ReFi ni nini?
Fedha za ufufuaji (refi) ni seti ya zana na mawazo yaliyojengwa juu ya , ambayo yanalenga kuunda chumi ambazo ni za ufufuaji, badala ya zile za unyonyaji au uchimbaji. Hatimaye, mifumo ya uchimbaji humaliza rasilimali zilizopo na kuporomoka; bila mifumo ya ufufuaji, inakosa ustahimilivu. ReFi inafanya kazi kwa dhana kwamba uundaji wa thamani ya kifedha lazima utenganishwe na uchimbaji usio endelevu wa rasilimali kutoka kwa sayari na jamii zetu.
Badala yake, ReFi inalenga kutatua matatizo ya kimazingira, kijamii, au ya kijumuia kwa kuunda mizunguko ya ufufuaji. Mifumo hii inaunda thamani kwa washiriki huku ikinufaisha mifumo ya ikolojia na jamii kwa wakati mmoja.
Moja ya misingi ya ReFi ni dhana ya uchumi wa ufufuaji iliyoanzishwa na John Fullerton wa Taasisi ya Capital. Alipendekeza kanuni nane zinazounganishwa (opens in a new tab) ambazo zinasimamia afya ya kimfumo:
Miradi ya ReFi inatekeleza kanuni hizi kwa kutumia na programu za ili kuhamasisha tabia za ufufuaji, k.m., kurejesha mifumo ya ikolojia iliyoharibiwa, na kuwezesha ushirikiano mkubwa kwenye masuala ya kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi na upotevu wa bioanuwai.
ReFi pia inaingiliana na vuguvugu la sayansi iliyogatuliwa (desci), ambalo linatumia Ethereum kama jukwaa la kufadhili, kuunda, kukagua, kutoa mikopo, kuhifadhi, na kusambaza maarifa ya kisayansi. Zana za DeSci zinaweza kuwa muhimu kwa kuunda viwango na mbinu zinazoweza kuthibitishwa kwa ajili ya kutekeleza na kufuatilia shughuli za ufufuaji kama vile kupanda miti, kuondoa plastiki baharini, au kurejesha mfumo wa ikolojia ulioharibiwa.
Uundaji wa tokeni wa salio la kaboni
Soko la hiari la kaboni (VCM) (opens in a new tab) ni utaratibu wa kufadhili miradi inayoleta athari chanya iliyothibitishwa kwenye uzalishaji wa kaboni, iwe kwa kupunguza uzalishaji unaoendelea, au kuondoa gesi chafu ambazo tayari zimetolewa kwenye angahewa. Miradi hii hupokea rasilimali inayoitwa "salio la kaboni" baada ya kuthibitishwa, ambayo wanaweza kuiuza kwa watu binafsi na mashirika yanayotaka kuunga mkono hatua za tabianchi.
Mbali na VCM, pia kuna masoko kadhaa ya kaboni yaliyoamriwa na serikali ('masoko ya kufuata sheria') ambayo yanalenga kuanzisha bei ya kaboni kupitia sheria au kanuni ndani ya mamlaka fulani (k.m., nchi au kanda), kudhibiti usambazaji wa vibali vitakavyosambazwa. Masoko ya kufuata sheria huwahamasisha wachafuzi ndani ya mamlaka yao kupunguza uzalishaji, lakini hayana uwezo wa kuondoa gesi chafu ambazo tayari zimetolewa.
Licha ya maendeleo yake katika miongo ya hivi karibuni, VCM inaendelea kukabiliwa na masuala mbalimbali:
- Ukwasi uliogawanyika sana
- Taratibu za muamala zisizo wazi
- Ada kubwa
- Kasi ndogo sana ya biashara
- Ukosefu wa uwezo wa kuongezeka
Kubadilisha VCM kwenda kwenye soko jipya la kidijitali la kaboni (DCM) linalotegemea mnyororo wa vitalu inaweza kuwa fursa ya kuboresha teknolojia iliyopo kwa ajili ya kuthibitisha, kufanya miamala na kutumia salio la kaboni. Minyororo ya vitalu inaruhusu data inayoweza kuthibitishwa na umma, ufikiaji kwa watumiaji wengi, na ukwasi zaidi.
Miradi ya ReFi inatumia teknolojia ya mnyororo wa vitalu kupunguza matatizo mengi ya soko la jadi:
- Ukwasi umejikita katika idadi ndogo ya mabwawa ya ukwasi ambayo yanaweza kuuzwa kwa uhuru na mtu yeyote. Mashirika makubwa pamoja na watumiaji binafsi wanaweza kutumia mabwawa haya bila kutafuta wauzaji/wanunuzi kwa mikono, ada za ushiriki, au usajili wa awali.
- Miamala yote inarekodiwa kwenye minyororo ya vitalu ya umma. Njia ambayo kila salio la kaboni inachukua kutokana na shughuli za biashara inaweza kufuatiliwa milele mara tu inapopatikana katika DCM.
- Kasi ya muamala ni karibu ya papo hapo. Kupata kiasi kikubwa cha salio la kaboni kupitia masoko ya zamani kunaweza kuchukua siku au wiki, lakini hii inaweza kufikiwa kwa sekunde chache katika DCM.
- Shughuli za biashara hufanyika bila waamuzi, ambao hutoza ada kubwa. Salio la kaboni la kidijitali linawakilisha upunguzaji mkubwa wa gharama ikilinganishwa na salio la jadi.
- DCM ina uwezo wa kuongezeka na inaweza kukidhi mahitaji ya watu binafsi na mashirika ya kimataifa kwa pamoja.
Vipengele muhimu vya DCM
Vipengele vinne vikuu vinaunda mandhari ya sasa ya DCM:
- Sajili kama vile Verra (opens in a new tab) na Gold Standard (opens in a new tab) zinahakikisha kuwa miradi inayounda salio la kaboni ni ya kuaminika. Pia zinaendesha hifadhidata ambazo salio la kaboni la kidijitali linatoka na linaweza kuhamishwa au kutumika (kustaafishwa).
Kuna wimbi jipya la miradi ya kibunifu inayojengwa kwenye minyororo ya vitalu ambayo inajaribu kuvuruga makampuni yaliyopo katika sekta hii.
- Madaraja ya kaboni, yanayojulikana pia kama waundaji wa tokeni, hutoa teknolojia ya kuwakilisha au kuhamisha salio la kaboni kutoka kwenye sajili za jadi kwenda kwenye DCM. Mifano mashuhuri ni pamoja na Toucan Protocol (opens in a new tab), C3 (opens in a new tab), na Moss.Earth (opens in a new tab).
- Huduma zilizounganishwa hutoa salio la kuepuka na/au kuondoa kaboni kwa watumiaji wa mwisho ili waweze kudai faida ya kimazingira ya salio na kushiriki uungaji mkono wao wa hatua za tabianchi na ulimwengu.
Baadhi kama vile Klima Infinity (opens in a new tab) na Senken (opens in a new tab) hutoa aina mbalimbali za miradi iliyotengenezwa na wahusika wengine na kutolewa chini ya viwango vilivyoanzishwa kama Verra; wengine kama Nori (opens in a new tab) hutoa tu miradi maalum iliyotengenezwa chini ya kiwango chao wenyewe cha salio la kaboni, ambacho wanatoa na ambacho wana soko lao maalum.
- Njia na miundombinu ya msingi inayowezesha kuongeza athari na ufanisi wa mnyororo mzima wa usambazaji wa soko la kaboni. KlimaDAO (opens in a new tab) hutoa ukwasi kama bidhaa ya umma (ikiruhusu mtu yeyote kununua au kuuza salio la kaboni kwa bei ya wazi), inahamasisha kuongezeka kwa uwezo wa upitishaji wa masoko ya kaboni na kustaafu kwa zawadi, na hutoa zana zinazoingiliana ambazo ni rahisi kutumia ili kufikia data kuhusu, pamoja na kupata na kustaafisha, aina mbalimbali za salio la kaboni lililoundwa kuwa tokeni.
ReFi zaidi ya masoko ya kaboni
Ingawa kwa sasa kuna msisitizo mkubwa kwenye masoko ya kaboni kwa ujumla na kubadilisha VCM kwenda DCM hasa ndani ya nafasi hii, neno "ReFi" halikomei tu kwenye kaboni. Rasilimali nyingine za kimazingira zaidi ya salio la kaboni zinaweza kutengenezwa na kuundwa kuwa tokeni, ambayo itamaanisha athari nyingine mbaya za nje pia zinaweza kuwekewa bei ndani ya tabaka za msingi za mifumo ya kiuchumi ya baadaye. Zaidi ya hayo, kipengele cha ufufuaji cha mtindo huu wa kiuchumi kinaweza kutumika katika maeneo mengine, kama vile ufadhili wa bidhaa za umma kupitia majukwaa ya ufadhili wa kipeo cha pili kama vile Gitcoin (opens in a new tab). Mashirika ambayo yamejengwa juu ya wazo la ushiriki wa wazi na usambazaji sawa wa rasilimali huwezesha kila mtu kuelekeza pesa kwenye miradi ya programu huria, pamoja na miradi ya kielimu, kimazingira, na inayoendeshwa na jamii.
Kwa kubadilisha mwelekeo wa mtaji kutoka kwenye mazoea ya uchimbaji kuelekea kwenye mtiririko wa ufufuaji, miradi na makampuni yanayotoa faida za kijamii, kimazingira, au za kijumuia—na ambayo yanaweza kushindwa kupata ufadhili katika fedha za jadi—yanaweza kuanza na kuzalisha athari chanya za nje kwa jamii kwa haraka na kwa urahisi zaidi. Kubadilika kwenda kwenye mtindo huu wa ufadhili pia kunafungua mlango kwa mifumo ya kiuchumi inayojumuisha zaidi, ambapo watu wa demografia zote wanaweza kuwa washiriki hai badala ya kuwa watazamaji tu. ReFi inatoa maono ya Ethereum kama utaratibu wa kuratibu hatua juu ya changamoto za kuwepo zinazokabili spishi zetu na maisha yote kwenye sayari yetu—kama tabaka la msingi la dhana mpya ya kiuchumi, kuwezesha mustakabali unaojumuisha zaidi na endelevu kwa karne nyingi zijazo.
Usomaji wa ziada kuhusu ReFi
- Muhtasari wa kiwango cha juu wa sarafu za kaboni na nafasi yake katika uchumi (opens in a new tab)
- Wizara ya Mustakabali, riwaya inayoonyesha jukumu la sarafu inayoungwa mkono na kaboni katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi (opens in a new tab)
- Ripoti ya kina ya Kikosi Kazi cha Kuongeza Masoko ya Hiari ya Kaboni (opens in a new tab)
- Ingizo la Faharasa ya CoinMarketCap la Kevin Owocki na Evan Miyazono kuhusu ReFi (opens in a new tab)

