Jinsi ya kubadili tokeni
Umechoshwa na kutafuta soko ambalo linaorodhesha tokeni zako zote uzipendazo? Unaweza kubadilishana tokeni nyingi kwa kutumia .
Kubadilishana tokeni kunahusisha ubadilishanaji wa mali mbili tofauti zilizopo kwenye mtandao wa Ethereum, kwa mfano kubadilishana ETH kwa DAI (tokeni ya ). Mchakato huu ni wa haraka na bei nafuu. Utahitaji kuwa na mkoba wa kripto kubadilisha tokeni.
Vigezo vya Awali:
- kuwa na ; kama huna, unaweza kufuata mwongozo huu kuhusu jinsi ya kufungua akaunti ya Ethereum
- weka fedha kwenye mkoba wako
1. Unganisha mkoba wako kwenye soko la kubadilishana tokeni lililoondolewa mfumo wa kati (DEX) unalolipenda
Baadhi ya masoko maarufu ya kubadilishana ni:
- Uniswap (opens in a new tab)
- Sushiswap (opens in a new tab)
- 1Inch (opens in a new tab)
- Curve (opens in a new tab)
Inavutia? Jifunze zaidi kuhusu fedha zilizogatuliwa (DeFi) ni nini na jinsi aina hizi mpya za masoko ya kubadilishana zinavyofanya kazi.
2. Chagua jozi ya tokeni unazotaka kubadilisha
Kwa mfano, ETH na DAI. Hakikisha una fedha kati ya mojawapo ya tokeni hizo mbili.

3. Ingiza kiasi cha tokeni unachotaka kubadilisha na bonyeza badilisha
Soko la kubadilishana litahesabu kiotomatiki idadi ya tokeni utakazopata.
4. Thibitisha muamala
Hakiki maelezo ya muamala. Kagua kiwango cha ubadilishaji na ada zingine zozote ili kuzuia mshangao mbaya.
5. Subiri muamala uchakatwe
Unaweza kuona maendeleo ya muamala kwenye kipelelezi cha kiambajengo chochote. Mchakato huu hautakiwi kuchukua muda zaidi ya dakika 10.
Utapokea kiotomatiki tokeni ulizobadilisha kwenye mkoba wako mara tu muamala utakapochakatwa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, ninaweza kubadilisha ETH kwa BTC kutoka kwenye mkoba wangu?
Hapana, unaweza tu kubadilisha tokeni ambazo ni za asili ya mtandao wa Ethereum, kama vile ETH, tokeni za ERC-20 au NFTs. Unaweza tu kubadilisha aina za Bitcoin zilizofungwa ambazo zinapatikana kwenye Ethereum.
Slippage ni nini?
Ni tofauti kati ya kiwango chako cha ubadilishaji unachotarajia na kiwango halisi.
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 18 Oktoba 2025

