Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Kuboresha uzoefu wa mtumiaji

Bado ni vigumu sana kwa watu wengi kutumia Ethereum. Ili kuhamasisha kukubalika na umma, Ethereum inapaswa kupunguza sana vikwazo vya kujiunga. Watumiaji wanapaswa kupata manufaa ya kutumia Ethereum kwa njia iliyogatuliwa, isiyo na ruhusa, na isiyoweza kudhibitiwa, lakini iwe rahisi kama kutumia programu ya kawaida ya web2.

Kutumia Ethereum kunahitaji kurahisishwa; kuanzia kusimamia na hadi kuanzisha miamala. Ili kuwezesha matumizi na watu wengi, Ethereum ni lazima iongeze urahisi wa matumizi kwa kiasi kikubwa, ikiwaruhusu watumiaji kupata ufikiaji usio na ruhusa na sugu dhidi ya udhibiti kwa Ethereum kwa urahisi kama wa kutumia programu za .

Zaidi ya vifungu vya mbegu

Akaunti za Ethereum zinalindwa na jozi ya funguo zinazotumika kutambua akaunti (ufunguo wa umma) na kutia saini kwenye jumbe (ufunguo wa siri). Ufunguo wa siri ni kama nenosiri kuu. Unaruhusu ufikiaji kamili wa akaunti ya Ethereum. Hii ni njia tofauti ya utendaji kazi kwa watu waliozoea benki na programu za Web2 ambazo husimamia akaunti kwa niaba ya mtumiaji. Ili Ethereum ikubalike na umma bila kutegemea wahusika wengine wa kati, lazima kuwe na njia rahisi na isiyo na usumbufu. Njia hii inapaswa kumwezesha mtumiaji kumiliki rasilimali zake na kudhibiti data yake bila kulazimika kuelewa kriptografia ya funguo za umma na siri au usimamizi wa funguo.

Suluhisho la hili ni kutumia mikoba ya ili kuingiliana na Ethereum. Pochi za mkataba janja huunda njia za kulinda akaunti ikiwa funguo zimepotea au kuibiwa, hutoa fursa za kugundua na kuzuia ulaghai vizuri zaidi, na huruhusu pochi kupata utendaji mpya. Ingawa pochi za mkataba janja zipo leo, ni ngumu kuzijenga kwa sababu itifaki ya Ethereum inahitaji kuziunga mkono vizuri zaidi. Usaidizi huu wa ziada unajulikana kama 'account abstraction'.

Maelezo zaidi kuhusu account abstraction

Nodi kwa kila mtu

Watumiaji wanaoendesha hawahitaji kuamini wahusika wengine kuwapa data, na wanaweza kuingiliana haraka, kwa faragha, na bila ruhusa na wa Ethereum. Hata hivyo, kuendesha nodi kwa sasa kunahitaji maarifa ya kiufundi na nafasi kubwa kwenye diski. Hii inamaanisha watu wengi lazima waamini wapatanishi badala yake.

Kuna maboresho kadhaa yatakayofanya uendeshaji wa nodi uwe rahisi zaidi na utumie rasilimali chache sana. Njia ya kuhifadhi data itabadilishwa ili kutumia muundo unaotumia nafasi vizuri zaidi unaojulikana kama Verkle Tree. Pia, kukiwa na hali ya kutohifadhi data au kuisha kwa muda wa data, nodi za Ethereum hazitahitaji kuhifadhi nakala ya data yote ya hali ya Ethereum, na hivyo kupunguza sana mahitaji ya nafasi kwenye diski kuu. Nodi nyepesi zitatoa manufaa mengi ya kuendesha nodi kamili lakini zinaweza kuendeshwa kwa urahisi kwenye simu za mkononi au ndani ya programu rahisi za kivinjari.

Soma kuhusu Verkle trees

Kwa maboresho haya, vikwazo vya kuendesha nodi vinapunguzwa na kuwa karibu na sifuri. Watumiaji watafaidika na ufikiaji salama na usio na ruhusa wa Ethereum. Hawatalazimika kutumia nafasi kubwa ya diski au CPU kwenye kompyuta au simu zao, na hawatalazimika kutegemea wahusika wengine kupata data au ufikiaji wa mtandao wanapotumia programu.

Maendeleo ya sasa

Pochi za mkataba janja tayari zinapatikana, lakini maboresho zaidi yanahitajika ili kuzifanya zigatuliwe na zisiwe na ruhusa iwezekanavyo. EIP-4337 ni pendekezo lililokomaa ambalo halihitaji mabadiliko yoyote kwenye itifaki ya Ethereum. Mkataba-erevu mkuu unaohitajika kwa EIP-4337 ulizinduliwa Machi 2023.

Hali kamili ya kutohifadhi data bado iko katika hatua ya utafiti na huenda ikachukua miaka kadhaa kabla ya kutekelezwa. Kuna hatua kadhaa muhimu kuelekea hali kamili ya kutohifadhi data, ikiwemo uondoaji wa data, ambazo zinaweza kutekelezwa mapema zaidi. Vipengele vingine vya mkakati wa maendeleo, kama vile Verkle Trees na Mgawanyo wa Mpendekezaji-mjenzi vinahitaji kukamilishwa kwanza.

Mitandao ya majaribio ya Verkle tree tayari inafanya kazi. Hatua inayofuata ni kuendesha 'client' zinazotumia Verkle-tree kwenye mitandao ya majaribio ya faragha, na kisha ya umma. Unaweza kusaidia kuharakisha maendeleo kwa kupeleka mikataba kwenye mitandao ya majaribio au kuendesha wateja wa mitandao ya majaribio.

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 19 Julai 2024

Je! ukurasa huu umekusaidia?