Danksharding
Danksharding ni jinsi Ethereum inavyokuwa blockchain inayoweza kupanuka kikweli, lakini kuna uboreshaji kadhaa wa itifaki unaohitajika ili kufika hapo. Proto-Danksharding ni hatua ya kati katika mchakato huo. Zote mbili zinalenga kufanya miamala kwenye Layer 2 iwe nafuu iwezekanavyo kwa watumiaji na zinapaswa kuongeza Ethereum hadi >100,000 ya miamala kwa sekunde.
Proto-Danksharding ni nini?
Proto-Danksharding, inayojulikana pia kama EIP-4844 (opens in a new tab), ni njia kwa rollups kuongeza data nafuu zaidi kwenye vizuizi. Jina linatokana na watafiti wawili waliopendekeza wazo hilo: Protolambda na Dankrad Feist. Kihistoria, rollups zilikuwa na kikomo katika jinsi zinavyoweza kufanya miamala ya watumiaji kuwa nafuu kwa sababu ya ukweli kwamba zinachapisha miamala yao katika CALLDATA.
Hii ni ghali kwa sababu inachakatwa na nodi zote za Ethereum na inabaki kwenye mnyororo milele, ingawa rollups zinahitaji data hiyo kwa muda mfupi tu. Proto-Danksharding inaleta blobs za data ambazo zinaweza kutumwa na kuambatanishwa kwenye vitalu. Data katika blobs hizi haiwezi kufikiwa na EVM na huondolewa moja kwa moja baada ya kipindi maalumu cha muda (kimewekwa kuwa epochs 4096 kwa wakati wa kuandika, au takriban siku 18). Hii inamaanisha kuwa rollups zinaweza kutuma data zao kwa gharama nafuu zaidi na kupeleka akiba hiyo kwa watumiaji wa mwisho kwa njia ya miamala ya bei nafuu.
Je, data ya blob inathibitishwaje?
Rollups huchapisha miamala wanayoitekeleza katika blobs za data. Pia huchapisha "ahadi" kwa data hiyo. Hufanya hivi kwa kufananisha kazi ya polynomial na data hiyo. Kazi hii inaweza kisha kutathminiwa kwenye pointi mbalimbali. Kwa mfano, tukifafanua kazi rahisi sana f(x) = 2x-1 basi tunaweza kutathmini kazi hii kwa x = 1, x = 2, x = 3 na kupata matokeo 1, 3, 5. Prover anatumia kazi ile ile kwenye data na kutathmini kwenye pointi sawa. Iwapo data ya awali itabadilishwa, kazi hiyo haitakuwa ile ile, na kwa hivyo thamani zinazopatikana kwenye kila pointi pia hazitakuwa sawa. Kwenye ukweli, ahadi na uthibitisho ni mgumu zaidi kwa sababu zimefungwa ndani ya kazi za kriptografia.
KZG ni nini?
KZG ni kifupi cha Kate-Zaverucha-Goldberg - majina ya waandishi watatu wa asili (opens in a new tab) wa mpango unaopunguza donge la data na kulifanya liwe "ahadi" ya kriptografia (opens in a new tab) ndogo. Blob ya data iliyowasilishwa na rollup lazima ithiibishwe ili kuhakikisha kuwa rollup haijatenda vibaya. Hii inahusisha prover kurudia kutekeleza miamala iliyoko kwenye blob ili kuangalia kuwa ahadi ilikuwa halali. Hii kwa dhana ni sawa na jinsi wateja wa utekelezaji wanavyokagua uhalali wa miamala ya Ethereum kwenye tabaka la 1 kwa kutumia uthibitisho wa Merkle. KZG ni uthibitisho mbadala unaofananisha mlinganyo wa polynomial na data. Ahadi inathibitisha polynomial kwa kutathmini kwenye pointi fulani za siri. Prover atafananisha polynomial ile ile juu ya data na kutathmini kwenye thamani sawa, akikagua kwamba matokeo ni yale yale. Hii ni njia ya kuthibitisha data ambayo inalingana na mbinu za zero-knowledge zinazotumika na baadhi ya rollups na hatimaye sehemu nyingine za itifaki ya Ethereum.
Sherehe ya KZG ilikuwa nini?
Sherehe ya KZG ilikuwa njia ya watu wengi kutoka jamii ya Ethereum kushirikiana kuunda mfuatano wa namba za siri za nasibu ambazo zinaweza kutumika kuthibitisha baadhi ya data. Ni muhimu sana kwamba mfuatano huu wa namba usijulikane na usiweze kuundwa upya na mtu yeyote. Ili kuhakikisha hili, kila mtu aliyeshiriki katika sherehe alipokea mfuatano kutoka kwa mshiriki aliyetangulia kabla yake. Kisha wakatengeneza thamani mpya za nasibu (k.m., kwa kuruhusu kivinjari chao kupima msogeo wa kipanya chao) na kuichanganya na thamani ya awali. Baada ya hapo walituma thamani hiyo kwa mshiriki aliyefuata na kuifuta kutoka kwenye kompyuta yao ya ndani. Iwapo mtu mmoja tu katika sherehe alifanya hivi kwa uaminifu, thamani ya mwisho haitajulikana kwa mshambuliaji.
Sherehe ya KZG ya EIP-4844 ilikuwa wazi kwa umma na maelfu ya watu walishiriki kuongeza usahihi wao wa nasibu (randomness). Kwa jumla kulikuwa na michango zaidi ya 140,000, na kuifanya kuwa sherehe kubwa zaidi ya aina yake duniani. Ili sherehe hiyo kudhuriwa, washiriki 100% wa sherehe hiyo wangehitajika kuwa wa udanganyifu kikamilifu. Kutoka kwa mtazamo wa washiriki, ikiwa wanajua walikuwa waaminifu, hakuna haja ya kumuamini mtu mwingine kwa sababu wanajua kwamba walihakikisha sherehe hiyo salama (kila mmoja alitimiza sharti la mshiriki 1-kati -ya -N kuwa waaminifu).
Danksharding ni nini?
Danksharding ni utekelezaji kamili wa upanuzi wa rollup ulioanza na Proto-Danksharding. Danksharding italeta nafasi kubwa sana kwenye Ethereum ili rollups waweze kuingiza data zao za miamala zilizokomeshwa. Hii inamaanisha kuwa Ethereum itakuwa na uwezo wa kuunga mkono mamia ya rollups binafsi kwa urahisi na kufanya mamilioni ya miamala kwa sekunde kuwa halisi.
Jinsi hii inavyofanya kazi ni kwa kupanua blobs zinazounganishwa na vitaku kuanzia sita (6) katika Proto-Danksharding, hadi 64 katika Danksharding kamili. Mabadiliko mengine yote yanayohitajika ni masasisho tu ya jinsi wateja wa makubaliano wanavyofanya kazi ili kuwawezesha kushughulikia blobs kubwa mpya. Mabadiliko kadhaa kati ya haya tayari yako kwenye mpango wa utekelezaji kwa madhumuni mengine ambayo hayahusiani na Danksharding. Kwa mfano, Dankharding inahitaji utengano wa wajenzi wa mapendekezo kutekelezwa. Hii ni sasisho linalotofautisha kazi za kujenga vitalu na kupendekeza vitalu kati ya validators tofauti. Vivyo hivyo, sampuli za upatikaji wa data zinahitajika kwa Danksharding, lakini pia zinahitajika kwa maendeleo ya wateja wepesi sana ambao hawahifadhi data nyingi za kihistoria ("stateless clients").
Maendeleo ya sasa
Full Danksharding bado ipo mbali kwa miaka kadhaa. Wakati huo huo, sherehe ya KZG imekamilika na zaidi ya michango 140,000, na EIP (opens in a new tab) ya Proto-Danksharding imekomaa. Pendekezo hili limewekwa kikamilifu kwenye mitandao yote ya majaribio, na liliaanza kutumika kwenye Mainnet kupitia sasisho la mtandao la Cancun-Deneb ("Dencun") mnamo Machi 2024.
Masomo zaidi
- Madokezo ya Proto-Danksharding (opens in a new tab) - Vitalik Buterin
- Madokezo ya Dankrad kuhusu Danksharding (opens in a new tab)
- Dankrad, Proto na Vitalik wakijadili Danksharding (opens in a new tab)
- Sherehe ya KZG (opens in a new tab)
- Hotuba ya Devcon ya Carl Beekhuizen kuhusu mipangilio inayoaminika (opens in a new tab)
- Zaidi kuhusu sampuli za upatikanaji wa data kwa blobs (opens in a new tab)
- Dankrad Feist kuhusu ahadi na ithibati za KZG (opens in a new tab)
- Ahadi za polinomial za KZG (opens in a new tab)
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 16 Februari 2026