Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Uondoji wa hisa

  • Sasisho la Shanghai/Capella liliwezesha uondoaji wa staking kwenye Ethereum
  • Waendeshaji wa validator lazima watoe anwani ya uondoaji ili kuwezesha
  • Zawadi zinasambazwa kiotomatiki kila baada ya siku chache
  • Validator wanaoacha kabisa staking watapokea salio lao lililobaki

Uondoaji wa staking unarejelea uhamisho wa ETH kutoka kwa akaunti ya mthibitishaji kwenye safu ya makubaliano ya Ethereum (Mnyororo Kioleza), hadi kwenye safu ya utekelezaji ambapo inaweza kufanyiwa miamala.

Malipo ya zawadi ya salio la ziada zaidi ya 32 ETH yatatumwa kiotomatiki na mara kwa mara kwa anwani ya uondoaji iliyounganishwa kwa kila mthibitishaji, pindi itakapowekwa na mtumiaji. Watumiaji wanaweza pia kuacha staking kabisa, na kufungua salio lao lote la mthibitishaji.

Zawadi za Kusimamisha

Malipo ya zawadi yanashughulikiwa kiotomatiki kwa akaunti za validator zinazofanya kazi na salio la juu la 32 ETH.

Salio lolote zaidi ya 32 ETH lililopatikana kupitia zawadi halichangii kwenye mtaji mkuu, au kuongeza uzito wa validator huyu kwenye mtandao, na hivyo hutolewa kiotomatiki kama malipo ya zawadi kila baada ya siku chache. Kando na kutoa anwani ya uondoaji mara moja, zawadi hizi hazihitaji hatua yoyote kutoka kwa mwendeshaji wa validator. Hii yote inaanzishwa kwenye safu ya makubaliano, hivyo hakuna gesi (ada ya muamala) inayohitajika katika hatua yoyote.

Tumefikaje hapa?

Katika miaka michache iliyopita, Ethereum imepitia maboresho kadhaa ya mtandao ikibadilika kuwa mtandao unaolindwa na ETH yenyewe, badala ya uchimbaji unaotumia nishati nyingi kama ilivyokuwa awali. Kushiriki katika makubaliano kwenye Ethereum sasa kunajulikana kama "staking", ambapo washiriki wamefunga ETH kwa hiari, kuiweka "hatarini" kwa uwezo wa kushiriki kwenye mtandao. Watumiaji wanaofuata sheria watapata zawadi, wakati majaribio ya kudanganya yanaweza kuadhibiwa.

Tangu kuzinduliwa kwa mkataba wa amana ya staking mnamo Novemba 2020, baadhi ya waanzilishi wa Ethereum wamefunga fedha kwa hiari ili kuanzisha "validators", akaunti maalum ambazo zina haki ya kuthibitisha na kupendekeza vitalu, zikifuata sheria za mtandao.

Kabla ya sasisho la Shanghai/Capella, hukuweza kutumia au kufikia ETH yako iliyowekwa kwenye staking. Lakini sasa, unaweza kuchagua kupokea zawadi zako kiotomatiki kwenye akaunti uliyochagua, na pia unaweza kutoa ETH yako iliyowekwa kwenye staking wakati wowote unapotaka.

Niandae vipi?

Waweka dhamana wa sasa

  • Baadhi ya watumiaji wametoa anwani ya utoaji yao ambapo mwanzo waliweka kiwango cha dhamana cha uwekaji - watumiaji hawa hawana cha kufanya zaidi
  • Waweka dhamana wengi hawakutoa anwani ya utoaji fedha kwenye uwekaji fedha wa kwanza, na watahitajika kuboresha hati zao za uondoaji. Jukwaa la kuweka dhamana lina maelekezo jinsi ya kufanya ivi

Unaweza ingiza namba yako ya mthibitishaji hapa kuona kama bado unahitaji kusahihisha hati zako(Hii unaweza kupata kwenye kumbukumbu za mteja wako):

Matangazo muhimu

Kutoa anwani ya uondoaji ni hatua inayohitajika kwa akaunti yoyote ya validator kabla ya kuwa na sifa ya kutoa ETH kutoka kwenye salio lake.

Hakuna tishio lolote kwa fedha zako kwa sasa kwa kutotoa hii, ikichukuliwa kuwa fungu la maneno yako ya mnemonic/msingi limebaki salama nje ya mtandao, na halijaathiriwa kwa njia yoyote. Kukosa kuongeza stakabadhi za uondoaji kutaacha tu ETH ikiwa imefungwa kwenye akaunti ya mthibitishaji kama ilivyokuwa hadi anwani ya uondoaji itakapotolewa.

Kuacha staking kabisa

Kutoa anwani ya uondoaji kunahitajika kabla fedha zozote haziwezi kuhamishwa kutoka kwa salio la akaunti ya mthibitishaji.

Watumiaji wanaotaka kuacha staking kabisa na kutoa salio lao lote lazima pia watie sahihi na kutangaza ujumbe wa "kujiondoa kwa hiari" na funguo za mthibitishaji ambao utaanza mchakato wa kujiondoa kwenye staking. Hii inafanywa na mteja wako wa kithibitishaji na kuwasilishwa kwenye nodi yako ya makubaliano, na haihitaji gesi.

Mchakato wa mthibitishaji kujiondoa kwenye staking huchukua muda tofauti, kulingana na wangapi wengine wanajiondoa kwa wakati mmoja. Mara tu itakapokamilika, akaunti hii haitawajibika tena kwa kutekeleza majukumu ya mtandao wa mthibitishaji, haistahiki tena zawadi, na haina tena ETH yake "iliyowekwa hisa". Kwa wakati huu akaunti itawekwa alama kuwa "inayoweza kutolewa" kikamilifu.

Mara tu akaunti itakapotiwa alama ya "inayoweza kutolewa", na stakabadhi za uondoaji zimetolewa, hakuna kingine ambacho mtumiaji anahitaji kufanya isipokuwa kusubiri. Akaunti hufagiliwa kiotomatiki na mfululizo na wapendekezaji wa bloku kwa ajili ya fedha zinazostahiki zilizotolewa, na salio la akaunti yako litahamishwa kikamilifu (pia inajulikana kama "uondoaji kamili") wakati wa ufagiaji unaofuata.

Uondoaji wa staking uliwashwa lini?

Utendaji wa uondoaji uliwezeshwa kama sehemu ya sasisho la Shanghai/Capella lililotokea tarehe 12 Aprili 2023.

Sasisho la Shanghai/Capella liliwezesha ETH iliyokuwa imewekwa hisa awali kurejeshwa kwenye akaunti za kawaida za Ethereum. Hii ilifunga mduara juu ya ukwasi wa staking, na kuleta Ethereum hatua moja karibu zaidi katika safari yake ya kujenga mfumo ikolojia endelevu, unaoweza kupanuka, na salama uliogatuliwa.

Malipo ya uondoaji hufanyaje kazi?

Iwapo mthibitishaji fulani anastahiki uondoaji au la huamuliwa na hali ya akaunti ya mthibitishaji yenyewe. Hakuna ingizo la mtumiaji linalohitajika wakati wowote ili kubaini kama akaunti inapaswa kuanzishiwa uondoaji au la—mchakato mzima unafanywa kiotomatiki na safu ya makubaliano katika mzunguko unaoendelea.

Wewe ni mwanafunzi wa kuona zaidi?

Angalia maelezo haya ya uondoaji wa staking wa Ethereum na Finematics:

"Ufagiaji" wa Mthibitishaji

Wakati mthibitishaji amepangiwa kupendekeza bloku inayofuata, inatakiwa kuunda foleni ya uondoaji, ya hadi uondoaji 16 unaostahiki. Hii inafanywa kwa kuanza na faharasa ya mthibitishaji 0, kubaini kama kuna uondoaji unaostahiki kwa akaunti hii kulingana na sheria za itifaki, na kuiongeza kwenye foleni ikiwa ipo. Seti ya mthibitishaji iliyopangwa kupendekeza bloku inayofuata itaendelea pale ambapo ya mwisho iliishia, ikiendelea kwa utaratibu bila kikomo.

Kukagua akaunti kwa ajili ya uondoaji

Wakati mpendekezaji anafagia wathibitishaji kwa ajili ya uondoaji unaowezekana, kila mthibitishaji anayekaguliwa anapimwa dhidi ya mfululizo mfupi wa maswali ili kubaini kama uondoaji unapaswa kuanzishwa, na ikiwa ndivyo, ni kiasi gani cha ETH kinapaswa kutolewa.

  1. Je, anwani ya uondoaji imetolewa? Ikiwa hakuna anwani ya uondoaji iliyotolewa, akaunti inarukwa na hakuna uondoaji unaoanzishwa.
  2. Je, mthibitishaji amejiondoa na anaweza kutoa? Ikiwa mthibitishaji amejiondoa kabisa, na tumefikia epoki ambapo akaunti yake inachukuliwa kuwa "inayoweza kutolewa", basi uondoaji kamili utachakatwa. Hii itahamisha salio lote lililobaki kwenye anwani ya uondoaji.
  3. Je, salio halisi limefikia kiwango cha juu cha 32? Ikiwa akaunti ina stakabadhi za uondoaji, haijatoka kikamilifu, na ina zawadi zaidi ya 32 zinazosubiri, uondoaji kiasi utachakatwa ambao utahamisha tu zawadi zilizo juu ya 32 kwenye anwani ya uondoaji ya mtumiaji.

Kuna vitendo viwili tu vinavyochukuliwa na waendeshaji wa vithibitishaji wakati wa mzunguko wa maisha wa mthibitishaji ambavyo huathiri mtiririko huu moja kwa moja:

  • Toa stakabadhi za uondoaji ili kuwezesha aina yoyote ya uondoaji
  • Toka kwenye mtandao, jambo ambalo litaanzisha uondoaji kamili

Bila gesi

Njia hii ya uondoaji wa staking huepuka kuwataka waweka hisa kuwasilisha muamala wao wenyewe wakiomba kiasi fulani cha ETH kitolewe. Hii inamaanisha hakuna gesi (ada ya muamala) inayohitajika, na uondoaji pia haushindani na nafasi iliyopo ya bloku ya safu ya utekelezaji.

Nitapata zawadi zangu za staking mara ngapi?

Uondoaji wa juu wa 16 unaweza kuchakatwa katika bloku moja. Kwa kiwango hicho, uondoaji wa wathibitishaji 115,200 unaweza kuchakatwa kwa siku (kwa kuchukulia hakuna nafasi zilizokosekana). Kama ilivyoelezwa hapo juu, wathibitishaji wasio na uondoaji unaostahiki watarukwa, na kupunguza muda wa kumaliza ufagiaji.

Kwa kupanua hesabu hii, tunaweza kukadiria muda utakaotumika kuchakata idadi fulani ya uondoaji:

Idadi ya uondoajiMuda wa kukamilisha
400,000siku 3.5
500,000siku 4.3
600,000siku 5.2
700,000siku 6.1
800,000siku 7.0

Kama unavyoona, hii hupungua kasi kadiri wathibitishaji wengi wanavyokuwa kwenye mtandao. Ongezeko la nafasi zilizokosekana linaweza kupunguza kasi hii kwa uwiano, lakini kwa ujumla hii itawakilisha upande wa polepole wa matokeo yanayowezekana.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Masomo zaidi

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 23 Februari 2026

Je! ukurasa huu umekusaidia?