Ubao wa Viongozi wa Kutafsiri
Tunataka kuangazia watafsiri bora kulingana na shughuli za hivi karibuni na pia kuangazia wachangiaji wetu wenye athari kubwa zaidi wa wakati wote. Ubao wetu wa viongozi hufuatilia data kuhusu watafsiri wanaofanya kazi zaidi kwa kutumia mwonekano wa kila mwezi, kila robo mwaka na wa wakati wote, na husasishwa mwanzoni mwa kila mwezi. Watafsiri huwekwa kwenye mbao za viongozi kulingana na idadi yao ya maneno ''yaliyoshinda'' (idadi ya maneno yaliyotafsiriwa ambayo yameidhinishwa wakati wa ukaguzi).
Watafsiri wetu
Jamii ndio msingi wa Programu ya Kutafsiri ya ethereum.org. Gundua jamii yetu kamili ya watafsiri hapa chini.

Tazama watafsiri wote
Angalia orodha yetu kamili ya watafsiri wanaojitolea muda na ujuzi wao kusaidia kufanya maudhui ya Ethereum yapatikane kwa kila mtu.
Cheti
Tunataka kuwashukuru watafsiri wetu na kuwaunga mkono katika njia zao za kikazi. Kwa kuzingatia hili, tumeunda cheti cha mtafsiri cha ethereum.org.
Cheti hiki kimekusudiwa watafsiri wa kitaalamu na wanaochipukia ambao wanataka kukitumia kama rejeleo, kuthibitisha utaalamu wao katika kutafsiri maudhui ya kiufundi au kuonyesha tu kujitolea kwao kwa Ethereum.
Ikiwa umechangia kwenye Programu ya Kutafsiri na angalau maneno 5,000 uliyotafsiri yameidhinishwa, unaweza kuomba cheti chako cha mtafsiri kwa kutuandikia kwenye translations@ethereum.org. Ujumbe wako unapaswa kujumuisha kiungo cha akaunti yako ya Crowdin na jina lako kamili (au jina la utani, ukipenda), ambalo tutaliongeza kwenye cheti.

OATs
Wachangiaji kwenye Programu ya Kutafsiri wanastahiki kupata OATs (tokeni za mafanikio mnyororoni) tofauti – tokeni zisizoweza kubadilishwa ambazo zinathibitisha ushiriki wao katika Programu ya Kutafsiri ya ethereum.org.
Tuna idadi ya OATs tofauti zinazopatikana kwa watafsiri, kulingana na shughuli zao.
Ikiwa umechangia katika juhudi za kutafsiri kwenye Crowdin, una OAT inayokusubiri!
Jinsi ya kudai
- Jiunge na seva yetu ya Discord (opens in a new tab)
- Bandika kiungo cha akaunti yako ya Crowdin katika chaneli ya #🥇 | proof-of-contribution.
- Subiri mshiriki wa timu yetu akupe majukumu yanayohitajika ili kudai OATs zako.
- Dai OATs zako!
Unapaswa kutumia tu pochi za uhifadhi binafsi kudai OATs. Usitumie akaunti za ubadilishaji au akaunti zingine ambazo huna funguo za faragha, kwani hizi hazitakuruhusu kufikia na kudhibiti OATs zako.
