Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 15 Februari 2026

Utangulizi wa mikataba-erevu

Mikataba ya busara ndio msingi wa safu ya maombi ya Ethereum. Hizi ni programu za kompyuta zilizohifadhiwa kwenye zinazofuata mantiki ya "ikiwa hii basi ile", na zimehakikishwa kutekelezwa kulingana na sheria zilizobainishwa na msimbo wake, ambao hauwezi kubadilishwa pindi unapoundwa.

Nick Szabo aliunda neno "mkataba mahiri". Mnamo 1994, aliandika utangulizi wa dhana hiyo (opens in a new tab), na mnamo 1996 aliandika uchunguzi wa kile ambacho mikataba-erevu ingeweza kufanya (opens in a new tab).

Szabo alitazamia soko la kidijitali ambapo michakato ya kiotomatiki, huwezesha miamala na shughuli za kibiashara kufanyika bila wasuluhishi wanaoaminika. Mikataba erevu katika sarafu ya kidigitali imeweka maono haya katika vitendo.

Tazama Finematics ikielezea mikataba mahiri:

Uaminifu katika mikataba ya kawaida

Moja ya tatizo kubwa katika mikataba ya jadi ni hitaji la watu wanaoaminika kufuata matokeo ya mkataba.

Huu ni mfano moja wapo:

Alice na Bob wana mashindano ya baiskeli. Tuseme Alice aliweka dau la $10 kuwa Bob ataibuka mshindi katika mashindano hayo. Bob anajiamini atakuwa mshindi na anakubaliana na dau lililowekwa. Mwishoni, Alice anamaliza mashindano mbele ya Bob na kuibuka mshindi. Lakini Bob anakataa kulipa dau na kulaumu kuwa Alice anaweza kuwa kadanganya.

Mfano huu unaonesha shida iliyopo katika makubaliano yasiyo ya busara au erevu. Hata kama masharti ya makubaliano yatatimizwa (yaani, wewe ndiye mshindi wa mbio), bado lazima umwamini mtu mwingine kutimiza makubaliano (yaani, malipo ya dau).

Mashine ya kuuza ya kidijitali

Msemo rahisi wa mkataba mahiri ni mashine ya kuuza, ambayo hufanya kazi kwa kiasi fulani sawa na mkataba mahiri ingizao mahususi uhakikisa matokeo yaliyoamiliwa mapema.

  • Umechagua bidhaa
  • Mashine ya kuuza inaonesha bei
  • Unalipia bei
  • Mashine ya kuuza inadhibitisha umelipa kiasi sahihi
  • Mashine ya kuuza inakupa bidhaa yako

Mashine ya kuuza itatoa tu bidhaa unayoitaka baada ya mahitaji yote kutekelezwa. Kama usipochagua bidhaa au kuweka pesa za kutosha, mashine ya kuuzia haitokupa bidhaa yako.

Utekelezaji wa kiotomatiki

Faida kuu ya mkataba mahiri ni kuwa hutekeleza msimbo usio na utata endapo masharti fulani yakitimizwa. Hakuna haja ya kusubiri binadamu kutafsiri au kuridhia matokeo. Hii inaondoa uhitaji wa wapatanishi wanao aminika.

Kwamfano unaweza kuandika mkataba mahiri unaohifadhi pesa za escrow kwa watoto, kuwaruhusu kutoa pesa baada ya kipindi fulani. Kama wakijaribu kiutoa kabla ya tarehe husika, mkataba mahiri hautoruhusu pesa kutolewa. Au unaweza kuandika mkataba ambao unaweza kukupa toleo la kidigitali la jina la gari unapomlipa muuzaji.

Matokeo yanayotabirika

Mikataba ya jadi ina utata kwasababu hutegemea binadamu kutafsiri na kuitekeleza. Kwamfano, majaji wawili wanaweza kutafsiri mkataba tofauti, ambapo huweza kusababisha maamuzi yasiyokuwa na usahihi na matokeo yasiyo na usawa. Mkataba-erevu huondoa uwezekano huu. Badala yake, Mkataba-erevu hutekeleza kwa usahihi kulingana na masharti yaliyoandikwa ndani ya kanuni za mkataba. Usahihi huu unamaana kuwa kwa kuzingatia hali sawa, Mkataba-erevu unaweza kutoa majibu sawa.

Rekodi ya umma

Mkataba-erevu hutumika katika ukaguzi na ufuatiliaji. Kwakuwa mikataba erevu ya Ethereum ipo katika mnyororo wa bloku katika umma, mtu yeyote anaweza kufuatilia uhamishaji wa mali papo hapo na taarifa nyingine zinazo husiana. Kwa mfano, unaweza kuangalia na kuona mtu akituma pesa katika anwani yako.

Ulinzi wa faragha

Mkataba-erevu pia hulinda faragha. Kwakuwa Ethereum ni mtandao usiojulikana (miamala yako inahusiswa hadharani na anwani ya pekee ya siri na si utambulisho wako) unaweza kulinda faragha zako kwa watazamaji.

Masharti yanayoonekana

Hatimaye, kama mikataba ya jadi unaweza kuona mkataba-erevu ni nini nkabla ya kujisajili (au kujihusisha nayo). Uwazi wa Mkataba-erevu unaruhusu mtu yeyote kuichunguza.

Matumizi ya mkataba-erevu

Mkataba-erevu inaweza kufanya chochote ambacho program za kompyuta zinaweza kufanya.

Zinaweza kufanya hesabu, kuunda sarafu, kuhifadhi data, kuunda , kutuma mawasiliano na hata kutengeneza michoro. Hii ni mifano ya ulimwengu halisi:

Masomo zaidi

Pima uelewaji wako wa Ethereum

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 15 Februari 2026

Je! makala haya yamekusaidia?