Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mwongozo wa kutafsiri ethereum.org

Ikiwa wewe ni mgeni kwenye Programu ya Kutafsiri na unasita kuanza, haya ni baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQs) yanayoweza kukusaidia kuanza. Tumia mwongozo huu kupata majibu ya maswali ya kawaida.

Je, ninaweza kulipwa kwa kutafsiri ethereum.org?

Ethereum.org ni tovuti ya chanzo wazi (open-source), ambayo inamaanisha kuwa mtu yeyote anaweza kushiriki na kuchangia.

Programu ya Kutafsiri ya ethereum.org ni mwendelezo wa hilo na imeandaliwa kwa kuzingatia falsafa sawa.

Lengo la Programu ya Kutafsiri ni kufanya maudhui ya Ethereum yapatikane kwa kila mtu, bila kujali lugha wanazozungumza. Pia inaruhusu mtu yeyote anayezungumza lugha mbili kushiriki katika mfumo wa ikolojia wa Ethereum na kuchangia kwa njia inayofikika.

Kwa sababu hii, Programu ya Kutafsiri iko wazi na ni ya hiari, na ushiriki haulipwi. Ikiwa tungewalipa watafsiri kwa idadi ya maneno wanayotafsiri, tungeweza tu kuwaalika wale walio na uzoefu wa kutosha wa kutafsiri (watafsiri wa kitaalamu) kujiunga na Programu ya Kutafsiri. Hili lingefanya Programu ya Kutafsiri iwe ya kibaguzi na kutuzuia kufikia malengo yaliyoainishwa, haswa: kuruhusu kila mtu kushiriki na kujihusisha na mfumo wa ikolojia.

Tunafanya kila jitihada kuwawezesha wachangiaji wetu kufanikiwa katika mfumo wa ikolojia wa Ethereum; motisha nyingi zisizo za kifedha zimewekwa kama vile: kutoa POAP na cheti cha mtafsiri, pamoja na kuandaa Bodi za Viongozi za Kutafsiri na kuorodhesha watafsiri wetu wote kwenye tovuti.

Je, ninatafsiri vipi tungo zenye <HTML tags>?

Sio kila tungo imeandikwa kwa muundo wa maandishi matupu. Kuna baadhi ya tungo zinazojumuisha hati mchanganyiko kama vile lebo za HTML (<0>, </0>). Hii kwa kawaida ni kwa ajili ya viungo au mitindo mbadala katikati ya sentensi.

  • Tafsiri maandishi yaliyo ndani ya lebo lakini sio lebo zenyewe. Chochote kilicho katika < na > hakipaswi kutafsiriwa au kuondolewa.
  • Ili kuweka tungo salama, tunapendekeza ubofye kitufe cha "Copy Source" (Nakili Chanzo) upande wa chini kushoto. Hii itanakili tungo asili na kuibandika kwenye kisanduku cha maandishi. Hii inakuwezesha kufafanua mahali lebo zilipo na inakusaidia kuepuka makosa.

Crowdin interface with copy source button highlighted

Unaweza kusogeza nafasi ya lebo ndani ya tungo ili kuifanya iwe ya asili zaidi katika lugha yako – hakikisha tu unasogeza lebo nzima.

Kwa maelezo ya kina zaidi kuhusu kushughulikia lebo na vijisehemu vya msimbo, tafadhali rejelea Mwongozo wa Mtindo wa Kutafsiri wa ethereum.org.

Tungo zinapatikana wapi?

Mara nyingi tungo chanzo pekee zinaweza zisiwe za kutosha kwako kutoa tafsiri sahihi.

  • Angalia "screenshots" (picha za skrini) na "context" (muktadha) kwa maelezo zaidi. Katika sehemu ya tungo chanzo, utaona picha ya skrini imeambatishwa ambayo itakuonyesha jinsi tunavyotumia tungo katika muktadha.
  • Ikiwa bado huna uhakika, inua bendera katika "comment section" (sehemu ya maoni). Huna uhakika jinsi ya kuacha maoni?

Showing how context can be provided for a string with a screenshot

An example screenshot added for context

Ninawezaje kuacha maoni au kuuliza maswali? Ningependa kuripoti suala au makosa ya chapa...

Ikiwa unataka kuripoti tungo fulani inayohitaji uangalizi, jisikie huru kuwasilisha maoni.

  • Bofya kitufe cha pili cha upau wa juu kulia. Kichupo kilichofichwa kitaonekana upande wako wa kulia. Acha maoni mapya na ubofye kisanduku cha kuteua cha "Issue" (Suala) chini. Unaweza kubainisha aina ya suala kwa kuchagua mojawapo ya chaguo kutoka kwenye menyu kunjuzi.
  • Baada ya kuwasilishwa, itaripotiwa kwa timu yetu. Tutasuluhisha suala hilo na kukujulisha kwa kujibu maoni yako na kufunga suala hilo.
  • Ikiwa utaripoti tafsiri isiyo sahihi, tafsiri na mbadala uliopendekeza vitakaguliwa na mzungumzaji asilia wakati wa ukaguzi unaofuata.

Showing how to make comments and issues

Kumbukumbu ya Kutafsiri (TM) ni nini?

Kumbukumbu ya Kutafsiri (TM) ni kipengele cha Crowdin kinachohifadhi tungo zote zilizotafsiriwa hapo awali kote kwenye ethereum.org. Wakati tungo inatafsiriwa, inahifadhiwa kiotomatiki kwenye TM ya mradi wetu. Hiki kinaweza kuwa chombo muhimu cha kukusaidia kuokoa muda wako!

  • Angalia sehemu ya "TM and MT Suggestions" (Mapendekezo ya TM na MT) na utaona jinsi watafsiri wengine walivyotafsiri tungo sawa au inayofanana. Ikiwa utapata pendekezo lenye kiwango cha juu cha kulingana, jisikie huru kurejelea tafsiri kwa kuibofya.
  • Ikiwa hakuna chochote kwenye orodha, unaweza kutafuta kwenye TM kwa tafsiri zilizofanywa hapo awali na kuzitumia tena kwa uthabiti.

A screenshot of the translation memory

Ninatumiaje faharasa ya Crowdin?

Istilahi za Ethereum ni sehemu nyingine muhimu ya kazi yetu ya kutafsiri kwani mara nyingi maneno mapya ya kiteknolojia yatakuwa bado hayajatafsiriwa katika lugha nyingi. Pia, kuna maneno ambayo yana maana tofauti katika muktadha tofauti. Zaidi kuhusu kutafsiri istilahi za Ethereum

Faharasa ya Crowdin ndio mahali pazuri pa kupata ufafanuzi wa maneno na fasili. Kuna njia mbili za kurejelea faharasa.

  • Kwanza, unapopata neno lililopigiwa mstari kwenye tungo chanzo, unaweza kuweka kipanya chako juu yake na kuona fasili fupi yake.

An example glossary definition

  • Pili, Ikiwa unaona neno ambalo hulifahamu lakini halijapigiwa mstari, unaweza kutafuta katika kichupo cha faharasa (kitufe cha tatu cha safu wima ya kulia). Utapata maelezo ya maneno maalum na yale yanayotumiwa mara kwa mara katika mradi.

A screenshot showing where to find the glossary tab in Crowdin

  • Ikiwa bado huwezi kuipata, ni nafasi yako ya kuongeza neno jipya! Tunakuhimiza ulitafute kwenye mtambo wa kutafuta na uongeze maelezo kwenye faharasa. Itakuwa msaada mkubwa kwa watafsiri wengine kuelewa neno hilo vizuri zaidi.

A screenshot showing how to add a glossary term to Crowdin

Sera ya kutafsiri istilahi

Kwa majina (chapa, kampuni, watu) na maneno mapya ya kiteknolojia (Mnyororo wa Beacon, minyororo ya shadi, n.k.)

Ethereum inawasilisha maneno mengi mapya ambayo yamebuniwa hivi karibuni. Baadhi ya maneno yatatofautiana kutoka kwa mtafsiri hadi mtafsiri kwani hakuna tafsiri rasmi katika lugha zao husika. Kutokubaliana kama huko kunaweza kusababisha kutoelewana na kupunguza usomaji.

Kutokana na utofauti wa lugha na viwango tofauti katika kila lugha, imekuwa karibu haiwezekani kuja na sera ya pamoja ya kutafsiri istilahi inayoweza kubadilishwa katika lugha zote zinazotumika.

Baada ya kuzingatia kwa uangalifu, tumefikia uamuzi wa kuacha istilahi zinazotumiwa mara kwa mara kwenu, watafsiri.

Hapa kuna kile tunachopendekeza, unapopata neno ambalo hulifahamu:

  • Rejelea Faharasa ya maneno, unaweza kupata jinsi watafsiri wengine walivyolitafsiri hapo awali. Ikiwa unafikiri neno lililotafsiriwa hapo awali halifai, jisikie huru kurejesha tafsiri yako kwa kuongeza neno jipya kwenye Faharasa ya Crowdin.
  • Ikiwa tafsiri kama hiyo ya awali haipo kwenye Faharasa, tunakuhimiza uitafute kwenye mtambo wa kutafuta au makala ya vyombo vya habari inayoonyesha jinsi neno hilo linavyotumiwa katika jamii yako.
  • Ikiwa hutapata marejeleo yoyote, jisikie huru kuamini angalizo lako na kupendekeza tafsiri mpya kwa lugha yako!
  • Ikiwa unajisikia huna ujasiri wa kufanya hivyo, acha neno hilo bila kutafsiriwa. Wakati mwingine, maneno ya Kiingereza yanatosha zaidi katika kutoa fasili sahihi.

Tunapendekeza uache majina ya chapa, kampuni, na wafanyakazi bila kutafsiriwa kwani tafsiri inaweza kusababisha mkanganyiko usio wa lazima na matatizo ya SEO.

Mchakato wa ukaguzi unafanyaje kazi?

Ili kuhakikisha kiwango fulani cha ubora na uthabiti katika tafsiri zetu, tunafanya kazi na Acolad (opens in a new tab), mmoja wa watoa huduma wakubwa wa lugha ulimwenguni. Acolad ina wataalamu wa lugha 20,000, ambayo inamaanisha kuwa wanaweza kutoa wakaguzi wa kitaalamu kwa kila lugha na aina ya maudhui tunayohitaji.

Mchakato wa ukaguzi ni wa moja kwa moja; mara tu seti ya maudhui inapotafsiriwa kwa 100%, tunaagiza ukaguzi kwa kundi hilo la maudhui. Mchakato wa ukaguzi unafanyika moja kwa moja katika Crowdin. Mara tu ukaguzi utakapokamilika, tunasasisha tovuti na maudhui yaliyotafsiriwa.

Ninawezaje kuongeza maudhui katika lugha yangu?

Kwa sasa, maudhui yote yasiyo ya Kiingereza yanatafsiriwa moja kwa moja kutoka kwa maudhui chanzo ya Kiingereza, na maudhui yoyote ambayo hayapo katika Kiingereza hayawezi kuongezwa kwa lugha nyingine.

Ili kupendekeza maudhui mapya kwa ethereum.org, unaweza kuunda suala (opens in a new tab) kwenye GitHub. Ikiwa yataongezwa, maudhui yataandikwa kwa Kiingereza na kutafsiriwa kwa lugha nyingine kwa kutumia Crowdin.

Tunapanga kuongeza usaidizi wa nyongeza za maudhui yasiyo ya Kiingereza katika siku za usoni.

Wasiliana nasi

Asante kwa kusoma haya yote. Tunatumai hii inakusaidia kujiunga na programu yetu. Jisikie huru kujiunga na chaneli yetu ya kutafsiri ya Discord (opens in a new tab) ili kuuliza maswali na kushirikiana na watafsiri wengine, au wasiliana nasi kupitia translations@ethereum.org (opens email client)!