganisha mkoba wako:

Hatua 2: Unganisha mkoba wako

Ukiwa tayari kwenye tovuti, bonyeza kwenye "Unganisha mkoba". Tovuti itakuletea wewe uunganishe mkoba wako.

Hakikisha kuwa unatumia mtandao mmoja kwenye mkoba wako na tovuti. Utaona tu mikataba mahiri inayohusiana na mtandao uliochagua. Kwa mfano, kama unaunganisha Ethereum Mainnet, utaona tu mikataba ya Ethereum, na sio mikataba kutoka kwenye minyororo mingine kama Polygon.

Hatua 3: Chagua mkataba mahiri unaotaka kuubatilisha

Unatakiwa kuona mikataba yote ambayo imeruhusiwa kuunganishwa na tokeni zako na kiasi chake cha matumizi. Tafuta ule unaotaka kusitisha.

Kama hujui mkataba upi wa kuchagua, unaweza batilisha mikataba yote. Haitakuletea matatizo yoyote, lakini utahitaji kutoa ruhusa mpya tena wakati mwingine utakaposhirikiana na yoyote kati ya mikataba hii.

Hatua 4: Batilisha ruhusa ya kuweza kufikia fedha zako

Mara tu unapobonyeza kubatilisha, unapaswa kuona pendekezo jipya la muamala kwenye mkoba wako. Hii ni ya kutarajiwa. Itabidi ulipe ada ili kufuta huko kufanikiwe. Kutegemea na mtandao, hii inaweza kuchukua kuanzia dakika moja hadi kadhaa ili kuchakatwa.

Tunakushauri uonyeshe upya chombo cha kubatilisha ruhusa baada ya dakika chache na kuunganisha tena mkoba wako ili kuangalia mara mbili kama mkataba uliotolewa umepotea kutoka kwenye orodha.

Tunapendekeza kamwe usiruhusu miradi ufikiaji usio na kikomo kwa tokeni zako na ughairi ruhusa zote za ufikiaji wa tokeni mara kwa mara. Kughairi ufikiaji wa tokeni kamwe hakupaswi kusababisha upotevu wa fedha, hasa ukitumia zana zilizoorodheshwa hapo juu.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, kubatilisha ufikiaji wa tokeni pia kunakomesha kusindika, kuweka kwa pamoja kwenye bwawa, kukopesha n.k?

Hapana, haitaathiri mikakati yoyote ya uliyonayo. Bado utabaki katika nafasi zako na kuendelea kupata zawadi n.k.

Je, kukata muungano wa mkoba kutoka kwenye mradi ni sawa na kuondoa ruhusa ya kutumia pesa zangu?

Hapana, ukiondoa mkoba wako kwenye mradi, lakini tayari umetoa ruhusa ya kutumia tokeni, bado wanaweza kutumia tokeni hizo. Inakupasa kubatilisha ruhusa hiyo.

Ruhusa ya mkataba itakwisha lini?

Hakuna tarehe ya mwisho wa matumizi kwenye ruhusa za mkataba. Kama utatoa ruhusa ya mkataba, zinaweza kutumika, hata miaka mingi baada ya kutolewa.

Kwa nini miradi huweka ruhusa ya matumizi ya tokeni isiyo na kikomo?

Miradi mara nyingi hufanya hivi ili kupunguza idadi ya maombi yanayohitajika, ikimaanisha mtumiaji anapaswa kuidhinisha mara moja tu na kulipa ada ya muamala mara moja tu. Ingawa hii ni rahisi, inaweza kuwa hatari kwa watumiaji kuidhinisha bila uangalifu, hasa kwenye tovuti ambazo hazijathibitishwa na wakati au kukaguliwa. Baadhi ya mikoba hukuruhusu kuzuia mwenyewe kiasi cha tokeni zinazoidhinishwa ili kupunguza hatari yako. Wasiliana na mtoa huduma wa mkoba wako kwa maelezo zaidi.

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 23 Februari 2026

Je! makala haya yamekusaidia?