Mpango wa Tafsiri
Mpango wa Tafsiri ni juhudi shirikishi ya kutafsiri ethereum.org katika lugha tofauti ili kufanya tovuti ipatikane zaidi na mabilioni ya watu wasiozungumza Kiingereza kote ulimwenguni.
Tusaidie kutafsiri
Mpango wa Tafsiri wa ethereum.org uko wazi na mtu yeyote anaweza kuchangia!
- Utahitaji kuingia katika akaunti yako ya Crowdin au ujisajili.
- Chagua lugha unayotaka kuchangia.
- Kabla ya kuanza, tafadhali angalia mwongozo wa Jinsi ya kutafsiri ili kujifunza jinsi ya kutumia Crowdin, na Mwongozo wa Mtindo wa Tafsiri kwa vidokezo na mbinu bora.
- Tafsiri za mashine hazitakubaliwa.
- Tafsiri zote hukaguliwa kabla ya kuongezwa kwenye tovuti, kwa hivyo kutakuwa na ucheleweshaji mfupi kabla ya tafsiri zako kuonekana.
Jiunge na Discord ya ethereum.org (opens in a new tab) ili kushirikiana kwenye tafsiri, kuuliza maswali, kushiriki maoni na mawazo, au kujiunga na kikundi cha tafsiri.
Anza kutafsiri (opens in a new tab)Kuhusu Mpango wa Tafsiri
Jamii ya Ethereu inalenga kuwa ya ulimwengu wote na inayojumuisha, japo maudhui yake yanahudumia wazungumzaji wa kiingereza tu, na ikiacha watu bilioni 6 wasiozungumza kiingereza. Ili Ethereum.org ifanye kazi kama lango la Ethereum kwa jamii duniani kote, tunaamini kutoa maudhui ya Ethereum kwa wasiozungumza kiingereza katika lugha zao ni kitu muhimu.
Programu ya Ufasiri wa ethereum.org unalenga kuifanya Ethereum kupatikana kwa kila mmoja kwa kufasiri ethereum.org na maudhui mengine ya Ethereum kwenda katika lugha nyingi iwezekanavyo.
Soma zaidi kuhusu dhamira na maono ya Mpango wa Tafsiri wa ethereum.org.
Maendeleo yetu hadi sasa
- 6,900 + watafsiri
- Lugha 68 ziko hai kwenye tovuti
- milioni 2.89 za maneno yaliyotafsiriwa mwaka wa 2024
Shukrani
Ethereum.org inatafsiriwa na maelfu ya wanajamii na wao ndio sehemu muhimu ya Mpango wa Tafsiri. Tunataka kuwashukuru watafsiri wetu na kuwaunga mkono katika njia zao za kikazi. Hizi ni baadhi ya shukrani zetu kwa watafsiri:
Cheti
Ikiwa umechangia katika Mpango wa Tafsiri na angalau maneno 5,000 uliyotafsiri yameidhinishwa, unastahiki cheti cha mtafsiri wa ethereum.org. Zaidi kuhusu vyeti
OATs
Wachangiaji katika Mpango wa Tafsiri wanastahiki OATs (tokeni za mafanikio za onchain) tofauti kulingana na idadi ya maneno waliyotafsiri mwaka wa 2024. OATs ni NFTs zinazothibitisha mchango wako kwa Mpango wa Tafsiri wa ethereum.org. Zaidi kuhusu OATs
Shukrani kwa watafsiri
Shukrani za hadharani kwa watafsiri wetu wakuu kwa kutumia bao za wanaoongoza na orodha ya wachangiaji wote kwenye Mpango wa Tafsiri.
Zawadi
Hapo awali, tumewazawadia wachangiaji wetu wenye bidii zaidi kwa kuwapa tiketi za mikutano ya Ethereum kama vile Devcon (opens in a new tab) na Devconnect (opens in a new tab), pamoja na bidhaa za kipekee za ethereum.org.
Tunafikiria kila mara njia mpya na bunifu za kuwazawadia wachangiaji wetu, kwa hivyo kaa nasi!
Miongozo na rasilimali
Ikiwa unachangia katika Mpango wa Tafsiri au unafikiria kujihusisha, unapaswa kuangalia miongozo ya tafsiri hapa chini:
- Mwongozo wa Mtindo wa Tafsiri – maagizo na vidokezo kwa watafsiri wa ethereum.org
- Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Tafsiri – maswali na majibu yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Mpango wa Tafsiri wa ethereum.org
- Mwongozo wa mhariri wa mtandaoni wa Crowdin (opens in a new tab) – mwongozo wa kina wa kutumia mhariri wa mtandaoni wa Crowdin na baadhi ya vipengele vya hali ya juu vya Crowdin
Kwa zana zingine muhimu za tafsiri, jumuiya za watafsiri na machapisho ya blogu ya Mpango wa Tafsiri, tafadhali tembelea ukurasa wa Rasilimali.
Wasiliana nasi
Je, una maswali yoyote? Au unataka kushirikiana na timu yetu na watafsiri wengine? Tafadhali chapisha katika chaneli ya #translations ya seva yetu ya Discord ya ethereum.org (opens in a new tab)
Unaweza pia kuwasiliana nasi kupitia translations@ethereum.org (opens email client)
Kuanzisha mpango wako wa tafsiri
Tumejitolea kutafsiri maudhui ya Ethereum katika lugha nyingi iwezekanavyo na kufanya maudhui ya kielimu yapatikane kwa kila mtu. Kulingana na mwelekeo wetu kwenye tafsiri, tunataka kusaidia miradi mingine ya Ethereum kupanga, kusimamia, na kuboresha juhudi zao za tafsiri.
Kwa sababu hii, tumeunda kitabu cha mwongozo cha Mpango wa Tafsiri ambacho kina vidokezo na mbinu bora tulizojifunza katika mchakato wa kutafsiri ethereum.org.
Unataka kushirikiana zaidi au kutumia baadhi ya rasilimali zetu za tafsiri? Una maoni yoyote kuhusu kitabu cha mwongozo? Tungependa kusikia kutoka kwako kupitia translations@ethereum.org (opens email client).
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 23 Februari 2026
