Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 23 Februari 2026

Matumizi ya nishati ya Ethereum

Ethereum ni Mnyororo wa bloku ambao ni nafuu kwa mazingara. Utaratibu wa makubaliano wa uthibitishaji-wa-dau wa Ethereum hutumia ETH badala ya nishati kuulinda mtandao. Matumizi ya nishati ya Ethereum ni takribani ~0.0026 TWh/mwakaopens in a new tab katika mtandao mzima wa kimataifa.

Makadirio ya matumizi ya nishati kwa Ethereum yanatokana na utafiti wa CCRI (Crypto Carbon Ratings Institute)opens in a new tab. Walitoa makadirio ya chini-juu ya matumizi ya umeme na kiwango cha kaboni cha mtandao wa Ethereum (tazama ripotiopens in a new tab). Walipima matumizi ya umeme ya nodi tofauti zenye usanidi mbalimbali wa maunzi na programu za wateja. Makadirio ya 2,601 MWh (0.0026 TWh) kwa matumizi ya umeme ya kila mwaka ya mtandao yanalingana na utoaji wa kaboni wa kila mwaka wa tani 870 za CO2e kwa kutumia vipengele vya kiwango cha kaboni maalum kwa eneo. Thamani hii hubadilika nodi zinapoingia na kutoka kwenye mtandao - unaweza kufuatilia kwa kutumia makadirio ya wastani wa siku 7 kutoka kwa Cambridge Blockchain network Sustainability Indexopens in a new tab (kumbuka kuwa wanatumia mbinu tofauti kidogo kwa makadirio yao - maelezo yanapatikana kwenye tovuti yao).

Ili kuweka matumizi ya nishati ya Ethereum katika muktadha, tunaweza kulinganisha makadirio ya mwaka kwa baadhi ya bidhaa na viwanda vingine. Hii hutusaidia kuelewa vizuri zaidi kama makadirio ya Ethereum ni ya juu au ya chini.

Annual Energy Consumption in TWh/yr

Chati iliyo hapo juu inaonyesha makadirio ya matumizi ya nishati katika TWh/mwaka kwa Ethereum, ikilinganishwa na bidhaa na viwanda vingine kadhaa. Makadirio yaliyotolewa yanatokana na maelezo yanayopatikana hadharani, yaliyofikiwa Julai 2023, pamoja na viungo vya vyanzo vinavyopatikana kwenye jedwali lililo hapa chini.

Matumizi ya nishati ya mwaka (TWh)Ulinganisho na PoS EthereumChanzo
Kituo cha data cha Kimataifa19073,000xchanzoopens in a new tab
Bitcoin14953,000xchanzoopens in a new tab
Uchimbaji wa Dhahabu13150,000xchanzoopens in a new tab
Michezo ya video nchini Marekani*3413,000xchanzoopens in a new tab
PoW Ethereum218,100xchanzoopens in a new tab
Google197,300xchanzoopens in a new tab
Netflix0.457176xchanzoopens in a new tab
PayPal0.26100xchanzoopens in a new tab
AirBnB0.028xchanzoopens in a new tab
PoS Ethereum0.00261xchanzoopens in a new tab

*Inajumuisha vifaa vya watumiaji wa mwisho kama vile Kompyuta, kompyuta mpakato, na koni za michezo.

Kupata makadirio sahihi ya matumizi ya nishati ni ngumu, hasa wakati kile kinachopimwa kina mnyororo mgumu wa ugavi au maelezo ya upelekaji ambayo huathiri ufanisi wake. Kwa mfano, makadirio ya matumizi ya nishati kwa Netflix na Google hutofautiana kulingana na kama yanajumuisha tu nishati inayotumiwa kudumisha mifumo yao na kuwasilisha maudhui kwa watumiaji (matumizi ya moja kwa moja) au kama yanajumuisha matumizi yanayohitajika kutengeneza maudhui, kuendesha ofisi za kampuni, kutangaza, n.k. (matumizi yasiyo ya moja kwa moja). Matumizi yasiyo ya moja kwa moja yanaweza pia kujumuisha nishati inayohitajika kutumia maudhui kwenye vifaa vya mtumiaji wa mwisho kama vile runinga, kompyuta na simu za mkononi.

Makadirio yaliyo hapo juu si ulinganisho kamili. Kiasi cha matumizi yasiyo ya moja kwa moja kinachohesabiwa hutofautiana kulingana na chanzo, na mara chache hujumuisha nishati kutoka kwa vifaa vya mtumiaji wa mwisho. Kila chanzo msingi kinajumuisha maelezo zaidi kuhusu kile kinachopimwa.

Jedwali na chati hapo juu pia zinajumuisha ulinganisho na Bitcoin na Ethereum ya uthibitishaji-wa-kazi. Ni muhimu kutambua kuwa matumizi ya nishati ya mitandao ya uthibitishaji-wa-kazi si thabiti na hubadilika kila siku. Makadirio yanaweza pia kutofautiana sana kati ya vyanzo. Mada hii huvutia mjadalaopens in a new tab wenye undani, sio tu kuhusu kiasi cha nishati inayotumiwa, lakini pia kuhusu vyanzo vya nishati hiyo na maadili yanayohusiana. Matumizi ya nishati si lazima yalingane moja kwa moja na athari za kimazingira kwa sababu miradi tofauti inaweza kutumia vyanzo tofauti vya nishati, ikiwa ni pamoja na sehemu ndogo au kubwa zaidi ya nishati mbadala. Kwa mfano, Cambridge Bitcoin Electricity Consumption Indexopens in a new tab inaonyesha kuwa mahitaji ya mtandao wa Bitcoin kinadharia yanaweza kuendeshwa kwa gesi inayochomwa au umeme ambao ungepotea katika usafirishaji na usambazaji. Njia ya Ethereum kuelekea uendelevu ilikuwa ni kubadilisha sehemu ya mtandao inayotumia nishati nyingi na mbadala wa kijani.

Unaweza kuvinjari makadirio ya matumizi ya nishati na utoaji wa kaboni kwa viwanda vingi kwenye tovuti ya Cambridge Blockchain Network Sustainability Indexopens in a new tab.

Makadirio kwa kila muamala

Makala nyingi hukadiria matumizi ya nishati "kwa kila muamala" kwa minyororo ya bloku. Hii inaweza kupotosha kwa sababu nishati inayohitajika kupendekeza na kuthibitisha bloku haitegemei idadi ya miamala ndani yake. Kitengo cha matumizi ya nishati kwa kila muamala kinamaanisha kuwa miamala michache ingesababisha matumizi madogo ya nishati na kinyume chake, jambo ambalo si kweli. Pia, makadirio ya kila muamala ni nyeti sana kwa jinsi upitishaji wa miamala wa mnyororo wa bloku unavyofafanuliwa, na kurekebisha ufafanuzi huu kunaweza kutumiwa vibaya ili kufanya thamani ionekane kubwa au ndogo.

Kwenye Ethereum, kwa mfano, upitishaji wa miamala sio tu ule wa safu ya msingi - pia ni jumla ya upitishaji wa miamala wa unda-mpya zake zote za "safu ya 2". Safu za 2 kwa ujumla hazijumuishwi katika mahesabu, lakini kujumuisha nishati ya ziada inayotumiwa na waratibu wa mfuatano (kidogo) na idadi ya miamala wanayochakata (kubwa) kunaweza kupunguza sana makadirio ya kila muamala. Hii ni sababu mojawapo kwa nini ulinganisho wa matumizi ya nishati kwa kila muamala katika mifumo tofauti unaweza kupotosha.

Deni la kaboni la Ethereum

Matumizi ya nishati ya Ethereum ni ya chini sana, lakini haikuwa hivi siku zote. Ethereum hapo awali ilitumia uthibitishaji-wa-kazi ambayo ilikuwa na gharama kubwa zaidi ya kimazingira kuliko utaratibu wa sasa wa uthibitishaji-wa-dau.

Tangu mwanzo kabisa, Ethereum ilipanga kutekeleza utaratibu wa makubaliano unaotegemea uthibitishaji-wa-dau, lakini kufanya hivyo bila kuathiri usalama na ugatuzi kulichukua miaka ya utafiti na maendeleo ya kina. Kwa hivyo, utaratibu wa uthibitishaji-wa-kazi ulitumika kuanzisha mtandao. Uthibitishaji-wa-kazi huhitaji wachimbaji kutumia vifaa vyao vya kompyuta kukokotoa thamani, wakitumia nishati katika mchakato huo.

Kulinganisha matumizi ya nishati ya Ethereum kabla na baada ya Muungano, kwa kutumia Mnara wa Eiffel (urefu wa mita 330) upande wa kushoto kuashiria matumizi makubwa ya nishati kabla ya Muungano, na sanamu ndogo ya Lego ya urefu wa sentimita 4 upande wa kulia kuwakilisha upungufu mkubwa wa matumizi ya nishati baada ya Muungano

CCRI inakadiria kuwa Muungano ulipunguza matumizi ya umeme ya mwaka ya Ethereum kwa zaidi ya 99.988%. Vile vile, kiwango cha kaboni cha Ethereum kilipungua kwa takribani 99.992% (kutoka tani 11,016,000 hadi tani 870 za CO2e). Ili kuweka hili katika muktadha, upungufu wa hewa chafu ni kama kutoka urefu wa Mnara wa Eiffel hadi sanamu ndogo ya kuchezea ya plastiki, kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio hapo juu. Matokeo yake, gharama ya kimazingira ya kuulinda mtandao imepungua sana. Wakati huo huo, usalama wa mtandao unaaminika kuboreka.

Safu ya programu ya kijani

Wakati matumizi ya nishati ya Ethereum ni ya chini sana, pia kuna jumuiya kubwa, inayokua, na yenye shughuli nyingi ya fedha za kuzalisha upya (ReFi) inayojengwa kwenye Ethereum. Programu za ReFi hutumia vipengele vya DeFi kujenga programu za kifedha ambazo zina athari chanya za nje zinazofaidisha mazingira. ReFi ni sehemu ya harakati pana ya "solarpunk"opens in a new tab ambayo inalingana kwa karibu na Ethereum na inalenga kuunganisha maendeleo ya kiteknolojia na utunzaji wa mazingira. Hali ya ugatuzi, isiyo na ruhusa, na inayoweza kuundwa ya Ethereum inaifanya kuwa safu ya msingi inayofaa kwa jumuiya za ReFi na solarpunk.

Mifumo asili ya Web3 ya kufadhili bidhaa za umma kama vile Gitcoinopens in a new tab huendesha raundi za hali ya hewa ili kuchochea ujenzi unaozingatia mazingira kwenye safu ya programu ya Ethereum. Kupitia maendeleo ya mipango hii (na mingine, k.m., DeSci), Ethereum inakuwa teknolojia yenye matokeo chanya kwa mazingira na jamii.

Masomo zaidi

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 23 Februari 2026

Je! makala haya yamekusaidia?