Mtandao wa Ethereum hulinda mabilioni ya dola za thamani 24/7, 365. Vipi?
Watu kote ulimwenguni hufungia (au “kuweka dhamana”) Etha (ETH) katika mikataba mahiri ili kuendesha programu inayochakata miamala ya Ethereum na kulinda mtandao wa Ethereum. Kama malipo, wanapata tuzo ya ETH zaidi.
Uwekaji dhamana upya ni teknolojia iliyojengwa kwa ajili ya waweka dhamana ili kupanua usalama huu kwa huduma, programu, au mitandao mingine. Kama malipo, wanapata tuzo za ziada za uwekaji dhamana upya. Hata hivyo, pia wanaweka ETH yao iliyowekwa dhamana katika hatari zaidi.
Uwekaji dhamana upya umefafanuliwa kwa dakika 18
Uwekaji dhamana upya ni nini?
Uwekaji dhamana upya ni pale waweka dhamana wanapotumia ETH yao ambayo tayari imewekwa dhamana kulinda huduma zingine zilizogatuliwa. Kama malipo, waweka dhamana upya wanaweza kupata tuzo za ziada kutoka kwa huduma hizo zingine juu ya tuzo zao za kawaida za uwekaji dhamana wa ETH.
Huduma zilizogatuliwa zinazolindwa na uwekaji dhamana upya zinajulikana kama "Huduma Zilizothibitishwa Kikamilifu" (Actively Validated Services - AVSs). Kwa njia sawa na ambayo waweka dhamana wengi wa ETH huendesha programu ya uthibitishaji ya Ethereum, waweka dhamana upya wengi huendesha programu maalum ya AVS.
Ni vyema kujua
Ingawa "Huduma Zilizothibitishwa Kikamilifu" (AVSs) ndiyo inayojulikana zaidi, majukwaa tofauti ya uwekaji dhamana upya yanaweza kutumia majina mengine kwa huduma zilizogatuliwa yanazosaidia kulinda, kama vile "Huduma Zilizothibitishwa Kiotomatiki," "Huduma Salama Zilizosambazwa," au "Mitandao."
Uwekaji dhamana dhidi ya uwekaji dhamana upya
| Uwekaji dhamana | Uwekaji dhamana upya |
|---|---|
| Pata tuzo za ETH | Pata tuzo za ETH + tuzo za AVS |
| Hulinda mtandao wa Ethereum | Hulinda mtandao wa Ethereum + AVSs |
| Hakuna kiwango cha chini cha ETH | Hakuna kiwango cha chini cha ETH |
| Kiwango cha chini cha hatari | Kiwango cha hatari cha chini hadi juu |
| Muda wa kutoa unategemea foleni | Muda wa kutoa unategemea foleni + kipindi cha kuondoa kifungo |
Kwa nini tunahitaji uwekaji dhamana upya?
Fikiria ulimwengu mbili; moja yenye uwekaji dhamana upya na nyingine isiyo nayo.


Katika ulimwengu huu wenye uwekaji dhamana upya, AVS na mweka dhamana wananufaika kwa kuweza kutafutana na kubadilishana usalama kwa tuzo za ziada.
Faida ya ziada ya uwekaji dhamana upya
AVSs zinaweza kuweka rasilimali zao zote katika kujenga na kutangaza huduma zao, badala ya kukengeushwa na ugatuzi na usalama.
Uwekaji dhamana upya unafanyaje kazi?
Kuna vyombo kadhaa vinavyohusika katika uwekaji dhamana upya — kila kimoja wapo kina jukumu muhimu.
| Neno | Maelezo |
|---|---|
| Majukwaa ya uwekaji dhamana upya | Jukwaa la uwekaji dhamana upya ni huduma inayounganisha AVSs, waweka dhamana wa ETH, na waendeshaji. Wanajenga programu zilizogatuliwa kwa waweka dhamana kuweka dhamana upya ETH yao, na masoko ambapo waweka dhamana, AVSs, na waendeshaji wanaweza kutafutana. |
| Waweka dhamana upya asilia | Watu wanaoweka dhamana ETH yao kwa kuendesha wathibitishaji wao wenyewe wa Ethereum wanaweza kuunganisha ETH yao iliyowekwa dhamana kwenye jukwaa la uwekaji dhamana upya, ikiwa ni pamoja na EigenLayer na mengineyo, ili kupata tuzo za uwekaji dhamana upya juu ya tuzo za mthibitishaji wa ETH. |
| Waweka dhamana upya wenye ukwasi | Watu wanaoweka dhamana ETH yao kupitia mtoa huduma wa uwekaji dhamana wenye ukwasi wa tatu, kama Lido au Rocket Pool, wanapata tokani za uwekaji amana wenye ukwasi (LSTs) zinazowakilisha ETH yao iliyowekwa dhamana. Wanaweza kuweka dhamana upya LSTs hizi ili kupata tuzo za uwekaji dhamana upya huku wakiweka ETH yao ya asili ikiwa imewekwa dhamana. |
| Waendeshaji | Waendeshaji huendesha programu ya uwekaji dhamana upya ya AVSs, wakifanya kazi za uthibitishaji ambazo kila AVS inahitaji. Waendeshaji kwa kawaida ni watoa huduma wa kitaalamu wanaohakikisha mambo kama vile muda wa kufanya kazi na utendaji. Kama waweka dhamana upya wasio waendeshaji, waendeshaji hutumia ETH iliyowekwa dhamana kulinda AVSs, lakini waendeshaji pia hupokea tuzo za ziada badala ya kazi yao. |
| AVSs | Hizi ni huduma zilizogatuliwa — kama vile orako za bei, madaraja ya tokeni, na mifumo ya data — zinazopokea usalama kutoka kwa waweka dhamana upya na kutoa tuzo za tokeni kama malipo. |
Ni vyema kujua
Waweka dhamana upya asilia na wenye ukwasi mara nyingi hukaimisha ETH yao iliyowekwa dhamana kwa mwendeshaji, badala ya kuendesha programu ya kulinda AVSs wenyewe.
Kwa njia hii hawahitaji kuwa na wasiwasi kuhusu mahitaji magumu ya kiufundi kutoka kwa AVSs, ingawa wanapokea kiwango cha chini cha tuzo kuliko waendeshaji.
Ni mifano gani ya uwekaji dhamana upya?
Ingawa ni wazo geni, miradi michache imeibuka ili kuchunguza uwezekano wa uwekaji dhamana upya.
EigenLayer (Restaking Platform)EigenLayer introduced the idea of restaking in 2023 and has grown to thousands of people restaking millions of ETH. Referred to as “Ethereum middleware”, it connects stakers, operators and AVSs.
Symbiotic (Restaking platform)Symbiotic is a permissionless restaking protocol that helps secure different blockchain networks by letting users “restake” their assets.
Tahadhari ya jina lisilo sahihi
Baadhi ya watu huchanganya "uwekaji dhamana upya" na ukopeshaji na ukopaji wa LSTs katika fedha zilizogatuliwa (DeFi). Zote mbili huweka ETH iliyowekwa dhamana kufanya kazi, lakini uwekaji dhamana upya unamaanisha kulinda AVSs, sio tu kupata faida kwenye LSTs.
Naweza kupata kiasi gani kutokana na uwekaji dhamana upya?
Ingawa AVSs hutoa viwango tofauti, Tokeni za Uwezeshaji Dhamana Upya Zenye Ukwasi (LRTs) kama eETH zinakupa wazo la kiasi unachoweza kupata. Kwa njia sawa na unavyopata LSTs kama stETH kwa kuweka dhamana ETH yako, unaweza kupata LRTs kama eETH kwa kuweka dhamana upya stETH. Tokeni hizi hupata tuzo za uwekaji dhamana wa ETH na uwekaji dhamana upya.
Ni muhimu kutambua hatari zinazohusiana na uwekaji dhamana upya. Tuzo zinazowezekana zinaweza kuvutia, lakini hazikosi hatari.
Ni zipi hatari za uwekaji dhamana upya?
| Hatari | Maelezo |
|---|---|
| Adhabu (au “ukataji”) | Kama uwekaji dhamana wa ETH, ikiwa waweka dhamana upya/waendeshaji wataenda nje ya mtandao, kudhibiti jumbe au kujaribu kuharibu mtandao, dhamana yao inaweza kukatwa (kuchomwa) kwa kiasi au kabisa. |
| Uwekaji kati | Ikiwa waendeshaji wachache watatawala sehemu kubwa ya uwekaji dhamana upya wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa waweka dhamana upya, AVSs na hata majukwaa ya uwekaji dhamana upya. |
| Athari za mnyororo | Ikiwa mweka dhamana upya atakatwa wakati analinda AVSs nyingi, hii inaweza kupunguza usalama kwa AVSs zingine, na kuzifanya ziwe hatarini. |
| Upatikanaji wa fedha mara moja | Kuna muda wa kusubiri (au “kipindi cha kuondoa kifungo”) kwa kutoa ETH iliyowekwa dhamana upya kwa hivyo huenda usiweze kupata ufikiaji mara moja kila wakati. |
Mwanzilishi mwenza wa Ethereum anaandika…
Vitalik, mwanzilishi mwenza wa Ethereum, alionya kuhusu hatari zinazowezekana za uwekaji dhamana upya katika chapisho la blogu la 2021 lililoitwa Usizidishe Mzigo Kwenye Mwafaka.
Jinsi ya kuanza na uwekaji dhamana upya?
| 🫡 Wanaoanza | 🤓 Watumiaji Wazoefu |
|---|---|
| 1. Weka dhamana ETH kwenye majukwaa kama Lido au Rocket Pool ili kupata LSTs. | 1. Weka dhamana ETH yako kama mthibitishaji kwenye Ethereum. |
| 2. Tumia LSTs hizo kuanza kuweka dhamana upya kwenye huduma ya uwekaji dhamana upya. | 2. Linganisha huduma za uwekaji dhamana upya kama EigenLayer, Symbiotic na zingine. |
| 3. Fuata maagizo ili kuunganisha mthibitishaji wako kwenye mkataba mahiri wa uwekaji dhamana upya. |
Uwekaji Dhamana wa Ethereum : Inafanyaje kazi?
Jifunze ZaidiYa Kina
Usomaji zaidi
- ethereum.org - Mwongozo wa uwekaji dhamana wa ETH
- Ledger Academy - Uwezeshaji Dhamana Upya wa Ethereum ni Nini? (opens in a new tab)
- ConsenSys - EigenLayer: Itifaki ya Uwezeshaji Dhamana Upya wa Ethereum Iliyogatuliwa Imefafanuliwa (opens in a new tab)
- Vitalik Buterin - Usizidishe mzigo kwenye mwafaka wa Ethereum (opens in a new tab)
- Cointelegraph - EigenLayer ni nini? Itifaki ya uwekaji dhamana upya ya Ethereum imefafanuliwa (opens in a new tab)
- a16z crypto research - EigenLayer: Uongezaji wa Kipengele Bila Ruhusa kwenye Ethereum na Sreeram Kannan (opens in a new tab)
- Junion - EigenLayer Imefafanuliwa: Uwezeshaji Dhamana Upya ni Nini? (opens in a new tab)
- The Block - Dashibodi ya Data ya Uwezeshaji Dhamana Upya (opens in a new tab)
